Uhuru Kenyatta Ampa ONYO Raila Odinga....Amtakaa Asahau Habari za Kubadili Tume


Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefunguka na kutoa onyo kwa mpinzani wake Raila Odinga kuwa asahu kuhusu tume mpya ya uchaguzi lakini pia amemtaka Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga kutoingilia kwani wao wameheshimu maamuzi ya mahakama

Uhuru Kenyatta amesema chama chake cha Jubilee kipo tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na sasa wanasubiri Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC iweze kutangaza siku ya uchaguzi na wanaiomba itangaze siku hiyo haraka.

Aidha Uhuru Kenyatta amesema kuwa wapinzani hao hawana haja ya uchaguzi bali ni watu ambao wanataka serikali ya mseto kitu ambacho yeye hawezi kukiruhusu hata kidogo

Mahakama ya juu nchini Kenya Septemba 1, 2017 ilifuta matokeo ya Urais nchini Kenya na kuamuru kuwa uchaguzi mpya ufanyike katika nafasi ya Urais kutokana na mahakama hiyo kubaini baadhi ya mapungufu wakati wa utoaji wa matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017.
Uhuru Kenyatta Ampa ONYO Raila Odinga....Amtakaa Asahau Habari za Kubadili Tume Uhuru Kenyatta Ampa ONYO Raila Odinga....Amtakaa Asahau Habari za Kubadili Tume Reviewed by RICH VOICE on Septemba 03, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...