Tundu Lissu Apelekwa Nairobi kwa Matibabu


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma usiku wa kuamkia leo kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Lissu  alijeruhiwa jana akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulika.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amesema, katika safari hiyo Lissu ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Selasini amesema kuwa Lissu anapelekwa katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi.

Ndege hiyo iliyombeba ya 5H-ETG imeondoka katika Uwanja wa Dodoma saa sita na robo usiku.
Tundu Lissu Apelekwa Nairobi kwa Matibabu Tundu Lissu Apelekwa Nairobi kwa Matibabu Reviewed by RICH VOICE on Septemba 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...