lhamisi, 29 Desemba 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita

MAPUNDA: ITC TAYARI TUMEIPATA

CARLOS TEVEZ AKAMILISHA UHAMISHO, ATUA SHANGHAI SHENHUA YA CHINA



TUME YA MIPANGO YATEMBELEA UJENZI WA KITUO CHA KUZALISHA UMEME KINYEREZI II

Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II, Mhandisi Bernd Siegemund akiweka bayana mipango na mikakati ya kumalizika kwa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II katika muda uliopangwa. Wengine ni wataalam kutoka Tume ya Mipango, wataalam kutoka TANESCO pamoja na wahandisi wanaotekeleza mradi huo.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II, Mhandisi Bernd Siegemund akitoa maelezo ya historia ya mradi huo kwa maofisa wa ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakati wataalam hao walipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujezi wa kituo hicho.

Mhandisi Omari Athuman (aliyeshika notebook) kutoka Tume ya Mipango akitoa ushauri kwa mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha kinyerezi II.

Picha ya pamoja kati ya wataalamu kutoka Tume ya Mipango, wataalam kutoka TANESCO pamoja na wahandisi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha kinyerezi II.


Shughuli za ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha kinyerezi II zikiendelea.

TAMWA WAPOKEA MALALAMIKO KUTOKA KWA MAKUNDI MAALUM YALIYOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA 2015 MANISPAA YA IRINGA


Baadhi ya washiriki walikuwa wakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu wa 2015 na mjadala huo uliongozwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

                                                                                                    Na fredy mgunda,iringa

MAKUNDI maalumu yanayohusisha vijana, walemavu na wanawake wa mjini Iringa walioingia katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 wakitoa masikitiko yao ya namna vyombo vya habari vilivyowapa nafasi finyu katika mchakato huo.

Makundi hayo yalikuwa yakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo iliyofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

Dora Nziku anatoa malalamiko yake kwa kuvilaumu vyombo vya habari mkoani iringa kwa kutowapa nafasi wanawake,walemavu hata wale wasio na kipato kwa kuwa waandishi wengi walikuwa wanajali maslai kuliko ukubwa wa habari
“Naona kama wanawake tuliathiriwa zaidi katika mchakato huo kwani habari zetu hazikupata nafasi kama ilivyo kwa wagombea wengine hasa wanawake,” alisema Diwani wa Viti Maalumu Iringa Mjini, Dora Nziku (CCM).

Nziku alisema imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wanahabari kuomba hela kwa wagombea na viongozi wa kisiasa ili waweze kutoa habari zao.

“Pamoja na kuwapa hela wakati mwingine habari hizo hazitoki na mimi ni mmoja wa wahanga wa hilo, nimewahi kuita wanahabari, wakaniomba hela lakini hawakutoa habari zangu na nadhani hazikutoka kwasababu mimi ni mwanamke,” alisema diwani huyo bila kutaja wanahabari hao.

Naye Agusta Mtemi aliyekuwa mgombea udiwani viti maalumu mjini Iringa (CCM) alisema katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda kwa kura 266 wagombea wenzake zaidi ya 10 lakini katika mazingira tata alionekana kama mshindi namba mbili na kukosa nafasi ya kuwawakilishi wanawake wenzake katika Baraza la Madiwani la Jimbo la Iringa Mjini.

Naye Imelta Mhanga kijana aliyegombea udiwani viti maalumu (CHADEMA) mjini Iringa alilaumu mchakato ndani ya chama akisema unawanyima uhuru wa kuongea na vyombo vya habari hasa wanapofanyiwa figisufigisu.

“Ndani ya taasisi kuna vitisho, kwamba shughuli za chama ni siri ya chama, hazitakiwi kutoka nje. Kwahiyo tunaogopa kukutana na wanahabari,” alisema huku akipinga kwamba wanahabari wanataka fedha mara zote ili kutoa habari zao.

Kwa upande wake, Selekti Sinyagwa ambaye ni mlemavu wa miguu aliyegombea udiwani viti maalumu ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) alisema; “kwa kweli walemavu tunabaguliwa sana katika mchakato wa kupata viongozi, jambo hili linatufanya tujione kama ni jamii tofauti na jamii tunayoishi nayo.”

Afisa Miradi wa TAMWA, Reonida Kanyuma alisema taasisi hiyo iliangalia namna makundi hayo yalivyoripotiwa katika vyombo vya habari ili kwa kushirikiana na wadau waje na suluhisho litakaloondoa tofauti zilizopo.

“Tulifanya ufuatiliaji katika mchakato huo, na kuona jinsi wanawake, walemavu na vijana walivyoripotiwa katika vyombo hivyo vya habari ikilinganishwa na wagombea wanaume katika nafasi za udiwani, ubunge na urais waliopewa nafasi,” alisema.

Alisema kwa kuwa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine, vyombo vya habari havipaswi kuwabagua wagombea kwa kuangalia udhaifu wao au mfumo dume na badala yake vitoe fursa sawa kwa kuzingatia uwezo na dhamira waliyonayo katika kuwatumikia watu wengine.
 

“Ni matarajio ya TAMWA na wadau wote wa maendeleo kwamba sekta ya habari itatenda haki kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote katika chaguzi zijazo,” alisema.

NGULI WA HOLLYWOOD DEBBIE AMFUATA BINTIE CARRIE ALIYEFARIKI DUNIA

DELE ALLI ATIKISA NYAVU MARA MBILI WAKATI TOTTENHAM IKIUWA

REA AWAMU YA TATU KUJA NA NGUZO ZA ZEGE

mule
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na wananchi wa Kijiji cha Kishuro,Kata ya Ngenge Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera. Dkt.Kalemani amefanya ziara Wilayani humo ya kukagua Mradi utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili na kueleza mipango ya Serikali kutekeleza Awamu ya Tatu ya mradi husika.
mule-1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na wananchi wa Kata ya Ngwanseri,wilaya ya Muleba, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.
mule-2
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango,akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalema ni kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.Wengine katika picha ni baadhi ya Viongozi wa Halmashauri hiyo,Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na Wakandarasi wanaotekeleza mradi husika.
mule-3
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, (Wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Prof.Anna Tibaijuka (wa pili kushoto),Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango,(wan ne kushoto)pmoja na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA Awamu ya Pili.
mule-4
Mmoja wa Wananchi katika akiuliza jambo wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani(hayupo pichani) katika Kata ya Ngwanseri.
mule-5
Wananchi wa Kata za Ngwanseri na Ngenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani na ujumbe wake wakati wa ziara yake a kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili wilayani Muleba.
mule-7
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof.Anna Tibaijuka (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani ( katikati) mara baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi wa Kijiji cha Kishuro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango.

WAZIRI MKUU ACHANGIA MABATI UJENZI WA ZAHANATI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahimiza wakazi wa vijiji saba wilayani Ruangwa waharakishe kufyatua matofali ili waanze ujenzi wa zahanati na yeye atawachangia mabati.

Ametoa ahadi hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula na viongozi wa wilaya ya Ruangwa, mkoa wa Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Amesema sera ya Serikali ni kuwa na zahanati kwa kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata na kwamba umefika wakati wa kuanza kutekeleza kaulimbiu ya jimbo hilo inayosema “Ruangwa kwa maendeleo, inawezekana.”

Katika kuhimiza ujenzi wa zahanati hizo, amechangia mabati kati ya 50 na 150 kwa kila kijiji na akawahimiza wahakikishe wanakamilisha mapema ujenzi wa maboma ili aweze kutimiza ahadi yake ya mabati.

Amesema katika awamu iliyopita, alikazania sana suala la elimu kwa kusimamia ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa kwenye shule ambazo hazikuwa na madarasa ya kutosha. Pia alisimamia ukarabati wa majengo chakavu katika baadhi ya shule.

“Kuanzia awamu hii na miaka minne iliyobakia, mkakati wangu ni kusimamia upatikanaji wa maji safi na suala la kuboresha sekta ya afya katika jimbo zima nikishirikiana na uongozi wa Halmashauri yetu,” amesema.

Pia amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Japhet Simeo ahakikishe anawasiliana na viongozi wa vijiji hivyo ili wapatiwe michoro ya ramani zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa kampuni ya Umemejua ya Baraka Solar Specialist, Bw. Ansi Mmasi amesema atajitolea kuweka mfumo wa umemejua wa watts 300 pamoja na nyaya zake kwenye zahanati inayotaka kujengwa kwenye kijiji cha Namilema.

Alisema anaishukuru kwa kuwapa kazi makandarasi wazawa na akawataka wakandarasi wenzake watumie vifaa bora na imara pindi wanapopewa kazi ya kutoa huduma na taasisi mbalimbali ikiwemo halmashauri na idara za Serikali.

“Tujitahidi kufanya kazi hizi kwa weledi na tutumie vifaa bora na imara ili watu wanaotarajia huduma zetu waweze kuridhika na kuendelea kuwa na umani na wakandarasi wazawa kwamba tunaweza kufanya kazi nzuri na zenye ubora unaotakiwa,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Wanyumbani Construction, Bw. Fakihi J. Bakili alisema atachangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji cha Namilema. Pia alichangia mifuko 100 kwenye zahanati ya kijiji cha Manokwe na mifuko mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chikundi.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU
Reviewed by RICH VOICE on Desemba 29, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...