Aslay, Nandy kuburuzwa mahakamani
Wimbo
wa 'Subalkheri Mpenzi', ulioimbwa na wasanii wa kizazi kipya Aslay
Ishack na Nandy, umezidi kuzua utata baada ya mmiliki wa wimbo huo,
Kikundi cha Tarab Asilia visiwani Zanzibar (Culture Music Club),
.........Kudai kuwa watawaburuza mahakamani kwa kuwa Sh. 800,000
zilizotolewa kama fidia hawazitambui.
Katibu
Mtendaji wa kikundi hicho, Taimur Rukuni Twaha, jana alisema wasanii
hao kabla ya kuimba tena upya wimbo huo walipaswa kuonana na uongozi huo
ili kukubaliana jambo ambalo hawakufanya hivyo.
Kwa
mujibu wa katibu huyo, wasanii wa kikundi hicho waliopewa mgawo huo wa
fedha ni waimbaji wawili (majina tunayo) ambao mmoja alipewa Sh. 500,000
na mwingine Sh. 300,000.
“Walichokifanya
Aslay na Nandy kwenda kwa waimbaji wetu na kuwapa kiwango hicho cha
fedha kwetu tunaona hakikubaliki na wametoa kama zawadi tu kwa sababu
thamani ya wimbo wetu haulingani na kiwango hicho,” alisema Twaha.
Alisema
kwa mujibu wa katiba ya kikundi hicho, ibara ya sita inaeleza nyimbo
zote zilizoimbwa na kikundi ni mali ya kikundi na kwamba muimbaji,
mtunzi na muweka sauti watakuwa na haki zao kupitia kikundi hicho.
Alisema
kimsingi msimamo wao utabaki pale pale wa kuwafikisha mahakamani
wasanii hao endapo watashindwa kutimiza masharti waliopewa na uongozi wa
kikundi hicho.
Aidha,
alisema masharti hayo hayatomhusu Aslay na Nandy peke yao bali na
mwanamuziki Hussein Mmanga Faki (maarufu HamaQ) na mwenzake Mosi
Suleiman kwa kuimba wimbo wa 'Mke wa Awali ni Wewe Aziza' ambao pia ni
mali ya kikundi hicho.
“Tunafahamu
kuwa nyimbo zetu wameziimba tena kwa lengo la kibiashara na wamekuwa
wakipata fedha kupitia nyimbo hizo,”alisisitiza katibu huyo.
Alisema
tayari wameshawaandaa mawakili wao, ambao wataisimamia kesi hiyo
mahakamani iwapo wasanii hao watashindwa kutimiza masharti waliyopewa.
Akizungumzia
suala hilo, Meneja wa Coconut FM, ambaye ni mwakilishi wa Aslay na
Nandy, alisema kuwa wasanii hao watafikishwa katika uongozi wa Kikundi
cha Taarab Asilia (Culture) ili kupata suluhu.
Alisema
wao hawana makosa kutumia wimbo huo, kwani kabla ya kurudia kuuimba
walishakutana na mtunzi wa wimbo huo Bakari Abeid ambaye sasa ni
marehemu na kumalizana naye wakati wa uhai wake.
Aslay, Nandy kuburuzwa mahakamani
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 12, 2018
Rating:
Hakuna maoni