ijumaaa hiii

 

 

JEMBE1.jpg

 

 

Friday, December 23, 2016


Dereva bodaboda akatwa sikio kwa tuhuma ya kufumaniwa na mke wa dereva teksi


Dereva bodaboda wa Mji Mdogo wa Qatesh wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara, amekatwa sikio kwa kisu kwa tuhuma za kufumaniwa akiwa na mke wa dereva wa teksi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Francis Massawe alisema tukio hilo lilitokea Desemba 21 saa 6:10 usiku kwenye Kitongoji cha Qendangonyi, Kata ya Ganana wilayani Hanang’.

Kamanda Massawe alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na majeruhi amepata kilema cha maisha baada ya sikio kutolewa.

Alisema wanamshikilia dereva teksi kwa uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani
 

 

riday, December 23, 2016


Rais Magufuli Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Wamtembelea Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Hatua hiyo ni kufuatia kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22 Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa na umri wa miaka 79.

Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali Pengo katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.


 

Friday, December 23, 2016

Picha: Mwenyekiti Mpya Wa NEC Jaji Semistocles Kaijage Aanza Kazi Rasmi.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini  Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
 

Friday, December 23, 2016

Rais Magufuli Akutana Na Waziri Mkuu Majaliwa Ikulu Jijini Dar

Rais John Magufuli  akisalimiana na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu jijini Dar es salaam, Desemba 23, 2016.
  Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu jijini Dar es salaam, Desemba 23, 2016.
Rais John Magufuli akizungumza na mtoto  Doreen Ndika ambaye aliambatana na baba yake, Jaji Dkt. Gerald Ndika  aliyeapishwa na Rais `Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 23, 2016 kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

 

Friday, December 23, 2016

Rais Magufuli Afanya Uapisho Wa Mwenyekiti NEC , Kamishna Wa Maadili Na Majaji Wa Mahakama Ya Rufani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Desemba, 2016 amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya Rufani aliowateua jana tarehe 22 Desemba, 2016.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na Viongozi wengine mbalimbali.

Walioapishwa ni Mhe. Mhe. Jaji Semistocles Simon Kaijage aliyeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Viongozi hawa watashika nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka mitano.

Kwa upande wa Majaji walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi na Mhe. Jaji Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika, Mhe. Jaji Jackobs Casthom Mwatebela Mwambegele.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yesamin Eralp ambapo viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki hususani katika masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kufuatia kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22 Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa na umri wa miaka 79.

Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali Pengo katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Desemba, 2016
.


 Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mohamed Hamid kuwa Makamu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapishaJaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam.




  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalaliwa Mwangesi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

riday, December 23, 2016

Madereva Wazembe Kuwekwa Selo Badala ya Kulipa Faini


JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini limesema litachukua hatua kali kwa kuweka mahabusu madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu badala ya kulipa faini kama ilivyozoeleka.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Kikosi hicho, Mohammed Mpinga, alipozungumza na vyombo vya habari akisema kutoza faini kumekuwa hakuwafanyi madereva kuacha kuvunja sheria.

“Kitendo cha kutoza faini, kimekuwa kikiwafanya madereva kuvunja sheria kwa makusudi, wakijua wakikamatwa watalipa faini na kuachwa,” alisema Mpinga.

Mpinga alisema katika kipindi hiki, watu wengi hupenda kusafiri kwenda maeneo mbalimbali na hivyo kuongeza matumizi ya vyombo vya moto barabarani ambapo pia huambatana na starehe nyingi ikiwa ni pamoja na ulevi kwa madereva.

Alieleza kutokana na hali hiyo ya starehe na ulevi, madereva wengi hupoteza umakini na kushindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hatimaye kusababisha ajali ambazo hugharimu maisha ya watu wengi.

Alifafanua, kwamba kipindi hiki madereva huwa na haraka na huendesha kwa mwendo kasi, hunywa pombe, hupenda kupita magari ambayo ya mbele yao bila hadhari na hufanya makosa ya kizembe yanayohatarisha maisha.

Kamanda Mpinga alisema kwa kutambua hilo, wamejipanga ili kuwatia mbaroni madereva hao na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha, alisema katika kipindi cha kuelekea mwishoni na mwanzoni mwa mwaka mpya, wamekuwa wakifanya operesheni katika barabara zote, stendi za mabasi ili kukagua ubora wa mabasi, mikanda, kupima ulevi madereva, uzidishaji abiria na nauli.

Alisema katika operesheni hii inayoendelea mikoani kwa kipindi kifupi madereva wa mabasi ya abiria wamekamatwa kwa mwendo kasi wa zaidi ya kilometa 90 kwa saa, ambapo katika mikoa tofauti jumla ya madereva 277 walifikishwa mahakamani wakitokea mahabusu na kulipa faini ya kati ya Sh. 300,000 na Sh 600,000


ijumaaa hiii ijumaaa hiii Reviewed by RICH VOICE on Desemba 23, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...