Waziri Makamba amlilia Muhingo Rweyemamu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amemtaja mwandishi wa habari mkongwe, Muhingo Rweyemamu kuwa alikuwa mwalimu na mshauri wake wa karibu.
Mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha wageni waliohudhuria msiba wa mwandishi huyo nyumbani kwake Mbezi Luis, January alisema alifanya kazi na Muhingo kwa karibu wakati wa uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete. 
 
Muhingo amewahi kuwa mkuu wa wilaya tatu kwa vipindi tofauti; Handeni, Makete na Morogoro. 
 
“Namkumbuka kwa mambo mengi alikuwa ni mtu anayepen-da kuelimisha, alikuwa akinishauri hata kusoma vitabu vya kunisaidia kunipa mwongozo,” alisema. 
 
Alisisitiza kuwa anaamini wana tasnia ya habari watamuenzi
kwa kuendelea kuandika habari zenye weledi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla. 
 
Kaka wa marehemu, Elisa Muhingo alisema kifo cha mdogo
wake ni pigo kubwa kwa familia kwa sababu alikuwa tegemeo lao. 
“Lakini kwa jinsi alivyougua, ameteseka kwa maumivu makali, kifo chake tusingeweza kukipinga. Tunamshukuru Mun-gu amempumzisha, tunatafakari na kujipanga kuishi bila yeye,” alisema.
 Aliyekuwa rafiki wa karibu wa marehemu ambaye pia ni mwandishi mkongwe, Absalom Kibanda alisema leo wanatarajia kuuhamisha mwili kutoka chumba cha maiti cha Hospitali ya Aga Khan alikofia na kuupeleka nyumbani kwake kwa maandal-izi ya maziko. 
“Baada ya kikao cha mashauriano, imekubaliwa kwamba Rweyemamu atazikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne, Septemba 5, 2017,” alisema. 
 
Alisema shughuli za mazishi zitatanguliwa na ibada ya kumuaga ambayo itafanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tan-zania (KKKT) Mbezi, Kibanda cha Mkaa.
Waziri Makamba amlilia Muhingo Rweyemamu Waziri Makamba amlilia Muhingo Rweyemamu Reviewed by RICH VOICE on Septemba 03, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...