TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO

Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM

 

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemruhusu kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuendelea kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumkuta hana hatia kufuatia tuhuma za kumshambulia refa.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti, Tarimba Abbas jana mjini Dar es Salaam na uamuzi huo unamnufaisha pia kiungo mpya wa Singida United, Deus Kaseke. 
Kwa pamoja, wakiwa wachezaji wa Yanga, Chirwa, Kaseke na winga mpya wa Difaa Hassan El- Jadida walidaiwa kumsukuma na kumwangusha refa Ludovic Charles katika mechi namba 236 ya Ligi Kuu iliyokutanisha timu hiyo na wenyeji, Mbao FC walioibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


Hata hivyo, baada ya kikao cha jana, wote Kaseke na Chirwa wamekutwa hawana hatia, huku Msuva pekee akitiwa hatiani na kupewa onyo kali.
Baada ya mchezo huo, Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi ilipitia matukio mbalimbali na kufikia uamuzi wa kuwasimamisha wasubiri suala lao kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Wachezaji hao walidaiwa kufanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ulizingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
Lakini refa, Ludovic Charles naye alipewa onyo kali kwa kutoumudu mchezo kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi. 




Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Peter Hella amesema kwamba wachezaji wote wapo huru kuendelea na Ligi Kuu baada ya onyo hilo, lakini wanapaswa kujirekebisha
TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO Reviewed by RICH VOICE on Septemba 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...