HABARI ZA JUMATATU HII


Seebait.com 2016

.
.

Monday, 26 December 2016

Magufuli awataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo ambaye alikuwa chini ya malezi ya fundi seremala.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli ametoa rai hiyo (jana) katika Kanisa la Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu mjini Singida katika kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
“Katika kipindi cha maisha yake Yesu Kristo hapa duniani, mbali ya kwamba alizaliwa na mfanyakazi, Joseph seremala, lakini na yeye alishiriki katika kufanya kazi, basi niwaombe watanzania wote tuchape kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure,” alisema Rais Magufuli. 
Pia amewataka watanzania kuimarisha upendo, kuvumiliana, na kutobaguana, kwani upendo utalisaidia taifa kupata maendeleo huku akiwakumbusha waumini kuwa Yesu Kristo hakuwa CHADEMA wala CCM bali alikuwa ni wa watu wote.
Rais Magufuli ambaye aliambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, katika ibada hiyo amesema, kusali ni moja ya nguzo muhimu ambayo Wakristo wote wanapaswa kutekeleza ili kuhakikisha taifa linaendelea kubakia katika hali ya amani na utulivu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo.
Aidha, Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wakulima kote nchini kuhakikisha wanazitumia vizuri mvua za sasa katika shughuli za kilimo pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame

Monday, December 26, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Disemba 26



Monday, December 26, 2016

Picha 15: Vodacom Wasafi Festival Ilivyofanyika Dec 25 Mkoani Iringa

Usiku wa Dec 25, 2016  wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Q Boy, Chege pamoja na msanii kutoka Nigeria Kcee wameandika historia katika mkoa wa Iringa.


Show hiyo iliyopewa jina la Vodacom Wasafi Festival imefanyika katika uwanja wa Samora Stadium, hizi ni baadhi ya picha kutoka mahali palipofanyika tamasha hilo.

Monday, December 26, 2016

Michezo: Haji Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro Kwa Rais Wa TFF

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa soka la Bongo.

Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai mwaka huu.

Manara katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.

"Nimekaa nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika Manara

Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba".

manara amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.

Kwa upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini yeye na Haji Manara.

Monday, December 26, 2016

Rais Magufuli Atoboa Siri ya Kula Christmass Mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini Singida mwaka huu.

Ametaja siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja (hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia kushinda uchaguzi huo.

Rais Magufuli ametoa siri hiyo jana  wakati akizungumza kwenye sherehe ya Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.

Akifafanua, alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.

“Hiyo ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.

Katika hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima, wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili ukame.

“Ndugu zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi. Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi … na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.

Akiijengea nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku wakijua hakuna cha bure.

Aidha, Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.

Awali askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira, ili yaweze kuwatunza na wao.

Alisema hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.

“Mimi nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira, ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.

Monday, December 26, 2016

Michezo: Ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Disemba 30

Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.
 
KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
 
KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.
 
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP
30/12/2016 Taifa ya Jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.
 
1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.
 
2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
 
3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
 
4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
 
5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
 
6/1/2017 Taifa ya Jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
 
7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
 
8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.
 
10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainali ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainali ya pili.
 
13/1/2017 Fainali saa 2: 30 usiku.


Monday, December 26, 2016

Michezo: TFF Yasema Mechi ya Simba na Yanga iko palepale

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ya mzunguko wa pili kati ya Simba na Yanga iliyokuwa imepangwa kuchezwa Februari 18 mwaka 2017 iko palepale kwa kuwa bado halijafikiria kuibadili tarehe hiyo.

Hatua hiyo inatokana na tarehe hiyo kugongana na kalenda ya CAF ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyotolewa hivi karibuni na kuipanga Yanga kucheza mchezo wa marudiano kati yake na Ngaya de Mbe ya Comoro kati ya tarehe 17, 18 na 19 mwezi Februari 2017.

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa hadi sasa shirikisho hilo kupitia Bodi ya Ligi halijafikiria kufanya mabadiliko yoyote kwenye ratiba hiyo, na kwamba ratiba itaendelea kubaki kama ilivyo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

"Ratiba imeshapangwa na haitabadilika, kila timu inajua itacheza lini, kuhusu ratiba ya CAF haiwezi kutuzuia kufanya mashindano yetu, kama kuna timu inacheza CAF inatakiwa ijipange, kila timu inatakiwa kuwa tayari wakati wowote ndiyo maana zinafanya matayarisho, zinaajiri makocha, zinasajili wachezaji , hiyo yote ni matayarisho kwahiyo sidhani kama watahitaji kupumzika na kutuharibia ratiba" Amesema Lucas

Jumatatu iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura akiwa kwenye kipindi cha 5Sports cha EATV, alisisitiza kuwa katika mzunguko wa pili wa ligi, ratiba haitakuwa tatizo, na kwamba haitabadilishwa badilishwa kwa kuwa katika upangaji wake kila kitu kilizingatiwa ikiwemo kalenda ya CAF.

Jumatatu, 26 Desemba 2016

MAN UNITED YAPATA USHINDI WA NNE MFULULIZO LIGI KUU YA UINGEREZA

Manchester United imepata ushindi wa nne mfululizo wa Ligi Kuu ya Uingereza katika mchezo walioutawala dhidi ya Sunderland inayobakia katika mstari wa kushuka daraja baada ya kulala kwa magoli 3-1.

Manchester United iliyostahili ushindi iliutawala mchezo huo kwa asilimia 63, ilipiga mashuti 25 kwenye goli, lakini zilikuwa jitihada za beki Daley Blind zilizozaa matunda na kuipatia goli la kwanza kufuatia pasi ya Zlatan Ibrahimovic.

Katika kipindi cha pili Zlatan Ibrahimovic aliongeza goli la pili akinasa pasi ya Paul Pogba huku Henrikh Mkhitaryan aliyetokea benchi akifunga goli la kisigino licha ya kuonekana ameotea.
                     Zlatan Ibrahimovic akianza kushangilia goli wakati mpira ukielekea wavuni
                          Mchezaji raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan akifunga goli kwa kisigino

OLIVER GIROUD AIPATIA ARSENAL USHINDI KATIKA DAKIKA ZA MWISHO

Mshambuliaji wa Arsenal Oliveir Giroud amefunga goli la ushindi katika dakika za mwisho na kumaliza gundu la kufungwa michezo miwili ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa ushindi dhidi ya West Brom.

Giroud alianza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza katika msimu huu, na alifanikiwa kufunga kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi ya Mesut Ozil katika dakika ya 86 ya mchezo huo.

Hadi Arsenal inapata goli hilo ilikuwa inaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 80, lakini ilikuwa na wakati mgumu kufanikiwa kutikisa nyavu za West Brom kazi kubwa akifanya kipa Ben Foster.
                     Olivier Giroud akiwa ameupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli pekee 
Aaron Ramsey akishangilia kuona mpira wa kichwa uliopigwa na Giroud ukitinga wavuni

RC GAMBO AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Arushaa ofisini kwake juzi kutoka vyombo mbalimba vya habari kuhusu sakata la kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV Halfani Liundi ambapo amehaidi kulishughulikia huku akiwataka waandishi kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mwandishi wa kituo cha ITV Halfani Liundi aliyekamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi, ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na hivyo mwandishi anauhuru wa kwenda popote kupata taarifa yeyote kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari
Mwandishi wa habari wa kituo cha channel Ten Aristrides Dotto akichangia katika mkutano huo wa waandishi wa habari na mkuu wa Mkoa juzi ofisinii kwake jijini Arusha
                                         Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mosses Mashalla akichangia katika mkutano huo wa mkuu wa Mkoa na waandishi wa habari mkoa wa Arusha. (Picha zote na Pamela Mollel)

Jumatatu, 26 Desemba 2016

MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHALANGWA MAPANGA NA MWALIMU

Mwanafunzi Marco Limbe akiwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa panga na Mwalimu Pendo Gabriel
Mwalimu Pendo Gabriel akiwa naye amelazwa baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira

Na Shushu Joel, BUSEGA

MWANAFUNZI Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega.

Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona akiwa na panga na kuanza kumchalanga”

Nilikimbia katika tukio na kutoa msaada kwa wote lakini mara watu walijaa na kuanza kumshambua mwalimu Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo lilikwama mara baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho mshemas bahai.

Mwandishi alikwenda katika kituo cha afya cha Nyashimo na kujionea hali mbaya kwa kijana Limbe ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 bila kujitambua na huku akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni mwalimu Gabriel naye akipata matibabu ya jeraha lake kichwani amabolo alishambuliwa na wananchi na huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la piolisi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio mwenyekiti wa Sogesca Bahai Mshemas alisema kuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa yesu imekuwa ni mbaya katika kijiji chake mara baada ya wananchi walio na hasira kali kufanya shambulio la kumshambulia mwalimu Pendo kwa kosa la kumchalanga na panga mwanafunzi wake aliyekuwa akitokea kwenye malisho na kupita karibu na shamba lake la mahindi.



Aliongeza kuwa alifanikiwa kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza kufanya mikakati ya kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za matibabu.

Aidha Mshemasi aliongeza kuwa walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili mwalimu pamoja na mwanafunzi.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk Ayubu Ismail alithibitisha kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana limbe ndiye aliyekuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu pendo.

Aliongeza kuwa kijana ameshonwa nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na majeraha na huku mwalimu yeye akiwa ameshonwa nyuzi 6.

ni kweli Limbe alikuwa ametokwa na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri alisema Dk Ismail”

NYOTA WA POP GEORGE MICHAEL AFARIKI DUNIA



Mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop George Michael amefariki dunia jana baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi akiwa nyumbani kwake huko Oxfordshire Uingereza.
Mwanamuziki huyo aliyeanza muziki katika miaka 80, na kupata mafanikio zaidi akiimaba peke yake nje ya bendi, amefariki dunia kwa amani jana siku ya Krismasi, kwa mujibu wa msemaji wake.


Mwanamuziki mwenzake wa zamani wa bendi ya Wham! Andrew Ridgeley amesema amevunjika moyo kuwa kumpoteza rafiki yake kipenzi.
           George Michael akiwa na Andrew Ridgeley wakiimba pamoja na bendi ya Wham !
Picha hii inaaminika kuwa ni picha ya mwisho kupiga George Michael hii ilikuwa Septemba mwaka huu akipata mlo wa usiku na rafiki yake
                                  Pata wimbo maarufu wa George Michael wa Careless Whisper

 
https://youtu.be/izGwDsrQ1eQ

habari za kimataifa

Wazamiaji wa Urusi wamepata mabaki ya ndege ya kijeshi iliyoanguka katika bahari nyeusi ikiwa na watu 92. Mabaki ya ndege hiyo yako katika kina cha mita 27 sawa na maili moja kutoka usawa wa bahari , amesema Rimma Chernova , msemaji wa operesheni ya msako na uokozi iliyoko mjini Sochi ikiongozwa na wizara ya masuala ya dharura ya Urusi. Mashirika ya habari ya Urusi hapo kabla yalimnukuu afisa ambaye hakutajwa akisema kwamba sehemu ya mbele ya ndege hiyo imepatikana, taarifa ambayo maafisa wa mji huo hawakuithibitisha wakati walipozungumza na shirika la habari la afp.Chernova aliongeza kusema kwamba wazamiaji wanapanga kutumia mashine maalum kuangalia ukubwa wa mabaki hayo na mahali yalipo ili kuweza kufahamu hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani Dan Kurtzer ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Israel amesema lugha chafu ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baada ya azimio la Umoja wa mataifa kushutumu ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi , haikubaliki. Dan Kurtzer ambaye alikuwa balozi wa Marekani nchini Israel wakati wa utawala wa rais George W Bush ameiambia redio ya Israel kwamba lugha inayotumiwa dhidi ya rais wa Marekani haikubaliki na haipaswi kutumiwa na mshirika hata kama amekasirika. Netanyahu amemshutumu rais anayeondoka madarakani Barack Obama jana usiku kwa kuwa nyuma ya azimio hilo , akiongeza kwamba Israel haina shaka kwamba utawala wa Obama ulianzisha , kusimamia ,na kuratibu juu ya maelezo yake na kutaka azimio hilo lipitishwe. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa liliidhinisha azimio ambalo linashutumu ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina na kuitaka Israel kusitisha hatua hiyo.
Maafisa nchini Syria wamewashutumu wapiganaji waasi kwa kuwauwa raia 21 , ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, kwa kuwapiga risasi wakati wakiondoka kutoka mji wa Aleppo wiki iliyopita. Miili ya watu hao ilipatikana katika vitongoji viwili mashariki mwa Aleppo. Mkuu wa kitengo cha kuchunguza ushahidi wa maeneo yanayotokea uhalifu mjini Aleppo zaher Hajjo aliliambia shirika la habari la Syria SANA kwamba miili ya raia 21 , ikiwa ni pamoja na watoto watano na wanawake wanne , waliouliwa na makundi ya magaidi, ilifukuliwa.Hajjo alinukuliwa akisema kwamba miili hiyo ilipatikana katika jela iliyokuwa ikiendeshwa na makundi ya kigaidi katika maeneo ya Sukkari na al-Kalasseh , na ilionekana kwamba watu hao walipigwa risasi kwa karibu.
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameshambulia soko la kuuza ng'ombe leo mjini Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria , mji ambao umekumbwa na mashambulio mengi zaidi katika mapambano ya miaka saba yanayofanywa na wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram. Polisi wamesema mshambuliaji huyo ambaye alikuwa ni mwanamke , ambaye alishambulia soko la Kasuwan Shanu katika wilaya ya kati ya kasuwa, alikuwa mtu pekee aliyeuwawa katika mripuko huo leo.Katika taarifa , polisi ilisema mwanamke wa pili ambaye alikuwa na bomu aliuwawa na kundi la watu karibu na eneo hilo, na majeshi ya usalama yalifanikiwa baadaye kuripua bomu hilo. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini lina alama zote za kundi la Boko Haram na linakuja siku chache baada ya rais Muhammadu Buhari kusema kambi muhimu ya kundi hilo katika ngome yao kuu iliyobakia imekamatwa.


Wanamgambo kutoka katika kundi la kabila la Nande katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewauwa raia 13 ikiwa ni pamoja na mtoto kutoka katika jamii ya Wahutu katika jimbo lisilo la utulivu la Kivu ya kaskazini. Afisa wa eneo hilo Alphonse Mahano ameliambia shirika la habari la AFP kuwa operesheni ya kijeshi kuzuwia mauaji holela yaliyotokea katika kipindi cha sikukuu ya Krismass yamesababisha wapiganaji watatu wa kabila la Nande kuuwawa. Maafisa wa eneo hilo hata hivyo hawakusema iwapo mashambulizi hayo mawili yanahusiana. Waathirika wa mauaji ya hivi karibuni ni watu wa kabila la wahutu. Wanamgambo wa Mai Mai Mazembe kutoka kabila la Nande na washirika wao walishambulia kijiji cha Nyanzale asubuhi ya Jumapili, na jeshi liliingilia kati kurejesha utulivu, amesema msemaji wa jeshi Guillaume Djike, na kuongeza kwamba wanamgambo sita wa kabila la Nande waliuwawa. Kiasi ya raia 35 waliuwawa katika jimbo la Kivu ya kaskazini mwishoni mwa juma.


Majeshi ya Iraq yataanza hatua ya kusongambele dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu ndani ya mji wa Mosul katika siku zijazo, amesema kamanda wa majeshi ya Marekani , katika awamu mpya ya operesheni ya miezi miwili ambayo itashuhudia majeshi ya Marekani yakiwekwa karibu na eneo la mapambano katika mji huo.Mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul yanayohusisha wanajeshi 100,000 wa Iraq, wapiganaji wa kundi la majeshi ya usalama ya Wakurdi na wanamgambo wa Kishia ni operesheni kubwa ya ardhini ya kijeshi nchini Iraq tangu uvamizi nchini Iraq uliofanywa na majeshi ya muungano ulioongozwa na Marekani mwaka 2003. Majeshi ya Iraq yamekomboa robo ya mji wa Mosul, ngome kuu ya wapiganaji wa jihadi nchini Iraq.

YANGA SASA WADAI MILIONI 420 ZA AZAM TFF

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM KATIKA hali inayoashiria ni kuyumba kiuchumi, klabu ya Yanga imeandika barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitaka ilipwe malimbikizo ya fedha zake za haki ya matangazo ya Televisheni ya Azam TV, Sh. Milioni 372. Kwa ujumla Yanga inataka ilipwe Sh. Milioni 422 pamoja na Sh. Milioni 50 za kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC). Yanga haikupewa zawadi yake ya kutwaa ubingwa wa Kombe la ASFC Mei mwaka huu ikiwafunga Azam FC 3-0 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga pia ilisusa kuchukua mgawo wa haki za matangazo ya Televisheni kwa miaka yote mitatu baada ya kutoridhia mkataba wa TFF na Azam TV.
Lakini katika hali ya kustaajabisha ghafla Yanga wameibua na kuiandikia barua bodi ya Ligi ya TFF kuomba malimbikizo ya fedha zake hizo, Sh. Milioni 372.  Habari za ndani ambazo Bin Zubeiry Sports - Online imezipata zimesema kwamba Bodi ya Ligi baada ya kupata barua hiyo ya Yanga waliwajibu wakiitaka klabu hiyo kwanza iandike barua ya kuutambua na kuukubali mkataba huo wa Azam TV ndipo utaratibu wa malipo yao ufanyike. Bodi ya Ligi bado inasubiri sasa barua kutoka Yanga wakiikubali Azam TV kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ili utaratibu wa malipo yao uanze. Na hatua ya Yanga kudai fedha hizo inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na matatizo hadi ya kulipa mishahara ya wachezaji. Inadaiwa wachezaji wa Yanga walipitisha miezi mitatu bila kulipwa mishahara kati ya Julai na Septemba na hiyo inatajwa kama sababu ya timu kufanya vibaya kwenye mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika. Aidha, wiki iliyopita wachezaji wa Yanga waligoma kwa simu mbili kufanya mazoezi, Jumatatu na Jumanne wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya Novemba. Kwa ujumla hali ya kiuchumi si njema ndani ya Yanga tangu kuondoka kwa waliokuwa wadhamini wakuu, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) waliokuwa wakiidhamini klabu hiyo pamoja na mahasimu, Simba kupitia bia ya Kilimanjaro.   Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alipotafutwa katika simu yake alisema hawezi kuzungumza chochote kwa leo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi. “Jamani hata siku za sikukuu pia mnatupigia simu?”alihoji Baraka na baada ya kuuliwa kuhusu klabu kuiandikia barua Bodi ya Ligi ya TFF kudai malimbikizo ya fedha za Azam TV, alisema; “We nani kakuambia, kwanza siwezi kuzungumza chochote nipo nje ya ofisi, nipigie kesho nikiwa ofisini,”alisema. 
CHANZO DW,MPEKUZI,RWEYUNGA.
HABARI ZA JUMATATU HII HABARI ZA JUMATATU HII Reviewed by RICH VOICE on Desemba 26, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...