JUMATANO HABARI ZA LEO HIZI HAPA
Jumatano, 21 Desemba 2016
KUWAIT YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA UJENZI WA BARABARA MKOANI TABORA
Maafisa
waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Mwakilishi wa
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Mohammad Rashid Alamiri (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza katika Kikao kati yake na Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), katika Makao Makuu ya Wizara
ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza
na ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, kuhusu miradi ya
miundombinu itakayofadhiliwa na Mfuko huo, ukiwemo mradi wa barabara kwa
kiwango cha lami kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora. Kulia ni
mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini Bw. Mohammad Rashid Alamiri,
Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait
(Kuwait Fund) baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na wajumbe hao
ambapo mbali na kutoa mkopo wa ujenzi wa barabara kutoka Chaya kwenda
Nyahua mkoani Tabora, walionesha nia ya kutoa mikopo mingine yenye
masharti nafuu katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana
mkono na Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Bw. Mohammad Rashid Alamiri huku
wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mkunano kati yao uliojikita
katika mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi
mbalimbali ikiwemo barabara na sekta ya afya, Mkutano huo
umefanyikaatika Makao makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Wataalamu
toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (kushoto) na wataalamu kutoka
Tanzania (kulia) wakijadili kuhusu mkopo wa masharti nafuu kutoka
Serikali ya Kuwait, utakao saidia kujenga barabara Mkoani Tabora,
Mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, Jijini Dar es
salaam.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa dola za Kimarekani Milioni 34 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Bw. Mohammad Rashid Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, ulipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.
Dkt. Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi maeneo hayo kutokana na umuhimu wa barabara katika kukuza uchumi wa Taifa.
Amesema kuwa kipande hicho cha barabara kutoka Chaya hadi Nyahua, ambacho kiko Barabara Kuu itokayo Dar es salaam kwenda katika mikoa ya Tabora na Kigoma, licha ya umuhimu wake katika kukuza biashara na usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani, ilikuwa haijapata fedha kwa ajili ya ujenzi wake.
“Riba waliyoiweka mezani kwa mazungumzo ni asilimia 2 lakini nimewaomba waangalie uwezekano wa kuiteremsha walau ifikie asilimia 1.5 na wamependekeza kipindi cha kuanza kulipa mkopo kiwe miaka ishirini ijayo lakini nimewaomba wasogeze hadi kufikia miaka 25 kama ilivyo kwa mradi wa Hospitali ya Mnazimmoja” aliongeza Dkt. Mpango
Dkt. Mpango amesema Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake huo wa Maendeleo wameonesha nia ya kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyoko Visiwani Zanzibar.
“Nawahakikishia kuwa baada ya muda si mrefu wananchi wa mikoa ya Tabora na Kigoma watarajie kuona mkandarasi akiingia kazini ili kujenga barabara hii muhimu sana kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo kutoka Chaya hadi Nyahua unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 61 lakini Kuwait haitatoa fedha zote hivyo ameuomba Mfuko huo uangalie uwezekano wa kutoa kiasi hicho chote cha fedha ili uweze kukamilika mapema.
Jumatano, 21 Desemba 2016
WANANCHI KATA ZA KIPUNGUNI, KIVULE NA MZINGA WAPEWA ELIMU KUPINGA UKEKETAJI
Anna
Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada
katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote
za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo
vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna
Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada
katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote
za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo
vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Anna
Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada
katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote
za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo
vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Muwasilishaji
wa mada, Bi. Agnes Lukanga (kulia mbele) kutoka TGNP Mtandao
akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na
Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya
kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya
ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.
Mmoja
wa viongozi wa Dini, Issa Abdullah (mbele) akijadili jambo katika
mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili
wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika
Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia)
akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana
na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji.
Baadhi
ya washiriki wakiwa katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi
kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya
ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na
Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Shina namba Saba Majohe, Mohamed Kassim (mbele) akichangia jambo
katika mkutano huo wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo
vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo
ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar
es Salaam.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu
kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo
vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni,
Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu
kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo
vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni,
Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.
Wednesday, December 21, 2016
Rais Magufuli Akataa Shule Kuitwa Jina Lake
Rais John Magufuli amekataa shule ya msingi iliyojengwa hivi karibuni eneo la Bunju, Wilaya ya Kinondoni kuitwa kwa jina lake badala yake ameagiza iitwe kwa jina la Mkuu wa wilaya hiyo, Ally Hapi.
Taarifa ya badiliko la jina haikutolewa
na Idara ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kama ilivyozoeleka bali
na mkuu wa wilaya hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya
usafi kwa uongozi wa shule hiyo.
“Shule hii imejengwa kwa fedha
zilizopatikana baada ya Serikali Kuu kubana matumizi. Tukaamua iitwe
John Magufuli lakini yeye akatoa agizo shule ipewe jina la mkuu wa
wilaya sina budi kukubaliana na hilo,” alisema Hapi.
Shule hiyo mpya
iliyopo Bunju jijini imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa
wanafunzi katika Shule ya Msingi Bunju A ambayo ilikuwa na wanafunzi
3,224.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo mpya, Ali Mwakapalila alisema ingawa
inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 9 mwakani inakabiliwa na
changamoto mbalimbali.
“Hakuna umeme wala maji, hii inaweza kuleta
madhara kwa wanafunzi hasa linapokuja suala la matumizi ya vyoo,”
alisema.
Baada ya hafla hiyo, Hapi alikwenda kwenye kiwanda cha saruji
cha Twiga Cement ambako alipokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa
ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa na majengo mengine.
Akipokea
msaada huo, Hapi alisema msaada kutoka Twiga Cement unaunga mkono
juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoipa sekta ya elimu kipaumbele
ili kuhakikisha inatolewa katika mazingira bora.
“Msaada huu umekuja
muda muafaka. Tumeshajenga shule ila tunataka kuongeza madarasa,
maabara, ofisi ya elimu na kuzungushia uzio ili watoto wawe katika
mazingira salama. Lengo ni kuifanya shule hii iwe ya kisasa na itakuwa
mfano kwa shule zote za Wilaya ya Kinondoni,” alieleza.
Pia, Hapi
alisema wilaya hiyo ipo kwenye mipango ya kujenga maktaba ya kisasa kwa
kushirikiana na kampuni hiyo ya saruji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga
Cement, Alfonso Velez alisema kuchangia katika shughuli za kijamii ni
moja ya mambo ambayo wamekuwa wakiyapa kipaumbele zaidi.
“Kushiriki
shughuli za maendeleo katika jamii ni jambo ambalo tunalipenda zaidi.
Yalipo maendeleo Twiga Cement ipo pia,” alisema Velez.
Wednesday, December 21, 2016
Rais wa Gambia: Hakuna wa kunitoa Madarakani, labda Mungu Pekee
Rais
wa Gambia Yahya Jammeh amesema kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi
wa eneo la magharibi mwa Afrika la kumlazimisha kuondoka madarakani
licha ya kushindwa katika uchaguzi na mpinzani wake, Adama Barrow.
Akihutubia
Wanachama wa Muungano nchini humo Bw. Jammeh amesema: ”Waje wajaribu
kuniondoa wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi
kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka
mshindi”.
“Mimi sio muasi, haki yangu haiwezi kuvurugwa. Hii ni nafasi yangu, hakuna mtu anayeweza kuniondoa labda Mungu,” amesema.
Amesema
kuwa alikataa wito wa Muungano wa Viongozi wa Mataifa ya Magharibi
ECOWAS akiwemo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf
wa Liberia kuondoka nchini Gambia.
“’Wao
ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu,” amesema na
kuwashutumu viongozi hao kwa kuingilia mambo ya ndani ya Gambia.
ECOWAS
tayari imesema kuwa inamtambua Bw. Barrow kama Rais wa taifa hilo na
kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi
yanaheshimiwa.
Viongozi wa eneo hilo watahudhuria kuapishwa kwa Bw. Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.
Rais
Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo mnamo Desemba 1,
2016 lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya
uchaguzi inayomcha Mungu kwa madai kuwa matokeo hayo uchaguzi
yaligubikwa na dosari.
Wednesday, December 21, 2016
Majambazi Wawili Wauawa Jijini Mbeya Katika Mapambano Makali Kati Yao Na Jeshi La Polisi
Askari
wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi
katika mapambano ya kurushiana risasi na watu waliosadikiwa kuwa ni
majambazi na kuua wawili kati yao.
Taarifa
iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari
imesema kuwa mnamo tarehe 19.12.2016 majira ya saa 1:45 jioni katika
Kijiji cha Busisya, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi walipata taarifa za
siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha ambao walikuwa na lengo la
kufanya uvamizi katika Duka la Mfanyabiashara wa soda na bia za jumla
ambaye pia ni wakala wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao.
Askari
hao walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 1:45 jioni
askari walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki
ambapo baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari
walianza kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya
risasi kati ya askari na majambazi hao.
Askari
walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo
hapo na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.
Aidha
katika tukio hilo silaha bunduki tatu pamoja na risasi tisa ziliweza
kupatikana zilizokuwa zinatumiwa na majambazi hayo. Silaha hizo ni Mark
IV yenye namba 38482 na risasi mbili, Short Gun Greener yenye namba
G.73878 na risasi 01 na Gobole lililotengenezwa kienyeji ambalo halina
namba na risasi 06.
Pia
baada ya kupekuliwa majambazi hao walikutwa na vitu vingine ambavyo ni
Rungu moja, Praizi moja, Bisibisi moja, mafuta ya cherehani, koti la
ngozi rangi ya brown pamoja na begi dogo rangi nyeusi ambalo lilitumika
kuhifadhi vitu hivyo.
Miili
ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Makandana Wilaya
ya Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu na bado haijatambulika. Msako
unaendelea. Katika tukio hilo hakuna mali iliyoporwa wala askari kupata
madhara. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea,
Upelelezi unaendelea.
Wednesday, December 21, 2016
Maoni Sheria ya Huduma za Habari mwisho Januari 10
Wednesday, December 21, 2016
Wizara yalaani Ukeketaji wa Watoto maeneo ya Kivule, Dar es Salaam
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakemea vikali
vitendo vya ukeketaji vinavyotaarifiwa kufanyika katika Kata ya Kivule,
Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, na mikoa mengine ambayo
imekaririwa na vyombo vya habari.
Wizara
inaagiza wazazi na walezi kuacha mara moja vitendo vya ukeketaji kwani
ni ukatili, husababisha madhara kwa watoto wa kike na wasichana ni kosa
la jinai.
Athari
za ukeketaji kwa wahanga ni pamoja na kusababisha majeraha kwa watoto,
vifo, vilema, maradhi kama fistula na mengineyo. Watoto wa kike na
wanawake wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa vitendo vya ukeketaji bila
ridhaa yao na wakati mwingine ridhaa hiyo huwa imepatikana kwa hila,
jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Wizara
inatoa rai kwa vyombo vya dola kuwakamata wazazi, walezi, mangariba, na
wote wanaoendeleza vitendo vya ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na
wasichana katika kata ya Kivule na maeneo mengine nchini, na kuwafikisha
mahakamani ili sheria iwezekuchukua mkondo wake.
Wizara
itaendelea kupambana na vitendo vya ukeketaji vinavyotaarifiwa katika
jamii zetu, na itaongeza juhudi ya utoaji elimu kwa jamii sambamba na
kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na mila potofu ya ukeketaji.
Wito
unatolewa kwa kila mwananchi kushiriki katika kuzuia vitendo vya
ukeketaji na hasa kufichua matukio ya ukeketaji, na kutoa ushahidi
mahakamani ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Wizara
inatoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii
katika Mikoa, Halmashauri na Kata katika maeneo ambako kunaarifiwa
kuwepo vitendo vya ukeketaji kuhakikisha kuwa wanashirikiana na mamlaka
husika kuzuia ukatili huo katika nchi yetu.
Msemaji wa Wizara-Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
21/12/2016
Wednesday, December 21, 2016
Jeshi la Polisi Lasema Linaendelea kuchunguza alipo msaidizi wa Mbowe, Ben Saanane.......Latoa ufafanuzi kuhusu maiti saba
Ukiwa
umetimia mwezi mmoja, baada ya Msaidizi wa Freeman Mbowe ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benard
Saanane (pichani) kupotea, Jeshi la Polisi limesema linachunguza taarifa
za kupotea kwake ambazo ilizopokea kutoka kwa mtu aliyejitambulisha
kama rafiki wa Saanane Desemba, 5, 2016.
Wakati
akizungumza na waandishi wa habari, Desemba 21, 2016 Kaimu Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz amesema Jeshi la polisi
limefungua jalada la uchunguzi na kwamba taratibu za kiupelelezi za mtu
aliyepotea zilifuatwa na bado upelelezi wa suala hilo unaendelea.
“Tuanashukuru
wananchi wanaotupatia taarifa kuhusu tukio hilo, tunaahidi kwamba
taarifa hizo tutazifanyia kazi. Tunazidi kuwaomba wananchi wenye taarifa
za kupotea Saanane waziwasilishe katika kituo chochote cha polisi,” amesema.
Sambamba
na hilo, Kamishna Boaz amefafanua tukio la uzikwaji wa maiti saba
zilizokufa maji katika mto Ruvu, pasipo kufanyiwa uchunguzi wa kutambua
waliokufa na chanzo cha vifo vyao.
“Mtakumbuka
kati ya tarehe 6 hadi 12, 1016 huko mto Ruvu jeshi la polisi lilipata
taarifa ya kuonekana maiti saba zikiwa zinaelea mtoni kwa nyakati na
maeneo mbalimbali, baada ya taarifa hizo kupatikana askari na daktari
walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitaalamu,” amesema na kuongeza.
“Kutokana
na ukweli kwamba baadhi ya maiti zilikuwa zimeharibika, maiti 6
ziliamuliwa kuzikwa katika eneo la tukio na moja yenye unafuu ilipelekwa
hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwenye chumba cha maiti hadi pale
ilipozikwa na halmashauri baada ya maiti hiyo kutotambuliwa na mtu
yeyote.”
CP
Boaz amesema hatua zote za kitaalam zilifuatwa na kwamba upelelezi
unaendelea kufanywa ikiwemo wa kuwatambua marehemu hao na kujua chanzo
cha vifo vyao
Wednesday, December 21, 2016
Mapya Yaibuka Sakata la Bwana harusi Aliyemkimbia Bi Harusi Siku ya Ndoa
Mapya
yameibuka sakata la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Samwel Mwakalobo na
Ginen Mgaya, baada ya kubainika kuwa moja ya sababu ni Bibi harusi
mtarajiwa kuendeleza uhusiano na mzazi mwenzake.
Bwana harusi, Samuel Mwakalobo alitoweka muda mfupi kabla ya kufunga
ndoa na Ginen Mgaya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Usharika wa Isanga jijini Mbeya.
Mwakalobo (26) alizua taharuki hiyo Ijumaa ya Desemba 16, baada ya
kutoonekana kanisani kufunga ndoa mbele ya Mchungaji Andagile
Mwakijungu.
Habari
zimedai kuwa kabla ya mpango wa kufunga ndoa hiyo, Mgaya tayari
alishapata mtoto kabla hajaolewa, na Bwana harusi kubaini dakika za
mwisho kuwa wawili hao walikuwa bado wana uhusiano wa karibu.
Habari
hizo za ndani kutoka familia ya Bibi harusi, zilidai kuwa kilichofanya
Bwana harusi amtelekeze Bibi harusi ni wasiwasi aliokuwa nao juu ya
uhakika wa ujauzito wa mkewe huyo mtarajiwa, kuwa ni wake kweli au wa
mpenzi wake huyo wa zamani.
“Hofu
hiyo ilijengeka kutokana na taarifa alizoziamini Bwana harusi kuwa Bibi
harusi anaendeleza uhusiano na mzazi mwenziwe. Ni hofu tu ambayo
angeifanyia kazi na angegundua kuwa haina ukweli wowote,” kilidai chanzo hicho.
Chanzo hicho kiliendelea kudai:
“Unajua muda mwingine binadamu tunahitaji kufanya uamuzi kwa kutafakari
… maana shemeji yetu (Bwana harusi) alipigiwa simu na mzazi mwenza wa
Bibi harusi na kuelezwa maneno ya ‘shombo’ na yeye bila kufanyia
utafiti, akaamua kususa harusi.”
Wakati
taarifa hizo zikibainisha hayo, familia ya Bwana harusi imeendelea
kufanya jitihada za kuhakikisha suala hilo linamalizika kistaarabu.
Anayeelezwa
kufuatilia suala hilo kwa karibuni ni kaka yake, ambaye hadi jana
jitihada za kumtafuta mdogo wake zilikuwa zimeshindikana kutokana na
kutopokea simu yake ya mkononi mara zote.
“Anayeongoza
familia ya Bwana harusi ni kaka yake. Inasemekana pia kuwa wawili hao
waliingia kwenye mgogoro dakika za mwisho kabla ya harusi na ndiyo maana
baada ya kutoweka hataki hata kupokea simu,” kilieleza chanzo kingine.
Awali,
mpambe wa Bibi harusi alieleza kuwa siku mbili kabla ya harusi hiyo,
Bwana harusi alikuwa kwenye migogoro ya kifamilia na ndugu zake kuhusu
fedha za sherehe na mpaka siku ya sherehe, suala hilo walikuwa
hawajalitatua.
“Lakini
tunashukuru kaka yake ni mstaarabu, aliamua kuonesha upendo kwa mdogo
wake na amekuwa akilifuatilia suala hilo ili limalizike kwa amani,
lakini mdogo mtu hapatikani,” alisema mpambe huyo.
Alisema
jitihada za Bibi harusi kumtafuta Bwana harusi hazijazaa matunda, kwani
hadi juzi alikuwa hapatikani hata nyumbani kwake, ingawa redio ilikuwa
inasikika ndani ya chumba hicho kilichofungwa kufuli kwa nje.
Simu
ya Bwana harusi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokewa, lakini hatua
zingine zilidai kuwa Bwana huyo ambaye ni mfanyabiashara kwenye kituo
cha mabasi yaendayo Chunya eneo la Isanga jijini Mbeya hajafungua duka
lake.
Wednesday, December 21, 2016
Ahukumiwa Miaka 25 Jela Au Faini Bilioni 3.7 Kwa Kujihusisha na Biashara ya Meno ya Tembo
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Tanga, imemtia hatiani na kumuhukumu kwenda jela miaka
25 au kulipa faini ya Sh bilioni 3.7 mfanyabiashara Charles Kijangwa kwa
kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.
Kijangwa
alihukumiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cresencia Kisongo,
baada ya kuruka dhamana kwa miaka sita. Alishindwa kulipa faini.
Mshtakiwa
huyo alikabidhiwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa na askari wa
kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana
na Jeshi la Polisi Wilaya ya Lushoto.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Saraji Iboru, alidai mahakamani kuwa mshtakiwa
Kijangwa alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu mwaka 2010
baada ya kuruka dhamana katika shauri la uhujumu uchumi namba 6/2007.
Mshtakiwa
alishtakiwa na wenzake Michael Msuya na Nyaisa Makori ambao walitiwa
hatiani na mahakama, wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la
kumiliki kilo 5,000 za meno ya tembo kwa shtaka la kwanza.
Katika
shtaka la pili la kula njama, washtakiwa wote walihukumiwa kwenda jela
miaka mitano au kulipa faini ya Sh 10,950,000 baada ya kupatikana na
hatia ya kusafirisha kilo 5,000 za meno ya tembo kwenda nchini Taiwan
mwaka 2006.
Iboru
aliiambia mahakama kuwa washtakiwa watatu, Kijangwa na wenzake
walihukumiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya Sh 50,000 katika
shtaka la kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali kinyume cha
sheria.
Alidai mshtakiwa hakufika mwenyewe mahakamani hapo bali aliletwa baada ya kukamatwa Desemba 11, mwaka huu wilayani Lushoto.
Aliiomba mahakama kumtia hatiani mshtakiwa na kuhakiksha anatumikia adhabu iliyotolewa dhidi yake akiwa hayupo.
Hakimu
Kisongo baada ya kusikiliza maombi hayo, alimtia hatiani mshtakiwa na
kumuhukumu kwenda jela miaka 25 au kulipa faini ya Sh bilioni 3.7.
Mshtakiwa
Kijangwa alitenda kosa hilo Novemba 2005 na Aprili 2006 kwa kusafirisha
makontena mawili ya meno ya tembo yenye ujazo wa tani 5,000
yaliyokamatwa katika bandari ndogo ya Konshugi nchini Taiwan.
Makontena
hayo ambayo yalitokea katika Bandari ya Tanga yakiwa na shehena ya
kamba za katani na meno ya tembo ndani yake, yalikuwa yanapelekwa Manila
nchini Philipine.
Wednesday, December 21, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 21
JUMATANO HABARI ZA LEO HIZI HAPA
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 21, 2016
Rating:
Hakuna maoni