Somaliland yapiga kura katika uchaguzi wa urais
Shughuli ya kupiga kura imeanza katika Jamhuri iliojitangaza ya Somaliland katika uchaguzi wa urais.
Uchaguzi huo utatumia mfumo wa kiteknolijia wa kutambua macho ya kila mpiga kura ikiwa ni mara ya kwanza duniani kulingana na msemaji wa uchaguzi.
Zaidi ya wapiga kura 700,000 watapiga kura katika uchaguzi ulio na wagombea watatu.
Takriban wachunguzi 60 wapo nchini humo kuangalia uchaguzi huo.
Mmoja ya wachunguzi Susan Mwape kutoka Zambia aliambia BBC kwamba watachunguza kila kitu katika uchaguzi huo ikiwemo utendaji kazi wa maafisa wa shirika linalosimamia uchaguzi huo.
Rashid Abdi kutoka shirila la kitaifa la Crisis aliambia BBC kwamba iwapo Somalia itafanikiwa kufanya uchaguzi huo kuwa huru na wazi basi itaimarisha uwezo wake wa kutaka kuwa taifa huru.
Ameitetea serikali kwa kuzima mitandao ya kijamii ili kuzuia kusambaa kwa habari bandia na zile zisizosahihi wakati wa kipindi chote cha uchaguzi.
Somaliland ilijitangaza kuwa huru baada ya kupinduliwa kwa aliyekuwa rais wa Somalia Siad Barre 1991.
Somaliland yapiga kura katika uchaguzi wa urais
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 13, 2017
Rating:
Hakuna maoni