Waziri Mkuu apinga madai ya mbunge wa Chadema Kuhusu wagombea Chadema kutotangazwa washindi
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema hajui kama kuna kata ambayo mgombea wa
Chadema ilishinda lakini hakutangazwa, badala yake akatangazwa mshindi
kutoka chama kingine cha siasa.
Ametoa
kauli hiyo leo Februari 8, 2018 bungeni Dodoma katika kipindi cha
maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, wakati akijibu swali la mbunge
wa viti maalumu (Chadema), Devotha Minja.
Katika
swali lake, Minja ametaka kujua Serikali inasema nini kuhusu
ukandamizwaji wa haki unaofanywa na wasimamizi wa uchaguzi ambao
wanawatangaza wagombea ambao hawakushinda na kuwaacha walioshinda.
Mbunge huyo ametoa mfano wa Kata ya Sofi mkoani Morogoro ambako mgombea wa Chadema alipata kura 1908, wa CCM kura 1878.
Pia,
ametaja Kata ya Siyui mkoani Singida, mgombea wa Chadema alipata kura
1,358 huku wa CCM akipata kura 1304, lakini waliotangazwa wote walikuwa
wa chama tawala.
Katika majibu yake, Waziri Majaliwa amesema hatarajii kuwa tume inaweza kuwatangaza walioshindwa na kuwaacha washindi.
"Lakini
sheria zinaipa nafasi Tume ya Uchaguzi (NEC) kukutana na vyama
vinavyogombea ili kuwapo na nafasi ya kujadiliana kwenye upungufu,"
amesema Majaliwa.
Hata
hivyo, amewataka wanaohisi kuonewa waende mahakamani kudai ushindi wao
katika kipindi kisichozidi miezi mitatu ili sheria itazamwe kwenye
ushindi huo.
Waziri Mkuu apinga madai ya mbunge wa Chadema Kuhusu wagombea Chadema kutotangazwa washindi
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 08, 2018
Rating:
Hakuna maoni