ijumaaa hiii
Friday, December 23, 2016
Dereva bodaboda akatwa sikio kwa tuhuma ya kufumaniwa na mke wa dereva teksi
Dereva
bodaboda wa Mji Mdogo wa Qatesh wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara,
amekatwa sikio kwa kisu kwa tuhuma za kufumaniwa akiwa na mke wa dereva
wa teksi.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Francis Massawe
alisema tukio hilo lilitokea Desemba 21 saa 6:10 usiku kwenye Kitongoji
cha Qendangonyi, Kata ya Ganana wilayani Hanang’.
Kamanda Massawe alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na majeruhi amepata kilema cha maisha baada ya sikio kutolewa.
Alisema wanamshikilia dereva teksi kwa uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani
riday, December 23, 2016
Rais Magufuli Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Wamtembelea Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo
Rais
wa Tanzania Dkt. John Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli
wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es
Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Hatua hiyo ni kufuatia kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22 Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa na umri wa miaka 79.
Mhe.
Rais Magufuli na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali
Pengo katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Friday, December 23, 2016
Picha: Mwenyekiti Mpya Wa NEC Jaji Semistocles Kaijage Aanza Kazi Rasmi.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto)
akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji
wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi
za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles
Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo
kwa kipindi cha miaka 5.
Baadhi
ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti
mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti
mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza
mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa
kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20
Desemba, 2016.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
Mwenyekiti
mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
Friday, December 23, 2016
Rais Magufuli Akutana Na Waziri Mkuu Majaliwa Ikulu Jijini Dar
Rais
John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ikulu
jijini Dar es salaam Desemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu jijini Dar es salaam, Desemba 23, 2016.
Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu jijini Dar es salaam, Desemba 23, 2016.
Rais
John Magufuli akizungumza na mtoto Doreen Ndika ambaye aliambatana na
baba yake, Jaji Dkt. Gerald Ndika aliyeapishwa na Rais `Ikulu jijini
Dar es salaam Desemba 23, 2016 kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Friday, December 23, 2016
Rais Magufuli Afanya Uapisho Wa Mwenyekiti NEC , Kamishna Wa Maadili Na Majaji Wa Mahakama Ya Rufani
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
23 Desemba, 2016 amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya
Rufani aliowateua jana tarehe 22 Desemba, 2016.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na Viongozi wengine mbalimbali.
Walioapishwa ni Mhe. Mhe. Jaji Semistocles Simon Kaijage aliyeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Viongozi hawa watashika nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa upande wa Majaji walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi na Mhe. Jaji Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika, Mhe. Jaji Jackobs Casthom Mwatebela Mwambegele.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yesamin Eralp ambapo viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki hususani katika masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kufuatia kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22 Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa na umri wa miaka 79.
Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali Pengo katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Desemba, 2016.

Jaji Semistocles Kaijage akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kiapo
cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mohamed Hamid kuwa Makamu kuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapishaJaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela kuwa Kamishna wa
Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalaliwa Mwangesi kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
vitendea kazi Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
riday, December 23, 2016
Madereva Wazembe Kuwekwa Selo Badala ya Kulipa Faini
JESHI
la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini limesema litachukua
hatua kali kwa kuweka mahabusu madereva watakaokiuka sheria za usalama
barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu badala ya kulipa faini kama
ilivyozoeleka.
Kauli
hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Kikosi hicho,
Mohammed Mpinga, alipozungumza na vyombo vya habari akisema kutoza
faini kumekuwa hakuwafanyi madereva kuacha kuvunja sheria.
“Kitendo
cha kutoza faini, kimekuwa kikiwafanya madereva kuvunja sheria kwa
makusudi, wakijua wakikamatwa watalipa faini na kuachwa,” alisema
Mpinga.
Mpinga
alisema katika kipindi hiki, watu wengi hupenda kusafiri kwenda maeneo
mbalimbali na hivyo kuongeza matumizi ya vyombo vya moto barabarani
ambapo pia huambatana na starehe nyingi ikiwa ni pamoja na ulevi kwa
madereva.
Alieleza
kutokana na hali hiyo ya starehe na ulevi, madereva wengi hupoteza
umakini na kushindwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hatimaye
kusababisha ajali ambazo hugharimu maisha ya watu wengi.
Alifafanua,
kwamba kipindi hiki madereva huwa na haraka na huendesha kwa mwendo
kasi, hunywa pombe, hupenda kupita magari ambayo ya mbele yao bila
hadhari na hufanya makosa ya kizembe yanayohatarisha maisha.
Kamanda
Mpinga alisema kwa kutambua hilo, wamejipanga ili kuwatia mbaroni
madereva hao na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Aidha,
alisema katika kipindi cha kuelekea mwishoni na mwanzoni mwa mwaka
mpya, wamekuwa wakifanya operesheni katika barabara zote, stendi za
mabasi ili kukagua ubora wa mabasi, mikanda, kupima ulevi madereva,
uzidishaji abiria na nauli.
Alisema
katika operesheni hii inayoendelea mikoani kwa kipindi kifupi madereva
wa mabasi ya abiria wamekamatwa kwa mwendo kasi wa zaidi ya kilometa 90
kwa saa, ambapo katika mikoa tofauti jumla ya madereva 277 walifikishwa
mahakamani wakitokea mahabusu na kulipa faini ya kati ya Sh. 300,000 na
Sh 600,000
ijumaaa hiii
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 23, 2016
Rating:
Hakuna maoni