Picture of landslides at Punggye-riMajaribio ya bomu la nyuklia ambayo yalifanywa na Korea Kaskazini Jumapili yalisababisha maporomoko kadha ya ardhi, kwa mujibu wa picha za setilaiti ambazo zinaaminika kuwa za kwanza kabisa za eneo ambalo majaribio hayo yalifanyika.
Majaribio hayo ya bomu yalifanyika chini ya ardhi katika eneo la kufanyia majaribio silaha linalotumiwa na Korea Kaskazini la Punggye-ri ambalo lina milima mingi.
Kundi la uchunguzi kwa jina 38 North limechapisha picha ambazo zinaonekana kuonyesha "maporomoko kadha katika eneo kubwa" kuliko yaliyowahi kushuhudiwa awali.
Mlipuko wa bomu hilo ulisababisha tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 kwenye vipimo vya Richter.Tetemeko hilo lilisikika hadi China na katika baadhi ya maeneo ya Urusi.
Korea Kaskazini imefanya majaribio sita ya silaha za nyuklia kufikia sasa, yote katika eneo la Punggye-ri, ambalo lina njia za chini kwa chini ambazo zimechimbwa ndani kwenye milima.
Picha za karibuni zaidi za 38 North zilipigwa siku moja baada ya majaribio hayo kufanywa na zinaonesha maporomoko pamoja na maeneo yenye vifusi na matope.
Kuna pia maeneo ya ardhi ambayo inaonekana yalirushwa juu angani lakini yakarejea tena chini bila kuhama.Picture showing the Punggye-ri test sitePicture of landslides at Punggye-riUharibifu ulitokea karibu na Mlima Mantap, mlima mrefu zaidi eneo hilo la majaribio.
Waliochunguza eneo hilo wamesema kulikuwa na "maporomoko makubwa na yaliyoenea sana kuliko tuliyoshuhudia wakati wa majaribio matano ya awali ambayo Korea Kaskazini iliyafanya."
Lakini waliongeza kwamba ingawa tetemeko hilo lilisababisha tetemeko lenye nguvu sana, hakuna dalili kwamba njia ya chini kwa chini ambayo ilitumiwa kulipua bomu hilo iliporomoka.
Baadhi ya wataalamu wanaamini kwamba mlipuko wa bomu ulisababisha shimo ambalo lilitumiwa kulipua bomu hilo Punggye-ri liliporomoka, sana kutokana na hali kwamba kulitokea tetemeko la pili mwendo wa dakika nane baada ya tetemeko la kwanza.Picture showing the Punggye-ri test sitePicture of landslides at Punggye-riBomu la Jumapili linakadiriwa kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 50 na 120.
Bomu la nguvu ya kilotani 50 linakadiriwa kuwa na nguvu mara tatu ukilinganisha na bomu la nyuklia lililoangushwa na Marekani katika mji wa Hiroshima mwaka 1945.
Majaribio kufanywa eneo moja Korea Kaskazini yameibua wasiwasi kuhusu iwapo eneo hilo linaweza kuwa hatari, ingawa wataalamu wamegawanyika.
Mapema wiki hii, wanasayansi wa China walieleza wasiwasi kwamba mlima huo unaweza kuporomoka na kutoa miali nururishi iwapo majaribio yataendelea kufanywa eneo hilo, gazeti la South China Morning Post liliripoti.
Lakini shirika la 38 North awali lilikuwa limesema hakuna uwezekano wa majaribio hayo kusababisha mlipuko wa volkano katika milima hiyo.
Marekani inaweza kuishambulia Korea Kaskazini?
Mzozo huo umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, lakini hali kwamba Korea Kaskazini inakaribia kuwa na/ au tayari ina uwezo wa kuunda kichwa kidogo cha nyuklia kinachoweza kuwekwa kwenye makombora, na kwamba ina makombora yanayoweza kufikia Marekani bara, yanabadilisha mambo sana.
Miezi kadha iliyopita, kumekuwa na hatua za 'uchokozi' mara kadha za Korea Kaskazini pamoja na majibizano kati yake na Marekani ambazo zimezidisha mzozo huo.
Korea Kaskazini ilitishia kurusha mabomu karibu na kisiwa cha Guam ambacho kinamilikiwa na Marekani katika Bahari ya Pacific.
Majuzinchi hiyo imerusha kombora kupitia anga ya Japan.
Lakini huku majibizano yakiendelea, bado ni vigumu kubashiri ni nini kitafuata.
Reviewed by RICH VOICE on Septemba 07, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...