DALALI: YANGA WANA NJAA, WANASHINDIA MIHOGO
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali amewatupia
dongo wapinzani wao wa jadi, Yanga kwa kusema kuwa ni kama pilipili
hoho, kubwa lakini haiwashi.
Dalali alisema hayo mara baada ya kushuhudia Simba ikipata ushindi wa
mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru, wikiendi
iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Amesema kuwa wao hawana hofu juu ya Yanga kwa kuwa kwao si lolote na wao wapo tayari kuwafumua vibaya pindi watakapokutana.
Akiinadi timu yake zaidi, Dalali alisema: “Yanga ni kama nyanya ya Mchina, hawana lolote, nyanya ya Mchina inalika bwana.
“Simba usiifananishe na Yanga, kwanza Yanga wana njaa wanashindia
mihogo, sisi tunaangalia mechi iliyo mbele yetu, wao Yanga wapo mbali,
hatuwajali.
“Mimi nawajua Yanga vizuri, wao ni kama chapati ya maji isiyokuwa na vitunguu.”
Ikumbukwe kuwa Simba ipo katika mchakato wa kubadili aina ya mfumo wa
uendeshaji wa klabu hiyo na mwanachama Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ ndiye
ambaye aliyeshinda tenda ya kununua hisa kwa asilimia 41 mara baada ya
mfumo huo wa mabadiliko kupita.
DALALI: YANGA WANA NJAA, WANASHINDIA MIHOGO
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni