Waandamanaji wakesha kupinga utawala wa Gnassingbe Togo

Waandamanaji washinda usiku kucha mitaani kupinga utawala wa Gnassingbe Togo
Vikosi vya usalama nchini Togo vimerusha gesi ya kutoa machozi mapema leo, kutawanya mamia ya waandamaji wanaoipinga seikali walioshinda usiku kucha mjini Lome.
Vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha picha za waandamanaji wakilala barabarani usiku.
Polisi walichukua hatua ya maandamano ya nchi nzima ya saa 48 ya kutaka kumalizika kwa utawala wa miaka 50 wa familia ya Gnassingbe

Hakuna taaraifa yoyote ya majeruhi au maafa.
Maandamano yaliendelea licha ya Rais Faure Gnassingbe, kuahidi kurejesha sheria ya kutaka rais ahudumu kwa mihula miwili pekee nchini humo.
Mamlaka zimeamrisha kuzimwa kwa mitandao kwa muda wa siku mbili kama njia ya kukabiliana na maandamano hayo.
Waandamanaji wakesha kupinga utawala wa Gnassingbe Togo Waandamanaji wakesha kupinga utawala wa Gnassingbe Togo Reviewed by RICH VOICE on Septemba 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...