LIVERPOOL YALIPA KISASI CHA KUFUNGWA NA LEICESTER CITY

Philippe Coutinho amefunga goli zuri la msimu huku Jamie Vardy akishuhudia penati yake ikiokolewa katika mchezo ambao Liverpool imeibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Leicester City.

Leicester City ambayo iliitungua Liverpool kwa magoli 2-0 katika kombe la Carabao siku ya jumanne, lakini safari hii Liverpool iliamua kulipa kisasi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Liverpool ilipata goli lake la kwanza baada ya Coutinho kumtengenezea pande la mpira wa kichwa Mohamed Salah, Coutinho akaongeza la pili, kisha Shinji Okazaki akachomoa goli moja.

Jordan Henderson akaiongezea Liverpool goli la tatu katika shambulizi la kushtukiza hata hivyo Leicester City haikukata tamaa na kufanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa Jamie Vardy.
                        Mohamed Salah akiifungia Liverpool goli la kwanza katika mchezo huo
                      Mbrazili Philippe Coutinho akifunga goli zuri kwa mpira wa adhabu 
                         Mjapani Shinji Okazaki akiifungia Leicester City goli lao la kwanza 
LIVERPOOL YALIPA KISASI CHA KUFUNGWA NA LEICESTER CITY LIVERPOOL YALIPA KISASI CHA KUFUNGWA NA LEICESTER CITY Reviewed by RICH VOICE on Septemba 24, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...