Jeraha la kichwa lamlazimu kustaafu akiwa na umri wa miaka 6

Kiungo wa kati wa klabu ya Hull City
nchini Uingereza Ryan Mason amelazimika kustaafu akiwa na umri wa miaka
26 kufuatia jeraha la fuvu la kichwa alilopata katika mechi dhidi ya
Chelsea 2017.
Mason ambaye aliichezea Uingereza mara moja 2015
alilazimika kufanyiwa upasuaji baada ya kichwa chake kugongana na kile
cha beki wa Chelsea Gary Cahill.Uamuzi wake wa kustaafu unafuatia ushauri wa madaktari wa upasuaji wa neva.

Baada ya dakika nane ya matibabu uwanjani wakati wa mechi ya ligi ya Uingereza iliopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge mwezi Januari 2016, Mason aliwekewa hewa alipobebwa katika machela na kutolewa uwanjani.

Mason alianza mazoezi na klabu hiyo tena mwezi Mei mwaka uliopita lakini hakuna tarehe ya yeye kurudi iliotolewa na baadaye mkufunzi wa klabu hiyo Leonid Slutsky alisema mwezi Agosti mwaka uliopita swali sio kuhusu soka bali kuhusu maisha yake wakati mchezaji huyo alipokutana na mtaalam wa tatu.
Klabu ya hull City imewashukuru wale wote waliomsaidia kupona katika kipindi cha miezi 12 iliopita.
Jeraha la kichwa lamlazimu kustaafu akiwa na umri wa miaka 6
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 13, 2018
Rating:
Hakuna maoni