Watano Wapoteza Maisha, Sita Wajeruhiwa Katika Ajali Kabuku Mkoani Tanga
Watu
watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya,
baada ya basi kubwa kugongana na hiace katika eneo la Kabuku wilayani
Handeni mkoa wa Tanga.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Leonce Rwegasira alisema ajali hiyo imetokea saa 5:30 asubuhi katika
eneo hilo la Kabuku.
Alitaja
mabasi hayo kuwa ni basi la kampuni ya AK Safari lililokuwa likitoka
Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi
wa Chamanzi Dar es salaam lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo
limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba
T591 AKE.
Alisema
waliofariki ambao ni pamoja na Dereva wa hiace aliyefahamika kwa jina
moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao
zimehifadhiwa Kwenye hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.
ACP
Rwegasira alisema majeruhi ambao hawakuchukua majina yao kutokana na
kuwasaidia kuwafikisha katika kituo cha afya Kabuku kwa ajili ya
kuendelea na matibabu.
Kaimu
Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa chanzo cha ajali ni kutozingatiwa
kwa sheria na alama za usalama barabarani kwa madereva hao.
Kamanda
huyo wa Polisi alitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia
sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Watano Wapoteza Maisha, Sita Wajeruhiwa Katika Ajali Kabuku Mkoani Tanga
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 12, 2018
Rating:
Hakuna maoni