habari za leooo.
Friday, December 2, 2016
Aliyetishia kumuua Trump mitandaoni aonja joto la jiwe
Maafisa
Usalama wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump wamemtembelea mtu
mmoja aliyetishia kumuua kiongozi huyo kwa ujumbe alioweka kwenye
mitandao ya kijamii.
Vyanzo
vya vyombo vya dola viliuambia mtandao wa TMZ kuwa kikosi maalum cha
mashushu wa usalama cha Trump pamoja na Mkuu wa Polisi msaidizi wa Ohio,
Jumatatu ya wiki hii walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo aliyeweka
ujumbe wake kwenye mitandao Novemba 14 mwaka huu, ukisioma “Kill Trump”
(Muue Trump).
Ilielezwa
kuwa kikao kati ya maafisa hao wa usalama nyumbani kwa mtu huyo
anayetumia jina la ‘Micah’, kilienda vizuri ambapo aliwaeleza kuwa
alikuwa anatania tu huku akisisitza kuwa huenda akapata wazo hilo pale
ambapo Trump ataanza kutekeleza ahadi zake tata.
Micah
pia alithibitisha kutembelewa na maafisa hao wa usalama na kueleza kuwa
waliridhika na maelezo yake kuwa alikuwa anafanya utani tu, hivyo
waliondoka.
Trump
amekuwa akipata vitisho vya kushambuliwa tangu alipokuwa akiendesha
kampeni zake. Mara kadhaa maafisa usalama walimuondoa ghafla jukwaani
baada ya kuhisi jaribio la kutaka kumdhuru kutoka kwa wahudhuriaji.
Friday, December 2, 2016
Godbless Lema Anyimwa Dhamana Kwa Mara Nyingine Tena
Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA)
Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wamtuhumiwa huyo
walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku10 kabla ya
kukata rufaa.
Hii
ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu
alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi
Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Katika
kesi ya msingi lema anatuhumiwa kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya
Rais Magufuli kwa madai kuwa Mungu ndiye aliyemwambia maneno hayo wakati
akiwa anaomba.
Friday, December 2, 2016
Mahakama Yawaachia Huru Wafuasi wa CHADEMA Waliokuwa Wakikusanya na Kusambaza Matokeo ya Uchaguzi Mkuu
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wanachama watano wa Chadema
pamoja na watu wengine watatu wasio raia wa Tanzania waliokuwa
wanakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kimtandao.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage aliwaachia huru washtakiwa hao jana chini
ya Kifungu cha 91(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) baada ya
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kusema hana nia ya kuendeleza mashtaka
dhidi ya washtakiwa hao.
Waliachiwa huru, baada ya Wakili wa Serikali, Elia Athanas kuomba kufutwa kesi hiyo chini ya kifungu hicho na Mahakama kuridhia.
Kesi
hiyo, imefutwa ikiwa katika hatua ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa
mashahidi wa upande wa mashtaka baada ya kukamilisha upelelezi wao na
washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.
Katika
kesi hiyo, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
Oktoba 27, 2015 na kusomewa mashtaka ya makosa ya uhalifu wa kimtandao,
wakidaiwa kukusanya na kusambaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika
Oktoba 25, 2015.
Washtakiwa hao ni Mashinda Edwin Mtei, Julius Mwita, Fredrick Eddie Fussi, Meshack Carlos Mlawa na Anisa Nicholaus Rulanyaga.
Mbali
na wanachama hao wa Chadema, washtakiwa wengine ambao ni raia wa kigeni
ni Julius Mwonga Matei (Kenya), Jose Mavinga Nimi ambaye kwa sasa ni
marehemu (Angola) na Kim Hyunwook (Korea) kwa pamoja wanadaiwa kutenda
makosa hayo kinyume cha Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Uhalifu
wa Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Kwa
pamoja, walidaiwa kuwa kati ya Oktoba 25 na 26, 2015 kwenye maeneo
tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam, walichapisha matokeo ya uchaguzi
wa urais wa mwaka 2015 yasiyo sahihi na ambayo hayakuthibitishwa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa lengo la kuipotosha jamii.
Walidaiwa
kuwa siku hiyo ya tukio, walichapisha na kusambaza matokeo hayo kupitia
mfumo wa uratibu wa uchaguzi uitwao ‘M4C Election Results Management’
na kupitia mitandao mingine ya kijamii, kama vile Facebook na Twitter.
Washtakiwa
Matei, Mavinga na Hyunwook wanadaiwa kujihusisha na ajira nchini bila
ya kuwa na kibali, kinyume cha Sheria ya Uhamiaji. Wanadaiwa kuwa Oktoba
26, 2015 katika Hoteli ya King D, iliyoko wilayani Kinondoni, Dar es
Salaam, wageni hao walijihusisha katika ajira ya kukusanya na kusambaza
matokeo ya uchaguzi wa urais nchini kwa Chadema bila kibali.
Pia
wageni hao walidaiwa kujihusisha na shughuli za biashara nchini kwa
niaba ya Wanama Saccos, bila ya kuwa na kibali kinyume cha Sheria ya
Uhamiaji.
Friday, December 2, 2016
Tundu Lissu : Tunakuja na staili mpya kumkabili Magufuli
Mwanasheria
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
amesema kuwa vyama vya upinzani vimejipanga vizuri kwaajili ya
kukabiliana na Rais Dkt. John Magufuli .
Amesema
hayo katika Semina iliyowashirikisha viongozi wa vyama vya upinzani
kutoka Mataifa 16 iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni
Jijini Dar es salaam, amesema wanapambana kuhakikisha uwanja wa siasa
unakuwa sawa lazima wabadili staili ya kumkabili Rais Magufuli.
Lissu
amesema watafanya siasa ikiwa Magufuli anataka ama hataki, ama
wanavunja Sheria ama hawavunji” Akipiga marufuku shughuli za kisiasa,
hatuwezi kwenda kanisani kuomba, hapana lazima kazi ziendelee katika
aina nyingine”amesema Lissu.
Aidha,
Lissu ameongeza kuwa katika Uchaguzi uliopita haukuwa wa haki na huru
ambapo mawakala waliokuwa wakihesabu kura walikamatwa na kupelekwa
polisi.
Hata
hivyo ameongeza kuwa hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa kiongozi yeyote
atakayefanya siasa anaonekana kama mhalifu na hukamatwa na kupelekwa
mahakamani, hivyo hakuna Demokrasia bali kuna udikteta mkubwa.
riday, December 2, 2016
Waziri Mkuu Majaliwa aiagiza Bodi ya Taifa ya Wahasibu Kuwaanika na Kuwachukulia Hatua Kali Wahasibu Wezi
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, ameiagiza Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi
wa Hesabu nchini (NBAA) kuwachukulia hatua wale wote wanaoitia doa
taaluma hiyo kwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.
Maagizo
hayo yametolewa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Mpango, wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC)
uliokwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa wahasibu
unaojumuisha wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki, katika eneo la
Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Amesema
kuwa Idadi ya Wahasibu wenye sifa inazidi kuongezeka na hivyo kuisaidia
Serikali, japo kuwa Serikali hairidhiki kuona wanataaluma wa Uhasibu na
Ukaguzi wa hesabu (CPA) wanaongezeka huku vitendo vya ubadhilifu wa
fedha za Umma na ufisadi vikiendelea kuripotiwa.
“Wapo
hata wahasibu wanaotumia taaluma yao vibaya, wanaowawezesha
wafanyabiashara kukwepa kodi, wanachakachua vitabu vya taarifa za fedha
na kufanya ufisadi kwa njia ya kalamu na kompyuta jambo ambalo
halikubaliki hata kidogo” Aliongeza Dkt. Mpango
Alisema
kuwa machozi ya masikini wa Tanzania yatawafuata mafisadi hadi kaburini
lakini serikali ya Awamu ya Tano haitasubiri hao mafisadi wafe,
itawatumbua na wala hakuna mzaha na kwamba tayari mahakama ya mafisadi
imeanza kazi na itawashughulikia.
Aidha,
Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaasa
wanataaluma wa uhasibu na ukaguzi wa hesabu kuitumia taaluma yao
kuisaidia Serikali katika hatua yake ya kuelekea katika uchumi wa kati
unaotegemea viwanda kwa kuwa taaluma hiyo ina umuhimu mkubwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu, Bw. Pius Maneno alisema kuwa, Kituo hicho
kilichozinduliwa cha APC hadi kumalizika, kitagharimu Sh. Bilioni 35
ambapo mpaka sasa fedha zilizotumika ni takribani Sh. Bilioni 31.5.
“Gharama
halisi za ujenzi wa kituo hicho zilikuwa Bilioni 14 lakini kutokana na
mzabuni wa ujenzi kuchelewesha ujenzi ndio maana kumekuwa na Ongezeko la
kiasi hicho cha fedha” aliongeza Bw. Maneno.
Ujenzi
wa kituo hicho ambao uko katika eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 14
umehusisha ujenzi wa Kumbi za mikutano zinazochukua zaidi ya watu 1600,
viwanja vya michezo na vyumba vya kisasa 108 vya kulala wageni.
Bw.
Maneno alisema kuwa kujengwa kwa kituo hicho kutaifanya Bodi hiyo
kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikitumika kukodi kumbi za
kufanyia na kusahisha mitihani ya Bodi (NBAA).
Alizitaja
faida zingine kuwa ni kuboreshwa kwa mazingira ya kitaaluma na
wanataaluma wa uhasibu pamoja na kuimarika kwa utawala bora na kuwa
chachu ya uchumi wa viwanda, kwa kuwa Kituo hicho, kinatoa elimu bora
itakayowawezesha wahitimu kuingia kwenye ushindani ndani ya nchi za
Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla.
Ujenzi
wa Kituo hicho umedhaminiwa na serikali kupitia mkopo kutoka Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii-NSSF, Bodi ya Uhasibu-NBAA na Mbia mwenza wa kituo
hicho, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali-GEPF.
Friday, December 2, 2016
Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi kufutia kifo cha SACP Peter Kakamba
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia
salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu
kufuatia kifo cha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Peter Kakamba kilichotokea tarehe 30
Novemba, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam
alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika
salamu hizo Rais Magufuli amesema anaungana na askari wote wa Jeshi la
Polisi, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na
kifo cha SACP Peter Kakamba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Natambua
mchango mkubwa alioutoa Marehemu (SACP) Peter Kakamba katika Jeshi la
Polisi na katika jukumu kuu la ulinzi wa raia na mali zao, kwa hakika
tumempoteza kiongozi aliyekuwa akifanya kazi zake vizuri” amesema Rais Magufuli.
“Nakuomba
IGP Ernest Mangu unifikishie salamu nyingi za pole kwa familia ya
marehemu, askari na wote walioguswa na msiba huu na sote tumuombee
Marehemu (SACP) Peter Kakamba apumzishwe mahali pema peponi, Amina” Amemalizia Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2016
Waziri wa Mambo ya Nje kuongoza ujumbe wa Tanzania Mkutano wa Mawaziri wa Afrika na Korea
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga (Mb) anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa
Mawaziri wa Afrika na Korea unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia
tarehe 06 na 07 Desemba, 2016 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano
huu ambao umeandaliwa na Serikali ya Korea kwa kushirikiana na Umoja wa
Afrika una lenga kukuza ushirikiano pamoja na kuandaa maeneo mapya ya
ushirikiano baina ya Korea na mataifa ya Afrika katika miaka mitatu
ijayo.
Tanzania
ni moja ya nchi nne (4) za Afrika ambazo Korea imezichagua kuanzisha
mahusiano ya kimkakati “strategic partnership” yatakayozifanya nchi hizo
kupewa kipaumbele katika kupokea misaada na mikopo nafuu kutoka Korea
katika kipindi cha miaka mitano ijayo kati ya 2016 hadi 2020.
Katika
kipindi hicho Tanzania itapokea kiasi cha dola za Kimarekani milioni
300 ikiwa ni asilimia 17.1 ya msaada utakaotolewa Barani Afrika, hivyo
kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza Barani humo kupata msaada wa
Jamhuri ya Korea.
Pamoja
na ushiriki kwenye Mkutano huo, imependekezwa ufanyike mkutano baina ya
Tanzania na Serikali ya Korea kuzungumzia masuala ya ushirikiano baina
ya nchi zetu mbili.
Aidha,
ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa Afrika na Korea ni fursa muhimu
ya kukuza mahusiano baina ya nchi zetu mbili hususan katika Nyanja ya
uchumi. Serikali ya Korea ilitoa ahadi ya kuongeza uwekezaji Barani
Afrika hususan katikasekta za nishati, miundombinu na viwanda.
Itakumbukwa
kuwa, tayari Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania katika miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Mradi wa kuendeleza kilimo cha Mwani
Zanzibar wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.6 na Awamu ya
Pili ya Mradi wa kuboresha Uchunguzi wa Afya ya Uzazi Jijini Dar es
Salaam wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni nne (4).
Miradi
mingine ambayo Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania ni ujenzi wa
Daraja la Selander Jijini Dar es Salaam, Mradi wa Daraja la Kikwete
kwenye Mto Malagarasi Mkoani Kigoma na Ujenzi wa Hospitali ya Kimataifa
iliyopo eneo la Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 01Desemba, 2016.
Friday, December 2, 2016
Askofu Gwajima akutwa na kesi ya kujibu.......Mahakama Yamtaka Ajieleze Disemba 13
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuona Askofu wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anayekabiliwa na kesi ya kushindwa
kuhifadhi silaha, ana kesi ya kujibu.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha alitoa uamuzi huo jana
baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa upande wa Jamhuri pamoja na
vielelezo.
Alisema
kutokana na ushahidi huo, ameona upande wa Jamhuri umejenga kesi hivyo
Gwajima na wenzake watatu, wana haki ya kujitetea, kuita mashahidi au
kukaa kimya.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa washtakiwa watajitetea kwa njia ya kiapo na watakuwa na mashahidi watatu.
Hakimu
Mkeha alisema Desemba 13, mwaka huu, washtakiwa watajitetea na siku
hiyo atasikiliza utetezi wa washtakiwa wote wanne pamoja na mashahidi
wao.
Mbali
na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu
huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi
wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31).
Inadaiwa
kuwa, Machi 29 mwaka jana, katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A,
washitakiwa walikutwa wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba
CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na
milipuko.
Aidha,
inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu
za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun. Gwajima
anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.
habari za leooo.
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 02, 2016
Rating:
Hakuna maoni