Wanaharakati waandamana Kenya kushinikiza kufunguliwa kwa vituo vya utangazaji
Maandamano makubwa yatarajiwa hii
leo Nairobi kuishinikiza serikali kuvifungua vyombo vitatu vya habari
nchini vilivyofungiwa kupeperusha matangazo kwa siku ya saba leo.
Maandamano
haya yanajiri wakati viongozi wa upinzani waliokamatwa kwa madai ya
kushiriki njama ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama
rais.
Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV,
Citizen na KTN kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja
matangazo licha ya onyo kutofanya hivo.
Na sasa makundi ya kutetea
haki za kibinadamu, waandishi habari na baadhi ya wananchi wanapanga
kufanya maadamano hii leo Nairobi kuishinikiza serikali kutii amri ya mahakama.
Waandalizi wa maandamano hayo wanaishtumu serikali wakidai imekiuka
haki za kibinadamu, kuendeleza mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari
kando na kupunguza uhuru wa demokrasia nchini kwa kutoheshimu katiba.
Kufutia kuapishwa kwa Odinga Jummanne iliyopita, vyomba vya
usalama vime wakamata viongozi wa upinzani inaodai walishiriki katika
kumuapisha Odinga kuwa anachokitaja Rais wa watu.
Viongozi watatu wa muunganow a upinzani NASA, wabunge TJ Kajwang na Geroge Aladwa pamoja na wakili Miguna Miguna walikamatwa.
Katika mkutano wa hadhara jijini Nairobi siku ya Jumapili viongozi wa upinzani wameapa kufanya maandamano iwapo Miguna hataachiliwa huru
'Ikifikia kesho kama Miguna Miguna hajaachiliwa.. Wale watu wote tulikuwa Uhuru Park, tutajitokeza twende police station.. tuwe tayari kushikwa', amesema Godfrey Otsosi kiongozi wa chama cha ANC katika muungano wa upinzani Nasa Kenya.
Lakini kwa upande wake, serikali imeshikilia kuwa upinzani unakiuka sheria na hauheshimu uamuzi wa wanachi uliowaweka madarakani.
Makamu wa Rais,William Ruto amesisitiza kuwa hawatafanya mazungumzo na upinzani kuhusu kugawana mamlaka serikali.
Wanaharakati waandamana Kenya kushinikiza kufunguliwa kwa vituo vya utangazaji
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni