habari za leo

 

 

Jumatatu, 19 Desemba 2016

BALOZI KIJAZI ATANGAZA UTEUZI WA MA-DC, MA-DED, MA-DAS NA WENYEVITI WA BODI ZA TAASISI ZA SERIKALI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza majina ya walioteuliwa kuwa wenyeviti wa bodi za taasisi za serikali, Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi na Mjumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 19, 2016. PICHA NA IKULU


MTOTO AWAKIMBIA WAZAZI WAKE JIJINI DAR ES SALAAM KUKWEPA KUKEKETWA

                                                            Kamanda wa Polisi Ilala, Salum Hamdun
                                                                                      
                                                                                       Na Dotto Mwaibale

MTOTO mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kivule Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam jina lake linahifadhiwa ameelezea jinsi alivyofanikiwa kuwatoroka wazazi wake ili asikeketwe.

Mtoto huyo hivi sasa analelewa na msamaria mwema baada kufungua kesi Kituo cha Polisi cha Stakishari Ukonga kufuatia kufikishwa kituoni hapo kwa ajili ya kujisalimisha na kuelezea madhila aliyotaka kufanyiwa.

Wakati mtoto huyo akijisalimisha katika kituo hicho kuna taarifa za ndani kuwa kuna mpango wa kuwakeketa watoto 85 wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 15 katika manispaa hiyo ambapo watoto zaidi ya 30 wanadaiwa kukeketwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam mtoto huyo alisema hawezi kurudi tena nyumbani kwao kwa kuhofia kupigwa na kukeketwa ambapo ameomba msaada wa hifadhi kutoka kwa watanzania.

“Baada ya baba yangu kufariki nyumbani kwetu Tarime tulikuja na mama hapa Dar es Salaam kwa kaka yake Chacha Nyanchiri anayeishi Kitunda Kivule karibu na Shule ya Msingi Misitu” alisema mtoto huyo.

Alisema katikati ya wiki iliyopita alifika bibi yake mzaa baba yake aliyemtaja kwa jina la Boke na kuwaambia yeye na wenzake wajiandaa kwenda kukeketwa.

Mtoto huyo alisema kwamba siku ya alhamisi majira ya saa mbili usiku wakiwa nyumbani kwa mjomba wao anakoishi na mama yake alifika bibi mzaa mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Debora huku akiwa ameongozana na mama yake Happyness na kuwaambia yeye na watoto wengine wawili wa mama yake mkubwa wakaoge ili waende kukeketwa.

Alisema ili kukwepa kukeketwa alipokwenda bafuni alifanikiwa kutoka na kupita njia nyingine na kufanikiwa kuwatoroka wazazi wake na kwenda kujificha kwenye pagala na ilipofika saa tatu usiku alifika eneo la kwa Mpemba akielekea darajani ambapo alikutana na dada mmoja aliyemsimulia mkasa huo.

Alisema dada huyo alimchukua hadi nyumbani kwake ambako alilala na siku iliyofuata alimpeleka kituo cha Polisi cha Stakishari kwa ajili ya usalama wake.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye alikataa kutaja jina lake alisema kuna mpango wa kuwakeketa watoto 85 kabla ya kuisha kwa mwaka huu wa 2016 na kuwa karibu watoto 30 wamekwisha keketwa.

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA AFANYA ZIARA WILAYANI NGARA MKOA WA KAGERA NA KUZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA UMOJA HUO

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara Katika Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako Wilayani Ngara.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Kijiji Cha BENACO Wilayani Ngara, Shaka yupo kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM 2015_2020
Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw. Yahya Kateme akizungumza
kumkaribisha Ndg: Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka
Kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara Katika Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako Wilayani Ngara
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizindua Mradi wa kikundi cha Vijana wajasiliamali cha Ufugaji wa Nyuki na Shamba la Upandaji wa Miti katika kijiji cha Nyaruku Wilayani Ngara.

KONGAMANO LA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA UN LAFANA TANGA


Tanga, WANAFUNZI wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa.
 
Wanafunzi hao walijadili mambo hayo yakiwemo Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika pamoja na changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko.
Pia walijadili uchafuzi wa mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa mazingira ya bahari kwa baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete, amezitaka Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali uchafuzi wa mazingira
Mwenyekiti wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini Rahim Nassir, akizungumza kwenye kongamano la vilabu vya umoja wa Mataifa lililowashirikisha wanafunzi vyuo vikuu na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga

MABONDIA VICENT MBILINYI NA IDD MKWELA WAENDELEA KUJIFUA KWA SUPER D COACH


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia Vicent Mbilinyi kwa ajili ya mpambano wake na Mrisho Adamu utakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park desemba 31 mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Iddi Mkwela wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake na Mrisho Adamu utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Iddi Mkwela kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake Desemba 31 kupambana na Mrisho Adamu Picha na SUPER D BOXING NEWS

ATHARI ZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

WASANII WAPEWA WARSHA JUU YA MASUALA YA UKOMBOZI WA MWANAMKE

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao.
Majadiliano katika warsha hiyo yakiendelea.
                                                           Majadiliano katika warsha hiyo yakiendelea.
Baadhi ya maofisa wa TGNP Mtandao wakiwa katika warsha hiyo.
                  
 Baadhi ya maofisa wa TGNP Mtandao wakiwa katika warsha hiyo.
 

Monday, December 19, 2016

Wananchi 21 wafikishwa mahakamani kwa kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi.

Jumla ya watuhumiwa 21 akiwemo mwanamke mmoja wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Chunya kwa kuhusika na vurugu zilizotokana na wananchi wilayani humo kuvamia kituo cha polisi kwa lengo la kuwatoa watuhumiwa wa mauaji ili kuwaadhibu.

Watu hao waliofikishwa mahakamani ni sehemu ya watuhumiwa 41 waliokamatwa, kati yao wanaume wakiwa 34 na wanaweke 7 baada ya vurugu zilizotokea jana na kusabababisha jumla ya watu 7 kujeruhiwa wakiwemo askari polisi wanne, na wananchi watatu huku mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la AMOKE MBILINYI (25) akifariki dunia.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya imeeleza kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 18.12.2016 majira ya saa 11:45 asubuhi katika Kituo cha Polisi Makongolosi kilichopo Kata ya Makongolisi, Wilayani Chunya ambapo kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi walivamia kituo hicho cha Polisi na kufanya fujo kwa kuwarushia  mawe hovyo askari.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, lengo la uvamizi huo ilikuwa ni kuwatoa watuhumiwa wawili waliofahamika kwa majina ya 1. ERASTO ROBERT, mkazi wa Kilombero na 2. BASI LINUS mkazi wa Makongolosi waliokuwa wanakabiliwa na kosa la mauaji kwa lengo la kuwatoa nje na kuwauawa kwa kuwachoma moto. 

Aidha wananchi hao walifunga barabara ya Chunya/Makongolosi kwa kuweka mawe makubwa na magogo hali iliyosababisha usumbufu mkubwa wa watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Jeshi hilo limesema thamani ya uharibifu bado kufahamika na hali imerejea kuwa shwari

Awali mnamo tarehe 11.12.2016 majira ya saa 23:20 katika Kitongoji cha Manyanya, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JACOB BROWN Mkazi wa Manyanya alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa peke yake shambani kwake na kuuawa ambapo Polisi walifanya msako na kuwakamata watu hao wawili kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Monday, December 19, 2016

Uteuzi: Rais Dkt Magufuli ateua Wenyeviti 7 wa Bodi za Taasisi za Serikali


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Wenyeviti 7 wa Bodi za Taasisi za Serikali, na pia ameteua Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania na Mjumbe mmoja wa Baraza la Taifa la Biashara.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 19 Desemba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kama ifuatavyo;
 
1. Rais Magufuli amemteua Bw. Ali Mufuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira.
 
Ali Mufuruki ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Infotech Investment na Mwenyekiti wa Taasisi ya Afrika inayojihusisha na uendelezaji wa vipaji vya uongozi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
 
2. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Christopher Kajolo Chiza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Mhandisi Christopher Kajolo Chiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sabetha Mwambenja ambaye amemaliza muda wake.
 
3. Rais Magufuli amemteua Bw. Peter M. Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
 
Peter M. Maduki anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Idrissa Mshoro ambaye amemaliza muda wake.
 
4. Rais Magufuli amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
 
Dkt. Yamungu Kayandabila ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Peter Ilomo ambaye amemaliza muda wake.
 
5. Rais Magufuli amemteua Prof. Godwin Daniel Mjema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Huduma za Fedha na Mikopo (UTT-MFI)
 
Prof. Godwin Daniel Mjema ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Fadhili D. Mbaga ambaye amemaliza muda wake.
 
6. Rais Magufuli amemteua Kepteni Ernest Mihayo Bupamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Bahari (DMI)
 
Kepteni Ernest Mihayo Bupamba ni Mwendesha Meli Mkuu (Principal Captain) Katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
 
7. Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce S. Hepelwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Miradi ya Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID)
 
Dkt. Aloyce S. Hepewa ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. John Jingu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Tanzania.
 
Dkt. John Jingu ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Dkt. Rashid Adam Tamatama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI).
 
 Dkt. Rashid Adam Tamatama ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Pia, Rais Magufuli amemteua Bibi. Zuhura Muro kuwa Mjumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (Tanzania National Business Council – TNBC).
 
Bibi. Zuhura Muro ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi inayojihusisha na huduma za ushauri wa ubora na mafunzo (Service Limited) katika ofisi zake za Dar es Salaam.
 
 Wateule wote waliotajwa hapo juu, uteuzi wao umeanza tarehe 17 Desemba, 2016
 
 Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Desemba, 2016
 
 

Picha: Mshindi wa shindano la Miss World 2016 lililofanyika jana Marekani

Jana, Jumapili Disemba 18, 2016 jijini Washington DC, Marekani lilifanyika shindano kubwa la kumsaka Mrembo wa Dunia (Miss World 2016) ambapo nchi mbalimbali zilishiriki kwa kuwapeleka warembo walioibuka na ushindi katika nchi hizo.

Shindano hilo lilimalizika kwa Mrembo kutoka nchini Puerto Rico, Stephanie Del Valle (19) kunyakuwa taji la Mrembo wa Dunia 2016 (Miss World 2016).

Mrembo huyo alitangazwa mshindi baada ya kuwashinda warembo wengine kutoka nchi 116 duniani kote na Tanzania ikiwa moja wapo.

Mshindi wa pili ni Yaritza Miguelina Reyes Ramirez kutoka Jamhuri ya Dominican huku nafasi ya tatu ikiwenda kwa Natasha Mannuela kutoka Indonesia.

Hapa chini ni picha za tukio hilo lililofanyika jana.


Monday, December 19, 2016

Sungura Amtikisa Mbatia .....Amtaka Ajiuzulu Nafasi ya Mwenyekiti NCCR-Mageuzi ili Kukinusuru Chama 

 




Aliyekuwa  Mkuu wa Idara ya Kampeni ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura, amenzisha fukuto kwa kumtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia kujiuzulu nafasi yake kwa madai kuwa ameshindwa kukiongoza chama hicho tangu alipoingia madarakani.

Sungura anasema bila kufanya hivyo, atashirikiana na wanachama wengine kumwondoa, kwa sababu amekisahau chama na kujikita katika shughuli nyingine zisizo na tija, jambo ambalo limechangia chama hicho kupata mbunge mmoja kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba, mwaka jana.

Anasema hali ilipofikia hivi sasa, chama hicho kinaweza kufa na kubaki historia ambayo haiwezi kuwasaidia wanachama wengine wanaopigania uhuru na demokrasia ndani ya nchi yao.

“Hatumwondoi Mbatia kwa sababu tunamchukia, bali tunamwondoa kwa kushindwa kuangalia masilahi ya chama na kujikita kwenye shughuli zisizo na tija, jambo ambalo limechangia kupoteza wabunge na kubaki na mbunge mmoja ambaye ndiye yeye katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

“Kwa sababu nafasi ya uenyekiti si ubatizo na wala si kiungo cha mwili wake, hata tuseme tutamuumiza, hivyo basi tunaamini vijana wenye mapenzi mema na chama wataungana na mimi kuhakikisha kuwa mwenyekiti anatoka madarakani ili tuweze kukiendesha chama,”- Sungura.

Anadai  kuwa lengo lao ni kufanya siasa zenye tija, zikiwamo za kuzunguka mikoani kutafuta wanachama wapya na kuandaa viongozi ambao wataweza kukisimamia chama hadi uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Anasema kutokana na hali hiyo, nafasi yake itakabidhiwa kwa mwanachama mwingine kama alivyonyang’anywa mwenzake na kijiti kukabidhiwa yeye ili aweze kukiongoza chama.

Sungura alijunga na chama hicho tangu mwaka 1992, akiwa mwanachama mwenye kadi N0. 00011763.

Ofisa Utawala wa chama hicho, Frolian Mbeo, alipoulizwa kuhusu kauli ya Sungura, alisema hadi jana mchana hakuwa na taarifa yoyote ya kuwapo malalamiko ya mwanachama huyo.

Alisema uamuzi wa Sungura, umekuja  baada ya kutolewa kwenye nafasi ya ukurugenzi wa kampeni, jambo ambalo limemfanya kuzunguka mikoani na kuanza kukisema vibaya chama.
 
 

Monday, December 19, 2016

Mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums Maxence Melo Aachiwa kwa dhamana





Mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums  Maxence Melo   ameachiwa kwa dhamana leo  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukaa mahabusu kwa takribani siku 5.

Melo anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumiliki na kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini Tanzania (JamiiForums).

Mashtaka mengine ni kuzuia na kuharibu taarifa ambazo Jeshi la Polisi wamekuwa wakizitaka kwa ajili ya uchagunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Mitandao na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi  na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha namba 22 cha Sheria ya Makosa ya Mitandao.

habari za leo habari za leo Reviewed by RICH VOICE on Desemba 19, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...