Diamond Platnumz, Hamisa warudi tena Mahakamani

Nyota wa muziki wa Bongo fleva na Rais wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao.

Diamond na Mobetto wamefika Mahakamani hapo, ikiwa ni wiki moja baada ya kufika na kusuluhishwa.

Hamisa Mobetto akizungumza nje ya Mahakama  amesema; “Maamuzi nimeridhika nayo na tumekubaliana kuhusu matunzo ya mtoto, Pande zote mbili tulikaa na kukubaliana, nashukuru kila mtu tumekubaliana na tumeridhika, hivyo yamekwisha.”

Naye Diamond Platnumz amesema mara ya mwisho ilikuwa ni usuluhishi haikuwa Kesi na leo tumeweka rekodi sawa ili kutunza kumbukumbu na kuweka vitu sawa ili yasije kuzushwa mengine ya uongo na kweli.

“Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani. Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz
Diamond Platnumz, Hamisa warudi tena Mahakamani Diamond Platnumz, Hamisa warudi tena Mahakamani Reviewed by RICH VOICE on Februari 13, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...