Utafiti: Mbwa mwitu hufanya uamuzi kwa kupiga chafya

An African wild dogMbwa mwitu hufanya maamuzi yao kwa kupiga kura kupitia kupiga chafya kwa mujibu wa utafiti mpya.
Utafiti huo wa pamoja uliofanywa na wasomi kutoka Swansea, Australia na Marekani ulifuatilia mbwa mwitu walio kwenye hatari ya kuangamia nchini Botswana.
Waligundua kuwa mbwa walitumia chafya kuamua wakati wanaelekea kuwinda baada ya kufanya mikutano inayofahamika kuwa mikutano wa kijamii.
African wild dogs
Awali ilikuwa ikifikiriwa kuwa mbwa hao ambayo ni familia ya wanyama walio kwenye hatari zaidi ya kuangamia duniani, walikuwa wakipiga chafya ya kawaida.
Lakini wakati watafiti walirekodi mikutano 68 ya mwa mwitu waligundua kuwa wakati walipiga chafya zaidi walikuwa wakiondoka na kuanza wa kuwinda.
Dr King anasema kuwa chafya hiyo ni lazima ifike kiwango fulani kabla ya wao kuamua kufanya kitu.
Pia uutafiti huo uligundua baadhi ya chafya huwa na uzito kuliko zingine.
Utafiti: Mbwa mwitu hufanya uamuzi kwa kupiga chafya Utafiti: Mbwa mwitu hufanya uamuzi kwa kupiga chafya Reviewed by RICH VOICE on Septemba 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...