habario za leo hiii
Saturday, December 3, 2016
Tume ya Utumishi wa Umma Yazungumzia Kuhusu Kuwatumbua na Kuwadhalilisha Watumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma imetaja mamlaka sita zenye dhamana na madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma kisheria ikiwa pamoja na kufuta nafasi za madaraka.
Vilevile, Tume hiyo imezitaka mamlaka za nidhamu zote kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya hivyo, watumishi wanaotuhumiwa kufanya kosa watatendewa haki.
Tume ya Utumishi wa Umma imetoa maelekezo hayo siku chache baada ya viongozi wengi katika Serikali ya Awamu ya Tano wakiwamo wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia kiholela hatua za nidhamu watumishi wa umma wakati baadhi hawana mamlaka hayo kisheria.
Baadhi ya wakuu wa mikoa wamekuwa waki- wasimamisha watumishi hadharani tena kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja bila kuwapa walalamikiwa nafasi ya kujitetea, na wakati mwingine kudhalilishwa katika mikutano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi Tume hiyo, Enos Mtuso alisema kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma yako chini ya watu wachache.
“Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 ilitungwa ili kuweka misingi ya kisheria katika kutekeleza malengo ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma iliyopitishwa na Serikali mwaka 1998.
Sheria hii ndiyo inayotoa uwezo kwa mamlaka za kinidhamu mbalimbali katika utumishi wa umma na kuweka misingi ya namna masuala hayo yanavyopaswa kushughuliwa,” alisema.
Mtuso alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu, wakuu wa idara na divisheni, na mamlaka za Serikali za Mitaa (Baraza la Madiwani).
Lakini alipoulizwa mkuu wa mkoa anapata wapi mamlaka ya kuwafukuza kazi watumishi wa umma na kuwadhalilisha mbele ya hadhara, Mtuso alisema wao kama Tume hawana mamlaka ya kuzungumzia jambo hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiuka maadili na kwamba suala hilo liko chini ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Kauli ya Tume iliwekewa uzito na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo ambaye amewataka wakuu wa idara kuacha kuwanyanyasa wafanyakazi kwani hali hiyo inasababisha wafanye kazi kwa hofu ya kutumbuliwa.
Akizungumza baada ya kuwatembelea watumishi wa umma wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam jana, Jaffo alisema wizara yake itatoa ushirikiano kwa watumishi wote wanaofanya kazi kwa bidii.
Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.
Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.
Alisema Watumishi hao wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo, kukiuka maadili ya kazi, kutotekeleza majukumu, ubadhilifu, rushwa, wizi wa fedha na mali, udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe, utovu wa nidhamu huku utoro kazini ukiwa na idadi kubwa ya waliofukuzwa kazi.
“Utoro kazini ni changamoto kubwa inayotukabili na ndiyo mashauri yake mengi yanathibitika, unakuta mtumishi haendi kazini siku tano na kuendelea bila sababu maalumu wala hatoi taarifa yoyote kwa waajiri wake kuwa anashida gani,” alieleza.
Saturday, December 3, 2016
Lema Aiaga Rasmi Familia Yake .....Awataka Mawakili Wake Wasihangaike Tena, Asema Yupo Tayari Kukaa Gerezani Hadi Dola Itakapoamua
Baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kukwama tena kupata dhamana mahakamani jana, amewataka mawakili wake kutomhangaikia na kuliacha suala hilo kama lilivyo na atakaa gerezani hadi Januari mwakani.
Akizungumza baada ya Mahakama Kuu kuondoa rufaa ya mbunge huyo aliyekuwa akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumnyima dhamana, Wakili wa Lema, John Malya alisema mteja wake amewaomba kutokata tena rufaa na kuiachia Jamhuri iamue inavyotaka.
“Baada ya kujadiliana na mbunge, tumeona tufuate kwanza maelekezo yake ya kutofanya lolote juu ya maombi mapya ya dhamana,” alisema Malya.
Kutokana na maombi ya dhamana yake kukwama, Lema alirejeshwa kwenye Gereza la Kisongo ambako ataendelea kuwa mahabusi kusubiri hatima ya kesi inayomkabili.
“Tulikuwa na njia nyingi za kufanya kwa ajili ya kudai haki ya dhamana ya Lema lakini mbunge ameshatoa agizo hilo,” alisema Malya.
Aidha mke wa Lema, Neema Lema alisema amejadiliana na mumewe na kuona kinachoendelea kwenye shauri la kesi hiyo.
Aidha mke wa Lema, Neema Lema alisema amejadiliana na mumewe na kuona kinachoendelea kwenye shauri la kesi hiyo.
“Wanasheria walitoa ushauri wa nini kifanyike lakini mume wangu ameamua kisifanyike chochote kuanzia sasa. Pamoja na yote yanayotokea sasa ifike mahala ieleweke kuwa nchi si mali ya mtu yeyote, bali ni mali ya Watanzania wote,” alisema Neema.
Lema alikamatwa Novemba 2, akiwa bungeni Dodoma na kurejeshwa Arusha kujibu mashtaka ya kutoa kauli za uchochezi namba 440 na 441/2016.
Katika kesi hiyo, anadaiwa kuwa kati ya Oktoba 23 na 26 alitoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli katika maeneo tofauti wakati wa mikutano yake ya hadhara.
Katika kesi hiyo, anadaiwa kuwa kati ya Oktoba 23 na 26 alitoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli katika maeneo tofauti wakati wa mikutano yake ya hadhara.
Tangu wakati huo mawakili wake wamejitahidi bila mafanikio kumtoa kwa dhamana na ndipo baadaye walikata rufaa Mahakama Kuu ambako pia imeshindikana kwa maelezo kuwa iliwasilishwa nje ya muda wa siku 10 unaotakiwa kisheria.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Angelo Rumisha akisoma uamuzi wa Jaji Mfawidhi, Fatuma Masengi alitaja sababu za kuondolewa rufaa hiyo kuwa ni mshtakiwa kushindwa kuonyesha kusudio la kukataa rufaa ndani ya muda. Pia, alisema Mahakama Kuu inafungwa mkono kutoa uamuzi mwingine.
Rumisha alisema mshtakiwa alipaswa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa hiyo ndani ya siku 10, tangu uamuzi wa Mahakama ulipofanyika lakini badala yake upande wa utetezi ulikata rufaa nje ya siku 10.
“Maamuzi yalifanyika tarehe 11 , ilipaswa hadi Novemba 21 wawe wameonyesha kusudio la kukata rufaa lakini walikata rufaa tarehe 22,”alisema Msajili.
“Mahakama inaungana na pingamizi la Jamhuri, hivyo imeiondoa rufaa hii,” alisema.
Awali, Jamhuri ndiyo iliweka pingamizi, kupitia mawakili wake, Paul Kadushi na Matenus Marandu ikipinga kusikilizwa kwa maombi ya rufaa hiyo ya Lema iliyowasilishwa na wakili Peter Kibatala kwa maelezo imekiuka sheria.
Wakili Marandu alisema Kifungu cha Sheria 361 (1)(a) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kinataka mkataji rufaa kuonyesha nia ya kukata rufaa kwa kuandika notisi ya rufaa hivyo kuitaka Mahakama itupilie mbali rufaa hiyo.
Chadema wasikitika
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema kutokana na uamuzi huo, kwa sasa wanaheshimu uamuzi wa Lema kuiachia Jamhuri kuamua hatima yake.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema kutokana na uamuzi huo, kwa sasa wanaheshimu uamuzi wa Lema kuiachia Jamhuri kuamua hatima yake.
“Tumefedheheshwa sana na kitendo Msajili alichokifanya kuwa kama Lema ataongea mawakili wake watoke nje na kama haiwezekani asubiri mpaka pale atakapomaliza kusoma maamuzi,” alisema Amani
Wakati Msajili akitaka kusoma uamuzi huo jana saa 3:50 asubuhi, Lema alinyoosha mkono akiashiria kutaka kuongea lakini hakupewa ruhusa na Msajili. Badala yake alisema mawakili wake ndiyo walipaswa kutoa hoja ya mshtakiwa huyo kwamba kama Lema ataongea itabidi mawakili wake watoke nje.
Wakati Msajili akitaka kusoma uamuzi huo jana saa 3:50 asubuhi, Lema alinyoosha mkono akiashiria kutaka kuongea lakini hakupewa ruhusa na Msajili. Badala yake alisema mawakili wake ndiyo walipaswa kutoa hoja ya mshtakiwa huyo kwamba kama Lema ataongea itabidi mawakili wake watoke nje.
Baada ya uamuzi kufanyika, Wakili wa Lema Adam Jabir alisimama na kutoa hoja ya mbunge huyo kumuomba Msajili awaruhusu ndugu zake mshtakiwa waingie ndani ya Mahakama kusikiliza shauri lake baada ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi.
Msajili alijibu kuwa mahakama haina fedha za kununua vipaza sauti. Pia, alisema wamezuia watu wengine kuingia kwenye Mahakama hiyo kwa kuwa eneo hilo ni dogo. Lema amerudishwa mahabusu huku kukiwa na sintofahamu ya lini rufaa ya kupinga dhamana yake itasikilizwa.
habari ya hiv pundeeeeeee
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inahitaji
ushirikiano mkubwa na wafanyabiashara, hivyo haitakubaliana na mtumishi yeyote
wa umma atakayefanya urasimu kwa lengo la kukwamisha uboreshaji wa sekta
binafsi.
Amesema miongoni mwa maboresho yanayofanywa na Serikali katika
sekta binafsi ni pamoja na kuimarisha utendaji wa watumishi na kuondoa urasimu
katika utendajikazi wa kila siku baada ya eneo hilo limelalamikiwa sana.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Desemba 2,
2016) wakati akizungumza na wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda mkoani Arusha
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Ziara hiyo inalenga kuangalia utelelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya CCM,Utendaji wa Serikali, kusikiliza na kujionea kero zinazowakabili
wananchi wa Mkoa huo na kushirikiana na viongozi wa Mkoa ili kuweza
kuzipatia suluhisho.
“Serikali inafanya jitihada kubwa katika kuhakikisha inaweka
mazingira mazuri ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa nchi yetu. Pia mapambano
dhidi ya rushwa yanayofanyika ndani ya Serikali na nje yanalenga kuleta
maboresho makubwa katika sekta binafsi ,” alisema.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
habario za leo hiii
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 03, 2016
Rating:
Hakuna maoni