HABARI ZA JUMATATU HII
Monday, 26 December 2016
Magufuli awataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika
Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli ametoa rai hiyo (jana) katika Kanisa la Parokia ya
Moyo Mtakatifu wa Yesu mjini Singida katika kuadhimisha Sikukuu ya
Krismasi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
“Katika kipindi cha maisha yake Yesu Kristo hapa duniani, mbali ya
kwamba alizaliwa na mfanyakazi, Joseph seremala, lakini na yeye
alishiriki katika kufanya kazi, basi niwaombe watanzania wote tuchape
kazi kwelikweli kwa sababu hakuna cha bure,” alisema Rais Magufuli.
Pia amewataka watanzania kuimarisha upendo, kuvumiliana, na
kutobaguana, kwani upendo utalisaidia taifa kupata maendeleo huku
akiwakumbusha waumini kuwa Yesu Kristo hakuwa CHADEMA wala CCM bali
alikuwa ni wa watu wote.
Rais Magufuli ambaye aliambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli,
katika ibada hiyo amesema, kusali ni moja ya nguzo muhimu ambayo
Wakristo wote wanapaswa kutekeleza ili kuhakikisha taifa linaendelea
kubakia katika hali ya amani na utulivu ambayo ndiyo msingi wa
maendeleo.
Monday, December 26, 2016
Picha 15: Vodacom Wasafi Festival Ilivyofanyika Dec 25 Mkoani Iringa
Usiku
wa Dec 25, 2016 wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz,
Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Q Boy, Chege pamoja na msanii kutoka
Nigeria Kcee wameandika historia katika mkoa wa Iringa.
Show
hiyo iliyopewa jina la Vodacom Wasafi Festival imefanyika katika uwanja
wa Samora Stadium, hizi ni baadhi ya picha kutoka mahali palipofanyika
tamasha hilo.
Mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop
George Michael amefariki dunia jana baada ya moyo wake kushindwa
kufanya kazi akiwa nyumbani kwake huko Oxfordshire Uingereza.
Monday, December 26, 2016
Michezo: Haji Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro Kwa Rais Wa TFF
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday
Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry
Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa
soka la Bongo.
Jerry
Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga
amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana
na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai
mwaka huu.
Manara
katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza
kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya
Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka
yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya
kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.
"Nimekaa
nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro
ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu,
ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia
karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa
keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi
wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika Manara
Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu
pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini
yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini
viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema,
ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba".
manara
amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na
kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry
bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.
Kwa
upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji
Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho
la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini
yeye na Haji Manara.
Monday, December 26, 2016
Rais Magufuli Atoboa Siri ya Kula Christmass Mkoani Singida
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri
ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini
Singida mwaka huu.
Ametaja
siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi
kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja
(hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia
kushinda uchaguzi huo.
Rais
Magufuli ametoa siri hiyo jana wakati akizungumza kwenye sherehe ya
Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na
kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.
Akifafanua,
alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho
wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.
“Hiyo
ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na
wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea
kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.
Rais
Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu
hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na
kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.
Katika
hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima,
wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa
kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili
ukame.
“Ndugu
zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha
zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi.
Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi …
na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.
Akiijengea
nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa
na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea
Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku
wakijua hakuna cha bure.
Aidha,
Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji
wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta
ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.
Awali
askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia
fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira,
ili yaweze kuwatunza na wao.
Alisema
hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu
mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.
“Mimi
nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu
mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke
kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira,
ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.
Monday, December 26, 2016
Michezo: Ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Disemba 30
Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua
vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku
ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe
na Jangombe Boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu
9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka
Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.
KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP
30/12/2016 Taifa ya Jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.
1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.
2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
6/1/2017 Taifa ya Jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.
10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainali ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainali ya pili.
13/1/2017 Fainali saa 2: 30 usiku.
Monday, December 26, 2016
Michezo: TFF Yasema Mechi ya Simba na Yanga iko palepale
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ya
mzunguko wa pili kati ya Simba na Yanga iliyokuwa imepangwa kuchezwa
Februari 18 mwaka 2017 iko palepale kwa kuwa bado halijafikiria
kuibadili tarehe hiyo.
Hatua
hiyo inatokana na tarehe hiyo kugongana na kalenda ya CAF ya michuano
ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyotolewa hivi karibuni na kuipanga
Yanga kucheza mchezo wa marudiano kati yake na Ngaya de Mbe ya Comoro
kati ya tarehe 17, 18 na 19 mwezi Februari 2017.
Afisa
Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa hadi sasa shirikisho hilo
kupitia Bodi ya Ligi halijafikiria kufanya mabadiliko yoyote kwenye
ratiba hiyo, na kwamba ratiba itaendelea kubaki kama ilivyo hadi hapo
itakapotangazwa vinginevyo.
"Ratiba
imeshapangwa na haitabadilika, kila timu inajua itacheza lini, kuhusu
ratiba ya CAF haiwezi kutuzuia kufanya mashindano yetu, kama kuna timu
inacheza CAF inatakiwa ijipange, kila timu inatakiwa kuwa tayari wakati
wowote ndiyo maana zinafanya matayarisho, zinaajiri makocha, zinasajili
wachezaji , hiyo yote ni matayarisho kwahiyo sidhani kama watahitaji
kupumzika na kutuharibia ratiba" Amesema Lucas
Jumatatu
iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura akiwa kwenye
kipindi cha 5Sports cha EATV, alisisitiza kuwa katika mzunguko wa pili
wa ligi, ratiba haitakuwa tatizo, na kwamba haitabadilishwa badilishwa
kwa kuwa katika upangaji wake kila kitu kilizingatiwa ikiwemo kalenda ya
CAF.
Jumatatu, 26 Desemba 2016
MAN UNITED YAPATA USHINDI WA NNE MFULULIZO LIGI KUU YA UINGEREZA
Manchester United imepata ushindi wa
nne mfululizo wa Ligi Kuu ya Uingereza katika mchezo walioutawala
dhidi ya Sunderland inayobakia katika mstari wa kushuka daraja baada
ya kulala kwa magoli 3-1.
Manchester United iliyostahili
ushindi iliutawala mchezo huo kwa asilimia 63, ilipiga mashuti 25
kwenye goli, lakini zilikuwa jitihada za beki Daley Blind zilizozaa
matunda na kuipatia goli la kwanza kufuatia pasi ya Zlatan
Ibrahimovic.
Katika kipindi cha pili Zlatan
Ibrahimovic aliongeza goli la pili akinasa pasi ya Paul Pogba huku
Henrikh Mkhitaryan aliyetokea benchi akifunga goli la kisigino licha
ya kuonekana ameotea.
Zlatan Ibrahimovic akianza kushangilia goli wakati mpira ukielekea wavuni
Mchezaji raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan akifunga goli kwa kisigino
OLIVER GIROUD AIPATIA ARSENAL USHINDI KATIKA DAKIKA ZA MWISHO
Mshambuliaji wa Arsenal Oliveir
Giroud amefunga goli la ushindi katika dakika za mwisho na kumaliza
gundu la kufungwa michezo miwili ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa ushindi
dhidi ya West Brom.
Giroud alianza kwa mara ya kwanza
katika kikosi cha kwanza katika msimu huu, na alifanikiwa kufunga kwa
mpira wa kichwa akiunganisha krosi ya Mesut Ozil katika dakika ya 86
ya mchezo huo.
Hadi Arsenal inapata goli hilo
ilikuwa inaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 80, lakini ilikuwa
na wakati mgumu kufanikiwa kutikisa nyavu za West Brom kazi kubwa
akifanya kipa Ben Foster.
Olivier Giroud akiwa ameupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli pekee
Aaron Ramsey akishangilia kuona mpira wa kichwa uliopigwa na Giroud ukitinga wavuni
RC GAMBO AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Arushaa ofisini kwake
juzi kutoka vyombo mbalimba vya habari kuhusu sakata la kukamatwa
kwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV Halfani
Liundi ambapo amehaidi kulishughulikia huku akiwataka waandishi
kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mwandishi wa kituo
cha ITV Halfani Liundi aliyekamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi,
ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anatambua umuhimu wa
vyombo vya habari na hivyo mwandishi anauhuru wa kwenda popote kupata
taarifa yeyote kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari
Mwandishi wa habari wa kituo cha
channel Ten Aristrides Dotto akichangia katika mkutano huo wa
waandishi wa habari na mkuu wa Mkoa juzi ofisinii kwake jijini Arusha
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifatilia mkutano huo
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi
Mosses Mashalla akichangia katika mkutano huo wa mkuu wa Mkoa na
waandishi wa habari mkoa wa Arusha. (Picha zote na Pamela Mollel)
Jumatatu, 26 Desemba 2016
MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHALANGWA MAPANGA NA MWALIMU
Mwanafunzi Marco Limbe akiwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa panga na Mwalimu Pendo Gabriel
Mwalimu Pendo Gabriel akiwa naye amelazwa baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira
Na Shushu Joel, BUSEGA
MWANAFUNZI Marco Limbe(14)
aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila
iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa
katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga
kichwani na mdomoni na mwalimu wake.
Tukio hilo limetokea jana majira ya
saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani
kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika
shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana
huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe
kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika
kituo cha afya Busega.
“Shuhuda wa tulio hilo
aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa
kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe
iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo
katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla
nilimuona mwalimu pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona
akiwa na panga na kuanza kumchalanga”
Nilikimbia katika tukio na kutoa
msaada kwa wote lakini mara watu walijaa na kuanza kumshambua mwalimu
Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo lilikwama mara baada ya
mwenyekiti wa kijiji hicho mshemas bahai.
Mwandishi alikwenda katika kituo cha
afya cha Nyashimo na kujionea hali mbaya kwa kijana Limbe ambaye
alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 bila kujitambua na huku
akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni mwalimu Gabriel naye akipata
matibabu ya jeraha lake kichwani amabolo alishambuliwa na wananchi na
huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la piolisi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
mwenyekiti wa Sogesca Bahai Mshemas alisema kuwa sikukuu ya kuzaliwa
kwa yesu imekuwa ni mbaya katika kijiji chake mara baada ya wananchi
walio na hasira kali kufanya shambulio la kumshambulia mwalimu Pendo
kwa kosa la kumchalanga na panga mwanafunzi wake aliyekuwa akitokea
kwenye malisho na kupita karibu na shamba lake la mahindi.
Aliongeza kuwa alifanikiwa
kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza kufanya mikakati ya
kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za matibabu.
Aidha Mshemasi aliongeza kuwa
walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili
mwalimu pamoja na mwanafunzi.
Kwa upande wake kaimu mganga
mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk Ayubu Ismail alithibitisha
kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana limbe ndiye aliyekuwa
na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu pendo.
Aliongeza kuwa kijana ameshonwa
nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na majeraha na huku
mwalimu yeye akiwa ameshonwa nyuzi 6.
“ni kweli Limbe alikuwa ametokwa
na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea kupoteza fahamu kwa muda wa
masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri alisema Dk Ismail”
NYOTA WA POP GEORGE MICHAEL AFARIKI DUNIA
Mwanamuziki huyo aliyeanza muziki
katika miaka 80, na kupata mafanikio zaidi akiimaba peke yake nje ya
bendi, amefariki dunia kwa amani jana siku ya Krismasi, kwa mujibu wa
msemaji wake.
Mwanamuziki mwenzake wa zamani wa
bendi ya Wham! Andrew Ridgeley amesema amevunjika moyo kuwa kumpoteza
rafiki yake kipenzi.
George Michael akiwa na Andrew Ridgeley wakiimba pamoja na bendi ya Wham !
Picha
hii inaaminika kuwa ni picha ya mwisho kupiga George Michael hii
ilikuwa Septemba mwaka huu akipata mlo wa usiku na rafiki yake
Pata wimbo maarufu wa George Michael wa Careless Whisper
Pata wimbo maarufu wa George Michael wa Careless Whisper
https://youtu.be/izGwDsrQ1eQ
habari za kimataifa
Mabaki ya ndege ya Urusi iliyoanguka yapatikana
Balozi wa zamani wa Marekani Israel ashutumu lugha chafu ya Netanyahu
Raia 21 wauwawa na waasi Aleppo
Shambulio la kujitoa muhanga katika soko Maiduguri
HABARI ZA JUMATATU HII
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 26, 2016
Rating:
Hakuna maoni