Thursday, December 1, 2016
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema kuwa wanafunzi 526,653 kati ya 555,291 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu wamechaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwakani katika shule za sekondari za Serikali.
Kwa
mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ni sawa na asilimia 94.85
ya wanafunzi wote waliofaulu.
Akizungumza
na Waandishi wa habari tarehe 28 Novemba 2016 mjini Dodoma Waziri
Simbachawene ameeleza kuwa wanafunzi 28,638 wakiwemo wavulana 12,937 na
wasichana 15,701 hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi.
Aidha
Waziri Simbachawene aliitaja mikoa ambayo wanafunzi wake walifaulu
lakini hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza kuwa ni pamoja na Dar Es
Salaam (18,820), Arusha (4,752), Songwe (1,465), Kigoma (1,208), Manyara
(1,141), Lindi (608), Mbeya (406) na Katavi (238).
Kuhusu
wanafunzi waliochaguliwa Waziri Simbachawene amesema kuwa, wasichana ni
268,052 sawa na asilimia 94.5 na wavulana ni 258,601 sawa na asilimila
95.2.
Aidha,
Waziri wa Nchi amesema kuwa wanafunzi wote wenye ulemavu waliofaulu
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2017.
Kwa
mujibu wa Waziri Simbachawene mchanganuo wa wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali umegawanyika katika
makundi manne ambapo kundi la kwanza limehusisha wanafunzi 900 wakiwemo
Wavulana 480 na Wasichana 420 ambao wamepelekwa katika shule za Bweni
kwa wenye ufaulu mzuri zaidi.
Ameongeza
kuwa kundi la pili limehusisha wanafunzi 1005 ikiwa ni Wavulana 915 na
Wasichana 90 ambao wamepelekwa katika shule za Bweni mahsusi kusomea
Ufundi.
Pia
amesema kuwa kundi la tatu limewahusisha Wanafunzi 780 wakijumuishwa
Wavulana 430 na Wasichana 350 ambao wamechaguliwa kujiunga na Shule za
Bweni Kawaida na kundi la nne limewahusisha wanafunzi 723 wakiwemo
wavulana 405 na wasichana 318 wa shule za bweni kwa ajili ya wanafunzi
walio na Ulemavu.
Kulingana
na takwimu hizo, Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya wanafunzi
3,407 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni kidato cha kwanza ambapo
wavulana ni 2,230 sawa na asilimia 65.4 na wasichana 1,178 sawa na
asilimia 34.6, pia watahiniwa wapatao 6,260 sawa na asilimia 0.78 ya
waliosajiliwa hawakufanya mtihani.
Aidha
Waziri Simbachawene amesema kuwa wanafunzi 523,245 wakiwemo wavulana
256,371 na wasichana 266,874 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
katika shule za kutwa.
Wakati
huo huo Mhe. Simbachawene amesema hatasita kuzichukulia hatua, shule
zilizohusika na udanganyifu wa mitihani kwani wanarudisha nyuma
maendeleo ya taaluma nchini yanayofanywa na Serikali.
“Serikali
imeanza kuwachukulia hatua kwa mujibu wa taratibu wale wote waliohusika
na udanganyifu huu� hatua hizo ni pamoja na kuwavua madaraka waliokuwa
Waratibu Elimu Kata na Walimu Wakuu, kuwashtaki mahakamani na kupeleka
mashauri yao Tume ya utumishi ya Walimu (TSC),” amesema Mheshimiwa
Waziri.
Pia
ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa kubainisha sababu za wanafunzi
walioingia darasa la kwanza kutomaliza masomo yao kama ilivyotarajiwa.
“Naagiza
Wakuu wa Mikoa kubainisha sababu za wanafunzi hao kutomaliza na hatua
stahiki za kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote
wanaoandikishwa darasa la kwanza wanamaliza mzunguko wa masomo kwa
mujibu wa Sera ya Elimu,” amesisitiza Mhe. Simbachawene na kutaka Wakuu
wa mikoa kuchukua hatua stahiki zilizoelekezwa.
Thursday, December 1, 2016
Warioba: Maadili yameporomoka kwa viongozi na jamii
Jaji
Mstaafu, Joseph Sinde Warioba amevishauri vyombo vinavyo simamia
maadili kubadilika kiutendaji na kuachana na masuala ya kisiasa na
amependekeza kuwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU),
na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali kupewa nguvu ili zifanye kazi zake
kiurahisi.
Aliyasema
hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akichangia kwenye mdahalo wa wadau
ulioandaliwa na TAKUKURU kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za
binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.
Warioba alisema ni jambo lisilofichika kuporomoka kwa maadili si kwa jamii pekee, bali hata kwa baadhi ya viongozi.
“Lazima kuwe na misingi ya uongozi,maadili yameporomoka sana na ni ngumu kuyarudisha”alisema Warioba.
Aidha, Warioba alisema maadili hayajengwi na sheria wala hayasimamiwi na taasisi bali yanajengwa na kusimamiwa na jamii.
Thursday, December 1, 2016
Wadaiwa Sugu NHC Washitakiwa kwa Rais Magufuli
Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), limewasilisha ripoti ya wadaiwa sugu wa
shirika hilo, zikiwamo wizara, taasisi za Serikali na watu binafsi kwa
Rais Dk. John Magufuli, huku wizara mbili zikiwa na deni kubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mikoa na
Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema uamuzi huo umekuja baada ya
Rais Magufuli kuwataka kukusanya madeni hayo na kuwasilisha taarifa hiyo
ofisini kwake ili aweze kuipitia.
Mndolwa
alisema NHC ilitoa notisi ya siku 90 ambayo ilianza Septemba, mwaka
huu, huku wadaiwa hao wakitakiwa kulipa madeni ndani ya muda
uliopangwa.
Alisema
kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto na
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bado zinadaiwa kiasi
kikubwa cha fedha, licha ya kuwapo kwa mazungumzo ya kulipa madeni yao.
“Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto inadaiwa Sh
bilioni 1.4, huku wakilipa Sh milioni 300, wakati Wizara ya Habari,
inadaiwa Sh bilioni 1.14, lakini imelipa Sh milioni 700,” alisema Mndolwa.
Mndolwa
alisema shirika hilo hadi sasa limekusanya Sh bilioni 5.9 kati ya Sh
bilioni 9.3 ambalo ni deni la Serikali kupitia wizara na taasisi
mbalimbali, huku Sh bilioni 2.5 zikikusanywa kutoka kwa wadaiwa binafsi
ambao awali walikuwa wanadaiwa Sh bilioni 4.
Alisema
lengo la shirika hilo ni kuhakikisha madeni yanalipwa ili fedha hizo
ziweze kutumika kwenye shughuli nyingine za maendeleo, ikiwamo ujenzi wa
nyumba za kisasa 300 mkoani Dodoma.
Alizitaja
wizara zinazodaiwa ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha na
Uchumi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi na iliyokuwa Wizara ya Ujenzi.
Wadaiwa wengine ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Thursday, December 1, 2016
Wafanyabiashara Wawili wa Madini Wafikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Kulawiti na Kubaka Watoto
Wafanyabiashara wawili mashuhuri wa madini katika miji ya Mererani na jiji la Arusha jana walifikishwa mahakamani mjini Moshi kwa wakikabiliwa na makosa ya ulawiti na ubakaji watoto.
Mmoja wao, Welaufoo Munisi (38) anashtakiwa kwa kosa la
kumlawiti mtoto wa kiume wa mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), mwenye umri wa miaka 16.
Mtoto anayedaiwa kufanyiwa
kitendo hicho ni mwanafunzi wa shule moja ya sekondari wilayani Hai
mkoani Kilimanjaro, baba yake ni mchungaji katika usharika ambao
tunauhifadhi kwa sababu za kimaadili.
Akimsomea mashtaka yake mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga, Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Tamari Mndeme alidai kuwa Munisi alitenda kosa hilo
Novemba 21, 2016.
Wakili huyo alidai kuwa siku hiyo katika nyumba za
wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),
mshtakiwa alimlawiti kijana huyo mwenye umri wa miaka 16.
Kabla ya kufikishwa kortini jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Koka Moita alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya kumnyeshwa kijana huyo dawa za kulevya.
Kabla ya kufikishwa kortini jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Koka Moita alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya kumnyeshwa kijana huyo dawa za kulevya.
Hata hivyo, Munisi alikana mashtaka hayo na
kesi hiyo imepangwa kutajwa Desemba 14 mwaka huu baada ya wakili Mndeme
kuiambia Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo ulikuwa haujakamilika.
Dhamana yake ilikuwa wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na hadi saa 8:00 mchana alikuwa hajatimiza masharti hayo.
Dhamana yake ilikuwa wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na hadi saa 8:00 mchana alikuwa hajatimiza masharti hayo.
Wakati Munisi
akikabiliwa na shtaka hilo, mfanyabiashara mwingine wa Mererani,
Benedict Kimario (42) jana alipandishwa kizimbani mjini Moshi,
akikabiliwa na mashtaka ya kumlawiti na kumbaka mtoto wa miaka minane.
Wakili Mndeme alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Mei 10 mwaka huu katika Kijiji cha Mrau, Wilaya ya Rombo, Kilimanjaro.
Mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Joseph Peter, alikana tuhuma hizo na kesi hiyo imepangwa kutajwa kesho ili kuangalia kama ametimiza masharti ya dhamana au la baada ya jana kukwama.
Wakili Mndeme alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Mei 10 mwaka huu katika Kijiji cha Mrau, Wilaya ya Rombo, Kilimanjaro.
Mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Joseph Peter, alikana tuhuma hizo na kesi hiyo imepangwa kutajwa kesho ili kuangalia kama ametimiza masharti ya dhamana au la baada ya jana kukwama.
Alikwama baada ya Hakimu Mwilapo kumtaka kuwa na wadhamini
wawili ambao kila mmoja angesaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni, lakini
wakajitokeza wadhamini ambao si wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Wadhamini hao walikuwa na barua kutoka Mererani wilayani Simanjiro Mkoa
wa Manyara, ambazo kiutaratibu zilipaswa kwanza kuidhinishwa na Hakimu
wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro.
Thursday, December 1, 2016
Mganga wa Kienyeji Auawa Akitaka Kumbaka Mgonjwa
Mganga
wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55), mkazi wa
kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani Shinyanga ameuawa
kwa kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.
Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) alikwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio
hilo ni la Novemba 29 mwaka huu, akisema lilitokea majira ya saa tano
asubuhi.
Alisema
Kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa hospitali baada ya
kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika jicho la kulia na kupigwa
kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukulia sheria mkononi.
“Watu
hao walijichukulia sheria mkononi baada ya mganga huyo kujaribu kumbaka
mwanamke (jina linahifadhiwa), mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya
ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze kupata
mtoto”, alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda
Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na
uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya
kumlewesha kwa dawa za kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga kelele na
ndipo wananchi walipomvamia mganga huyo.
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 01, 2016
Rating:
Hakuna maoni