Halima Mdee Agoma Kujisalimisha kwa DCI


Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaa Halima James Mdee amesema hajaenda kuripoti kwa DCI kama ilivyotakiwa kwa sababu yeye hajaitwa rasmi.

Mdee amesema DCI ametoa tangazo la ujumla, lakini yeye binafsi hajapewa wito wowote, hivyo hawezi kwenda kutokana na taarifa hiyo.

"Mimi nimesikia tangazo la ujumla, wakiniita in personel Halima njoo nitaenda na hakuna popote kwenye kauli yao iliposema Halima Mdee njoo, lakini siwezi kwenda kwa 'general statement', amesema Halima Mdee

Juzi Jeshi la Polisi liliwataka watu wote waliopost kwenye mitandao ya kijamii kuhusu askari wao aliye nchini Nairobi wakimuhusisha na kumfuatilia  Tundu Lissu nchini Kenya kwenye matibabu na kutakiwa kuripoti wenyewe kwa DCI, kabla ya kitengo cha sheria za makosa ya mtandaoni hakijawachukulia hatua zaidi.
Halima Mdee Agoma Kujisalimisha kwa DCI Halima Mdee Agoma Kujisalimisha kwa DCI Reviewed by RICH VOICE on Septemba 14, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...