JUMATANO HABARI ZA LEO HIZI HAPA

 

 

 

Jumatano, 21 Desemba 2016

KUWAIT YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA UJENZI WA BARABARA MKOANI TABORA

Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Mohammad Rashid Alamiri (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Kikao kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, kuhusu miradi ya miundombinu itakayofadhiliwa na Mfuko huo, ukiwemo mradi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora. Kulia ni mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini Bw. Mohammad Rashid Alamiri, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na wajumbe hao ambapo mbali na kutoa mkopo wa ujenzi wa barabara kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora, walionesha nia ya kutoa mikopo mingine yenye masharti nafuu katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania. Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Bw. Mohammad Rashid Alamiri huku wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mkunano kati yao uliojikita katika mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara na sekta ya afya, Mkutano huo umefanyikaatika Makao makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Wataalamu toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (kushoto) na wataalamu kutoka Tanzania (kulia) wakijadili kuhusu mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Kuwait, utakao saidia kujenga barabara Mkoani Tabora, Mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
 
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa dola za Kimarekani Milioni 34 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Bw. Mohammad Rashid Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, ulipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.

Dkt. Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi maeneo hayo kutokana na umuhimu wa barabara katika kukuza uchumi wa Taifa.

Amesema kuwa kipande hicho cha barabara kutoka Chaya hadi Nyahua, ambacho kiko Barabara Kuu itokayo Dar es salaam kwenda katika mikoa ya Tabora na Kigoma, licha ya umuhimu wake katika kukuza biashara na usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani, ilikuwa haijapata fedha kwa ajili ya ujenzi wake.

“Riba waliyoiweka mezani kwa mazungumzo ni asilimia 2 lakini nimewaomba waangalie uwezekano wa kuiteremsha walau ifikie asilimia 1.5 na wamependekeza kipindi cha kuanza kulipa mkopo kiwe miaka ishirini ijayo lakini nimewaomba wasogeze hadi kufikia miaka 25 kama ilivyo kwa mradi wa Hospitali ya Mnazimmoja” aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango amesema Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake huo wa Maendeleo wameonesha nia ya kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyoko Visiwani Zanzibar.

“Nawahakikishia kuwa baada ya muda si mrefu wananchi wa mikoa ya Tabora na Kigoma watarajie kuona mkandarasi akiingia kazini ili kujenga barabara hii muhimu sana kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt. Mpango.

Ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo kutoka Chaya hadi Nyahua unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 61 lakini Kuwait haitatoa fedha zote hivyo ameuomba Mfuko huo uangalie uwezekano wa kutoa kiasi hicho chote cha fedha ili uweze kukamilika mapema.

 

Jumatano, 21 Desemba 2016

WANANCHI KATA ZA KIPUNGUNI, KIVULE NA MZINGA WAPEWA ELIMU KUPINGA UKEKETAJI

Anna Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Muwasilishaji wa mada, Bi. Agnes Lukanga (kulia mbele) kutoka TGNP Mtandao akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Muwasilishaji wa mada, Bi. Agnes Lukanga (kulia mbele) kutoka TGNP Mtandao akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Mmoja wa viongozi wa Dini, Issa Abdullah (mbele) akijadili jambo katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa viongozi wa Dini, Issa Abdullah (mbele) akijadili jambo katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia) akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia) akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Shina namba Saba Majohe, Mohamed Kassim (mbele) akichangia jambo katika mkutano huo wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Shina namba Saba Majohe, Mohamed Kassim (mbele) akichangia jambo katika mkutano huo wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.

 

Wednesday, December 21, 2016

Rais Magufuli Akataa Shule Kuitwa Jina Lake


Rais John Magufuli amekataa shule ya msingi iliyojengwa hivi karibuni eneo la Bunju, Wilaya ya Kinondoni kuitwa kwa jina lake badala yake ameagiza iitwe kwa jina la Mkuu wa wilaya hiyo, Ally Hapi. 
Taarifa ya badiliko la jina haikutolewa na Idara ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kama ilivyozoeleka bali na mkuu wa wilaya hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa uongozi wa shule hiyo. 
“Shule hii imejengwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Serikali Kuu kubana matumizi. Tukaamua iitwe John Magufuli lakini yeye akatoa agizo shule ipewe jina la mkuu wa wilaya sina budi kukubaliana na hilo,” alisema Hapi. 
Shule hiyo mpya iliyopo Bunju jijini imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Bunju A ambayo ilikuwa na wanafunzi 3,224.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo mpya, Ali Mwakapalila alisema ingawa inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 9 mwakani inakabiliwa na changamoto mbalimbali. 
“Hakuna umeme wala maji, hii inaweza kuleta madhara kwa wanafunzi hasa linapokuja suala la matumizi ya vyoo,” alisema. 
Baada ya hafla hiyo, Hapi alikwenda kwenye kiwanda cha saruji cha Twiga Cement ambako alipokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa na majengo mengine. 
Akipokea msaada huo, Hapi alisema msaada kutoka Twiga Cement unaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoipa sekta ya elimu kipaumbele ili kuhakikisha inatolewa katika mazingira bora. 
“Msaada huu umekuja muda muafaka. Tumeshajenga shule ila tunataka kuongeza madarasa, maabara, ofisi ya elimu na kuzungushia uzio ili watoto wawe katika mazingira salama. Lengo ni kuifanya shule hii iwe ya kisasa na itakuwa mfano kwa shule zote za Wilaya ya Kinondoni,” alieleza. 
Pia, Hapi alisema wilaya hiyo ipo kwenye mipango ya kujenga maktaba ya kisasa kwa kushirikiana na kampuni hiyo ya saruji. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Alfonso Velez alisema kuchangia katika shughuli za kijamii ni moja ya mambo ambayo wamekuwa wakiyapa kipaumbele zaidi. 
“Kushiriki shughuli za maendeleo katika jamii ni jambo ambalo tunalipenda zaidi. Yalipo maendeleo Twiga Cement ipo pia,” alisema Velez.

 

Wednesday, December 21, 2016

Rais wa Gambia: Hakuna wa kunitoa Madarakani, labda Mungu Pekee

Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa eneo la magharibi mwa Afrika la kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mpinzani wake, Adama Barrow.

Akihutubia Wanachama wa Muungano nchini humo Bw. Jammeh amesema: ”Waje wajaribu kuniondoa wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi”.

“Mimi sio muasi, haki yangu haiwezi kuvurugwa. Hii ni nafasi yangu, hakuna mtu anayeweza kuniondoa labda Mungu,” amesema.

Amesema kuwa alikataa wito wa Muungano wa Viongozi wa Mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.

“’Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu,” amesema na kuwashutumu viongozi hao kwa kuingilia mambo ya ndani ya Gambia.

ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua Bw. Barrow kama Rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.

Viongozi wa eneo hilo watahudhuria kuapishwa kwa Bw. Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.

Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo mnamo Desemba 1, 2016 lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha Mungu kwa madai kuwa matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.
 
 

Wednesday, December 21, 2016

Majambazi Wawili Wauawa Jijini Mbeya Katika Mapambano Makali Kati Yao Na Jeshi La Polisi

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi katika mapambano ya kurushiana risasi na watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi na kuua wawili kati yao.

Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari imesema kuwa mnamo tarehe 19.12.2016 majira ya saa 1:45 jioni katika Kijiji cha Busisya, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi walipata taarifa za siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha ambao walikuwa na lengo la kufanya uvamizi katika Duka la Mfanyabiashara wa soda na bia za jumla ambaye pia ni wakala wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao.

Askari hao walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 1:45 jioni askari walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki ambapo baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari walianza kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi hao.

Askari walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo hapo na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.

Aidha katika tukio hilo silaha bunduki tatu pamoja na risasi tisa ziliweza kupatikana zilizokuwa zinatumiwa na majambazi hayo. Silaha hizo ni Mark IV yenye namba 38482 na risasi mbili, Short Gun Greener yenye namba G.73878 na risasi 01 na Gobole lililotengenezwa kienyeji ambalo halina namba na risasi 06.

Pia baada ya kupekuliwa majambazi hao walikutwa na vitu vingine ambavyo ni Rungu moja, Praizi moja, Bisibisi moja, mafuta ya cherehani, koti la ngozi rangi ya brown pamoja na begi dogo rangi nyeusi ambalo lilitumika kuhifadhi vitu hivyo.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Makandana Wilaya ya Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu na bado haijatambulika. Msako unaendelea. Katika tukio hilo hakuna mali iliyoporwa wala askari kupata madhara. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea, Upelelezi unaendelea.

Wednesday, December 21, 2016

Maoni Sheria ya Huduma za Habari mwisho Januari 10


Wednesday, December 21, 2016

Wizara yalaani Ukeketaji wa Watoto maeneo ya Kivule, Dar es Salaam

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakemea vikali vitendo vya ukeketaji vinavyotaarifiwa kufanyika katika Kata ya Kivule, Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, na mikoa mengine ambayo imekaririwa na vyombo vya habari.

Wizara inaagiza wazazi na walezi kuacha mara moja vitendo vya ukeketaji kwani ni ukatili, husababisha madhara kwa watoto wa kike na wasichana ni kosa la jinai.

Athari za ukeketaji kwa wahanga ni pamoja na kusababisha majeraha kwa watoto, vifo, vilema, maradhi kama fistula na mengineyo. Watoto wa kike na wanawake wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa vitendo vya ukeketaji bila ridhaa yao na wakati mwingine ridhaa hiyo huwa imepatikana kwa hila, jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wizara inatoa rai kwa vyombo vya dola kuwakamata wazazi, walezi, mangariba, na wote wanaoendeleza vitendo vya ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wasichana katika kata ya Kivule na maeneo mengine nchini, na kuwafikisha mahakamani ili sheria iwezekuchukua mkondo wake.

Wizara itaendelea kupambana na vitendo vya ukeketaji vinavyotaarifiwa katika jamii zetu, na itaongeza juhudi ya utoaji elimu kwa jamii sambamba na kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na mila potofu ya ukeketaji.

Wito unatolewa kwa kila mwananchi kushiriki katika kuzuia vitendo vya ukeketaji na hasa kufichua matukio ya ukeketaji, na kutoa ushahidi mahakamani ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Wizara inatoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii katika Mikoa, Halmashauri na Kata katika maeneo ambako kunaarifiwa kuwepo vitendo vya ukeketaji kuhakikisha kuwa wanashirikiana na mamlaka husika kuzuia ukatili huo katika nchi yetu.



Msemaji wa Wizara-Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto

21/12/2016

Wednesday, December 21, 2016

Jeshi la Polisi Lasema Linaendelea kuchunguza alipo msaidizi wa Mbowe, Ben Saanane.......Latoa ufafanuzi kuhusu maiti saba

Ukiwa umetimia mwezi mmoja, baada ya Msaidizi wa Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benard Saanane (pichani) kupotea, Jeshi la Polisi limesema linachunguza taarifa za kupotea kwake ambazo ilizopokea kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama rafiki wa Saanane Desemba, 5, 2016.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Desemba 21, 2016 Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz amesema Jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi na kwamba taratibu za kiupelelezi za mtu aliyepotea zilifuatwa na bado upelelezi wa suala hilo unaendelea.

“Tuanashukuru wananchi wanaotupatia taarifa kuhusu tukio hilo, tunaahidi kwamba taarifa hizo tutazifanyia kazi. Tunazidi kuwaomba wananchi wenye taarifa za kupotea Saanane waziwasilishe katika kituo chochote cha polisi,” amesema.

Sambamba na hilo, Kamishna Boaz amefafanua tukio la uzikwaji wa maiti saba zilizokufa maji katika mto Ruvu, pasipo kufanyiwa uchunguzi wa kutambua waliokufa na chanzo cha vifo vyao.

“Mtakumbuka kati ya tarehe 6 hadi 12, 1016 huko mto Ruvu jeshi la polisi lilipata taarifa ya kuonekana maiti saba zikiwa zinaelea mtoni kwa nyakati na maeneo mbalimbali, baada ya taarifa hizo kupatikana askari na daktari walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitaalamu,” amesema na kuongeza.

“Kutokana na ukweli kwamba baadhi ya maiti zilikuwa zimeharibika, maiti 6 ziliamuliwa kuzikwa katika eneo la tukio na moja yenye unafuu ilipelekwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwenye chumba cha maiti hadi pale ilipozikwa na halmashauri baada ya maiti hiyo kutotambuliwa na mtu yeyote.”

CP Boaz amesema hatua zote za kitaalam zilifuatwa na kwamba upelelezi unaendelea kufanywa ikiwemo wa kuwatambua marehemu hao na kujua chanzo cha vifo vyao

Wednesday, December 21, 2016

Mapya Yaibuka Sakata la Bwana harusi Aliyemkimbia Bi Harusi Siku ya Ndoa

Mapya  yameibuka sakata la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Samwel Mwakalobo na Ginen Mgaya, baada ya kubainika kuwa moja ya sababu ni Bibi harusi mtarajiwa kuendeleza uhusiano na mzazi mwenzake.
Bwana harusi, Samuel Mwakalobo alitoweka muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Ginen Mgaya  katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Isanga jijini Mbeya.
Mwakalobo (26) alizua taharuki hiyo  Ijumaa ya Desemba 16, baada ya kutoonekana kanisani kufunga ndoa mbele ya Mchungaji Andagile Mwakijungu.

Habari zimedai kuwa kabla ya mpango wa kufunga ndoa hiyo, Mgaya tayari alishapata mtoto kabla hajaolewa, na Bwana harusi kubaini dakika za mwisho kuwa wawili hao walikuwa bado wana uhusiano wa karibu.

Habari hizo za ndani kutoka familia ya Bibi harusi, zilidai kuwa kilichofanya Bwana harusi amtelekeze Bibi harusi ni wasiwasi aliokuwa nao juu ya uhakika wa ujauzito wa mkewe huyo mtarajiwa, kuwa ni wake kweli au wa mpenzi wake huyo wa zamani.

“Hofu hiyo ilijengeka kutokana na taarifa alizoziamini Bwana harusi kuwa Bibi harusi anaendeleza uhusiano na mzazi mwenziwe. Ni hofu tu ambayo angeifanyia kazi na angegundua kuwa haina ukweli wowote,” kilidai chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kudai: “Unajua muda mwingine binadamu tunahitaji kufanya uamuzi kwa kutafakari … maana shemeji yetu (Bwana harusi) alipigiwa simu na mzazi mwenza wa Bibi harusi na kuelezwa maneno ya ‘shombo’ na yeye bila kufanyia utafiti, akaamua kususa harusi.”

Wakati taarifa hizo zikibainisha hayo, familia ya Bwana harusi imeendelea kufanya jitihada za kuhakikisha suala hilo linamalizika kistaarabu.

Anayeelezwa kufuatilia suala hilo kwa karibuni ni kaka yake, ambaye hadi jana jitihada za kumtafuta mdogo wake zilikuwa zimeshindikana kutokana na kutopokea simu yake ya mkononi mara zote.

“Anayeongoza familia ya Bwana harusi ni kaka yake. Inasemekana pia kuwa wawili hao waliingia kwenye mgogoro dakika za mwisho kabla ya harusi na ndiyo maana baada ya kutoweka hataki hata kupokea simu,” kilieleza chanzo kingine.

Awali, mpambe wa Bibi harusi alieleza kuwa siku mbili kabla ya harusi hiyo, Bwana harusi alikuwa kwenye migogoro ya kifamilia na ndugu zake kuhusu fedha za sherehe na mpaka siku ya sherehe, suala hilo walikuwa hawajalitatua.

“Lakini tunashukuru kaka yake ni mstaarabu, aliamua kuonesha upendo kwa mdogo wake na amekuwa akilifuatilia suala hilo ili limalizike kwa amani, lakini mdogo mtu hapatikani,” alisema mpambe huyo.

Alisema jitihada za Bibi harusi kumtafuta Bwana harusi hazijazaa matunda, kwani hadi juzi alikuwa hapatikani hata nyumbani kwake, ingawa redio ilikuwa inasikika ndani ya chumba hicho kilichofungwa kufuli kwa nje.

Simu ya Bwana harusi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokewa, lakini hatua zingine zilidai kuwa Bwana huyo ambaye ni mfanyabiashara kwenye kituo cha mabasi yaendayo Chunya eneo la Isanga jijini Mbeya hajafungua duka lake.

 

Wednesday, December 21, 2016

Ahukumiwa Miaka 25 Jela Au Faini Bilioni 3.7 Kwa Kujihusisha na Biashara ya Meno ya Tembo

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Tanga, imemtia hatiani na kumuhukumu kwenda jela miaka 25 au kulipa faini ya Sh bilioni 3.7 mfanyabiashara Charles Kijangwa kwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.

Kijangwa alihukumiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cresencia Kisongo, baada ya kuruka dhamana kwa miaka sita. Alishindwa kulipa faini.

Mshtakiwa huyo alikabidhiwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Lushoto.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Saraji Iboru, alidai mahakamani kuwa mshtakiwa Kijangwa alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu mwaka 2010 baada ya kuruka dhamana katika shauri la uhujumu uchumi namba 6/2007.

Mshtakiwa alishtakiwa na wenzake Michael Msuya na Nyaisa Makori ambao walitiwa hatiani na mahakama, wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kumiliki kilo 5,000 za meno ya tembo kwa shtaka la kwanza.

Katika shtaka la pili la kula njama, washtakiwa wote walihukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh 10,950,000 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo 5,000 za meno ya tembo kwenda nchini Taiwan mwaka 2006.

Iboru aliiambia mahakama kuwa washtakiwa watatu, Kijangwa na wenzake walihukumiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya Sh 50,000 katika shtaka la kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Alidai mshtakiwa hakufika mwenyewe mahakamani hapo bali aliletwa baada ya kukamatwa Desemba 11, mwaka huu wilayani Lushoto.

Aliiomba mahakama kumtia hatiani mshtakiwa na kuhakiksha anatumikia adhabu iliyotolewa dhidi yake akiwa hayupo.

Hakimu Kisongo baada ya kusikiliza maombi hayo, alimtia hatiani mshtakiwa na kumuhukumu kwenda jela miaka 25 au kulipa faini ya Sh bilioni 3.7.

Mshtakiwa Kijangwa alitenda kosa hilo Novemba 2005 na Aprili 2006 kwa kusafirisha makontena mawili ya meno ya tembo yenye ujazo wa tani 5,000 yaliyokamatwa katika bandari ndogo ya Konshugi nchini Taiwan.

Makontena hayo ambayo yalitokea katika Bandari ya Tanga yakiwa na shehena ya kamba za katani na meno ya tembo ndani yake, yalikuwa yanapelekwa Manila nchini Philipine.

Wednesday, December 21, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 21



JUMATANO HABARI ZA LEO HIZI HAPA JUMATANO HABARI ZA LEO HIZI HAPA Reviewed by RICH VOICE on Desemba 21, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...