Thursday, 29 December 2016

Mapya Yaibuka Sakata la Kijana Aliyefariki Baada ya Nyoka wake Kuuawa na Wananchi

Tukio  la kushangaza lililohusishwa na kifo cha Denis Komba (24) baada ya nyoka aliyekuwa naye kuuawa, limechukua sura mpya baada ya mambo kadhaa kuibuka.

Hayo ni pamoja na familia kudai mzoga wa nyoka na kwenda nao kuuzika nyumbani, jambo lililoendelea kuhusisha suala hilo na imani za kishirikina.

Imeelezwa kuwa familia ilielezwa na mganga wa kienyeji kuwa mwili uliohifadhiwa hospitali, si wa mtoto wao, jambo lililowafanya kuuchukua mzoga wa nyoka na kwenda kuuweka katika mfuko wa sarandusi (kiroba) na kuuzika.

Hata hivyo, mashuhuda walieleza kuwa, familia hiyo ilikikata kichwa cha nyoka na kukizika kivyake na kiwiliwili sehemu nyingine huku mwili wa Komba ambaye naye alizikwa jana, ukizikwa katika kaburi eneo lingine tofauti. Tukio hilo ni la juzi na lilimhusu Komba, mkazi wa Mateka, manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Nyumbani kwao ni kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Songea. Kabla ya maziko, baadhi ya vijana waliokuwa wamebeba jeneza, walikuwa wakikimbia nalo mwendo wa mchakamchaka huku wakiimba “mkimbize mkimbize nyoka awahi asije kudhuru watu wengine”.

Katika maziko hayo, hakuna ndugu aliyeonekana kulia wala hakukuwa na ibada yoyote wakati jina la marehemu linadhihirisha kuwa ni wa imani ya Kikristo. 
Wakati hayo yakiendelea msibani, baadhi ya watu wake wa karibu walidai alikuwa na tabia ya kucheza na nyoka mara kwa mara.

Hata hivyo, baba mzazi alikana kumuona mwanawe na nyoka. Naye daktari aliyechunguza mwili, alisema kifo cha Komba kinatokana na kugongwa na nyoka mwenye sumu kali, lakini hakuna jeraha wala alama yoyote iliyoonekana katika mwili huo.

Habari zinaeleza kuwa juzi familia ilikwenda kuzungumza na watu wa Idara ya Maliasili, waliochukua mzoga wa nyoka kwa uchunguzi kama nyara ya serikali. Walikubaliana kuwa familia itakwenda kuufukia na ndipo Maliasili walimrudisha nyoka hadi eneo la tukio na familia kumchukua.

Ilielezwa kuwa hatua hiyo, inatokana na madai kuwa kuna mganga amehusisha mzoga wa nyoka huyo na mwili wa Komba.

Watu wa karibu wa familia hiyo, ambao hawakutaka kutaja majina yao wakiwemo mafundi seremala na majirani, walieleza kuwa familia wakiongozwa na baba mzazi Sevelin Komba, walirudi eneo la tukio baada ya kutoka kwa mganga wa kienyeji na kumchukua nyoka na kumpeleka nyumbani.

Habari zinaeleza kuwa familia baada ya tukio hilo, walikwenda kwa mtaalamu wa mambo ya asili (mganga wa kienyeji) ambaye hakufahamika mara moja na kuelezwa kwa nini wamekubali kumuacha mtoto wao akiteseka juani kwani mwili walioupeleka nyumbani kutoka hospitali si wa Denis (Komba).

Aidha familia baada ya kumchukua nyoka huyo eneo la tukio alikouawa, baada ya kufikishwa nyumbani alikatwa kichwa kwa makubaliano ya familia ya marehemu na kiwiliwili kuzikwa tofauti na kichwa katika mfuko wa sarandusi. Baba mzazi alikanusha suala hilo la kwenda kwa mganga.

Katika maziko hayo, hakukuwa na chakula wala matanga na watu wengi walijitokeza ili kushuhudia kitakachoendelea.

Amuua Rafiki Yake, Ala Ubongo wake na Sehemu Za Siri

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamshikilia mchimba dhahabu, Shija Salum (38), mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua rafiki yake na kula ubongo wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba pamoja na mtuhumiwa huyo kula ubongo wa rafiki yake huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Shija, pia alitafuna sehemu zake za siri baada ya kuzikata.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu, usiku katika Kijiji cha Manyanya, Kata ya Makongorosi, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Alisema mtuhumiwa na marehemu walifika kijijini hapo wakitokea Shinyanga miezi mitatu iliyopita.

“Inasemekana wawili hao walikuwa ni marafiki kwani walifika wilayani Chunya, Kata ya Makongolosi kwenye machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na mfanyabiashara mmoja aitwaye Teddy Mwantega.

“Siku hiyo ya tukio, marehemu Shija, alikuwa amejilaza mahali na hapo ndipo alipofika rafiki yake huyo, akiwa na panga mkononi na kumkata kwa nguvu kichwani.

“Baada ya hapo, alimvua nguo na kuzikata sehemu zake za siri na kuzishika mkononi.

“Wakati akiwa na sehemu hizo za siri mkononi, alichukua ubongo wa marehemu na kuula, kisha akatafuna zile sehemu za siri.

“Kwahiyo, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” alisema Kamanda Kidavashari
 
 
Habari kwa mujibu wa 
Dunia Kiganjani Blog

BENKI YA KILIMO YAMUAGA DR. TONIA KANDIERO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto) akimpatia Zawadi ya Ramani ya Tanzania Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia).
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia aliyesimama) akizungumza wakati alipotembelea TADB. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga.
Afisa anayeshughulikia masuala ya kijinsia katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bibi Beatrice Mrema akitoa neno la Shukrani kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Wapili kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na maafisa waandamizi wa TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Katikati) akimkaribisha Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia). Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia) akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipotembelea TADB. Anayemtazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru (Aliyesimama) akizungumza wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Aliyesimama) akizungumza wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Wapili kulia aliyesimama) akihimiza jambo wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.

JESHI LA POLISI ARUSHA:WATAKAOCHOMA MATAIRI,FAINI MILIONI NNE,MADEREVA WALEVI KUKAMATWA NA KUNYANG'ANYWA LESENI,WAZAZ I/WALEZI WATAKAOWAACHA WATOTO WAKAZURURA OVYO KUSHTAKIWA,WENYE VIBALI VYA KUFYATUA FATAKI KUTUMIA DAKIKA TATU TU

Image result for kamanda wa polisi charles mkumbo 
Na.Vero Arusha.


Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema kuwa katika kusheherekea mwaka mpya ,kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya watu kufanya matukio ya kuhatarisha usalama kwa kuchoma matairi,kupanga mawe barabarani,na hata kuwarushia mawe askari pindi wanapothibiti matukio hayo,haswa maeneo ya majengo,kwa mrombo,kwa mrefu huku wengine wakitumia mwanya huo kufanya uhalifu.

Kwa wale watakaochoma na watakaokamatwa wamechoma matairi barabarani,wakumbuke kwamba watashtakiwa kwa sheria za Tanroad, ambapo watatakiwa kulipa faini isiyopungua milioni nne

Lakini pia baadhi ya madereva huwa wanatumia vilevi kupita kiasi katika majumba ya starehe inapofika saa 00:00 usiku unapoanza mwaka mpya huwa wanashangilia kwa kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi na kupiga honi mitaani huku wakiwa wamepakia watu kwa kuwaning’iniza milangoni kama njia ya kuonyesha furaha zao.

Uzowefu unaonyesha kwamba maeneo ya sakina mpaka kwa iddi baadhi ya madereva wanatuamia magari aina ya altezana Subaru huwa wanafanya maonyesho kwa kuendesha mwendo kasi vyombo hivyo huku vikitoa sauti kama risasi.

Kwa upande wa wamiliki wa bar wazingatie masharti ya leseni zao ambazo zinaonyesha muda halisi wa kufunga na wasiwe na tama ya kuendelea kupata pesa baada ya kuona wateja wengi katika biashara ,hali kadhalika wamiliki wa kumbi na maeneo mengine ya starehe wanatakiwa kuzingatia usalama katika maeneo yao hasa kwa kuweka wasimamizi na kutojaza watu kupita kiasi.

Aidha wazazi na walezi tunawakumbusha pamoja na kusheherekea mwaka mpya wa 2017 wasisahau majukumu yao ya kuwa makini na watoto kwa kutowaacha peke yao na hata kutoacha mtu yeyote katika majumba ili kuondokana na matukio yanayoweza kuepukika sambamba na kuangalia watoto wao katika maeneo ya round about hasa kijenge mnara wa mwenge,wasizagae barabarani

Jeshi la polisi linatoa onyo kwa baadhi ya watu watakaofanya makosa yaliyoorodheswa hapo juu ,tutawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wawe wahalifu ,wamiliki wa bar na kumbi nyingine za starehe pamoja na wazazi au walezi na madereva walevi ambao pia watapima na ikithibitika wamevuka viwango tutawafungia leseni.

Kwa upande wa waaliomba vibali vya kufyatua fataki ,watatakiwa watumie dakika tatu na wote kwa pamoja watatakiwa kufyatua saa 00:00 na pia hawataruhusiwa kufyatua katika makazi ya watu.

Tutahakikisha nyumba zote za ibada ,kumbi za starehe na maeneo mengine kutakuwa na ulinzi wa kutosha ambapo askari watakuwa katika doroa za miguu na doria za magari kila kona ya jiji la Arusha na wilaya zote za mkoa huu ,hivyo waumini wa dini mbalimbali wasiwe na hofu pindi watakapokuwa wanaendelea na ibada.

Kama ilivyo kwa nyakati zote tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana nasi katika kuwabaini na kuwafichua wahalifu na uhalifu ili kuimarisha amani na utulivu uliopo.

Mwisho tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari radio,magazeti,blogs,televisheni,kwa  ushirikiano mkubwa mnaotoa kwa jeshi la polisi mkoa wa Arusha kwa kuwa mbele katika kufichua, kuelimisha,na kuhabarisha umma juu ya uhalifu.

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha tunawatakia heri ya mwaka mpya wa 2017 wakazi wote wa Arusha .

       IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA

                         NAIBU KAMISHANA WA POLISI

                          (DCP)CHARLES MKUMBO

                                  TAREHE 29/12/2016


HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha limeanza utekelezaji wa Agizo la Rais
John Pombe Magufuli la kuwatafutia wafanya biashara wadogo ‘machinga’
eneo salama kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

Katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, sambamba na kuondoa
kero hiyo, uongozi wa Jiji la Arusha umenza hatua za awali za kujenga
jengo la kufanyia shughuli wafanyabiashara wadogo maarufu kama
‘Wamachinga complex.

Mradi huo unaolengwa kufanyika katika eneo lililopo mkabala na soko la
kilombero kiwannja Namba 69 chenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja,
lililorejeshwa hivi karibuni serikalini na waziri mkuu, Kasim Majaliwa
wakati wa ziara yake mkoani Arusha.

Akiliongelea suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,
Athumani Kihamia alisema eneo hilo lina uwezo wa kuhifadhi
wafanyabiashara wadogo zaidi ya 2000 pamoja na shughuli zao mara baada
ya mradi wa kujenga miundombinu utakapokamilika.

“Baada ya agizo la Rais na kero inayojitokeza tumeamua kufanya haraka
zaidi ambapo hadi jana tumeshaunda kamati inayofanya tathmini ya
ujenzi wa eneo hilo, na lengo ni kuakikisha tutawaondoa
wafanyabiashara kutoka kwenye maeneo hatarishi ambayo wengi ndio
wanayatumia kufanya shughuli zao, hii ni pamoja na kando za barabara
ya Maromboso, stendi kuu na ile ya Col. Middleton,” alisema Kihamia

“Pamoja na kuwa katika uongozi wa jiji ukiwaandalia maeneo mengine ya
kufanyia biashara zao, ni vizuri wafanyabiashara hawa waendeleze
shughuli kwa busara bila kuvunja sheria, hususan za barabarani au
kuvamia sehemu za maduka na biashara za watu wengine, ikiwemo kujali
usalama wao binafsi,maana sasa wamefunga hata badhi ya barabara,”
alisema Kihamia.

Mmoja wa wafanyabiashara wadogo anayeuza viatu, Hussein Issa, ameomba
kusiwepo na urasimu wakati wa ugawaji wa maeneo ya biashara
yaliyotengwa; “tatizo wala sio wingi wa wamachinga, bali ni kwamba
vingozi wakubwa huwa wanahodhi maeneo hayo ili baadae waje kuwauzia
watu wengine, sasa unakuta mtu anamiliki maeneo zaidi ya kumi peke
yake ili ayauze au awakodishie watu,” alisema.

Serikalini yatahadharisha wananchi Arusha na baa la njaa

MWANAFUNZI AFA MAJI AKIOGELEA HOTEL YA MOUNT MERU ARUSHA

Mount Meru Hotel
Mwanafunzi  wa darasa la tano  shule ya msingi ya Sekei iliyopo
halmashauri ya Arusha DC wilayani Arumeru Criff Laiza (12), amekufa
maji wakati akiogelea kwenye  bwawa la maji yenye kina kirefu katika
hotel ya kitalii ya Mount Meru iliyoko jijini Arusha .


Tukio hilo limetokea Desemba 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni
wakati marehemu na watoto wengine wakiogelea katika hotel hiyo ikiwa
ni sehemu ya kusheherekea sikukuu ya X-mass .


Kaimu Meneja wa Hotel ya Mount Meru, Eric Mgenya akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na atalitolea ufafanuzi
baada ya polisi kukamilisha upelelezi wa tukio hilo.


Alisema  baada ya kutokea uongozi wa hotel hiyo, walitumia gari aina
ya Noah lenye namba T.883 DJM pamoja na gari dogo lenye namba T.445
BSC aina ya Toyota Corrola walipakia mwili wa marehemu kwa lengo la
kuokoa uhai wake na walipofika katika hospital ya Aicc na mwili huo
kupimwa waliarifiwa kuwa tayari marehemu alishafariki kitambo.


Baadhi ya watoto  waliokuwa wakiogelea na marehemu  katika hotel hiyo
walisema, marehemu Laiza alihama ghafla kwenye bwawa la watoto na
kwenda kuogelea bwawa  linalotumiwa na watu wazima ambalo wakati huo
hapakuwa na mtu yoyote akiogelea, lakini ghafla hakuonekana tena hadi
alipo kutwa ameelea juu ya maji .


Kwa upande wake Babu wa mtoto huyo Emanuel Meage alisema tukio hilo
limeshtua sana, kwani  mjukuu wake aliaga kuwa anaenda kuogelea katika
hotel hiyo na wenzake hata hivyo alishangaa kupata taarifa za mjukuu
wake kufa maji.


Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wazazi  ambao hawakutaka kutaja
majina yao wameutupia lawama uongozi wa hotel ya hiyo kwa kushindwa
kuwa na usimamizi mzuri na ulinzi wa watoto hao, badala yake wamekuwa
wakijali kukusanya fedha ya kuogelea na kuwaacha watoto wafanye
wawezavyo kitendo ambacho sio sahihi wakidai kuwa eneo hilo ni hatari
na  sio salama kwa mazingira ya mtoto .


Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo alithibitisha tukio
hilo na kueleza kuwa polisi wapo katika hatua ya uchunguzi na
atalitolea ufafanuzi, mara baada ya uchunguzi kukamilika na hakuna mtu
yoyote hadi sasa anashikiliwa kutokana na tukio hilo.

Kijana afariki dunia baada ya Nyoka wake kupigwa hadi kufa

SeeBait

Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) afariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIDAIWA KUNYWA SODA YA MWENZIE SIKU YA KRISMASI

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mkazi wa Olasiti, jijini Arusha, Hamisi Amani (17), kwa tuhuma za kumuua mwenzake wakati wakigombea soda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu, saa mbili usiku katika eneo la Kwa Morombo.

Kamanda Mkumbo alimtaja marehemu kuwa ni Novatus Tadei (26), mkazi wa Kwa Morombo na kwamba aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto.

“Marehemu na mtuhumiwa walikuwa wapishi kwenye kampuni inayojulikana kwa jina la ZZ Catering inayomilikiwa na Bashiri Ally.

“Siku ya tukio, marehemu pamoja na wafanyakazi wengine, akiwamo mtuhumiwa, baada ya kumaliza kazi waliyokuwa wanafanya, walipanda gari lenye namba za usajili T 375 CHH, aina ya Toyota Hiace wakirejea nyumbani.

“Wakiwa ndani ya gari hilo, mtuhumiwa Hamis aligundua kuwa soda aliyokuwa ameiweka ndani ya begi lake, haipo na kuanza kuhisi marehemu ndiye aliyeichukua.

“Kwa hiyo, ulizuka ugomvi baina yao na kuanza kutukanana matusi. Wakati ugomvi huo ukiendelea, mtuhumiwa alimkaba marehemu na kuchukua kisu wanachotumia kwenye shughuli zao za mapishi kilichokuwa ndani ya vyombo na kumchoma kifuani.

“Baada ya kuchomwa kisu, Tadei alianguka chini na jitihada za wafanyakazi wenzake waliokuwamo ndani ya gari hilo kuokoa maisha yake zilishindikana, kwani alifariki wakati anapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu,” alisema Kamanda Mkumbo.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika

MAAMUZI YA RUFAA YA KESI YA LEMA KUJULIKANA JANUARI 4, 2017





Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016

Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maauzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa wamshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa lema masharti ya dhamana

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 disemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwaajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017

Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?

Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja  

"Unajua leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema Kibatala.

Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama.
Reviewed by RICH VOICE on Desemba 29, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...