Wapinzani waendelea na mgomo Ethiopia
Waandamanaji wanaoipinga serikali
katika mkoa ulio mkubwa nchini Ethiopia wa Oromia wanafanya mgomo wa
siku tatu kushinikiza madai yao ya kuachiwa kwa wanasiasa wote na
Waandsihi wanaoshikiliwa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili
kilichotokea machafuko.
Katika siku ya kwanza ya mgomo huo, jana Jumatatu, barabara nyingi ziliwekewa vizuizi na biashara kufungwa.
Hata
hivyo serikali ya Ethiopia imesema itamwachilia huru kiongozi mgonjwa
wa upinzani, licha ya maandamano kuendelea katika baadhi ya maeneo ya
nchi.
Mwendesha mashtaka mkuu nchini Ethiopia ametangaza kuwa
serikali itamuondolea mashtaka ya kuchochea ghasia Katibu Mkuu wa chama
cha Oromo Federalist Congress.
Kiongozi huyo wa upinzani
alikamatwa Desemba, 2015 kwa mashtaka ya awali ya kuwa na mahusiano na
vikundi ya kigaidi. Lakini hata hivyo mashtaka hayo baadaye yalishushwa
na kubadilika kuwa uchochezi wa ghasia.
Ataachiwa huru pamoja na wenziye sita aliokamatwa nao.
Serikali
pia imewaachia huru na kuwaondolea mashtaka maelfu ya watu, ikiwa
sehemu ya mageuzi iliyoahidi kumaliza maandamano ya upinzani yaliyodumu
kwa zaidi ya miaka mitatu nchini humo.
Mwaka 2016 hali ya hatari ilitangazwa na maelfu ya waandamanaji walikamatwa.
Wapinzani waendelea na mgomo Ethiopia
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 13, 2018
Rating:
Hakuna maoni