CHAN 2018: Morocco imefunga Nigeria 4-0 na kuibuka washindi
Michuano ya kombe la Afrika kwa
wachezaji wa Ligi za Ndani ( CHAN) imehitimishwa Jumapili kwa ushindi wa
wenyeji Morocco waliofanikiwa kulinyanyua taji la michuano hiyo
kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nigeria.
Mchezaji wa
Morocco Zakaria Hadraf alifanikiwa kupachika wavuni bao la kwanza muda
mfupi kabla ya kipindi cha mapumziko huku mchezaji wa Nigeria Peter
Eneji Moses akitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano
muda mfupi baad ya bao hilo.
Walid El Karti na Hadraf - katika bao lake la pili - waliipatia Morocco uongozi katika mechi hiyo kufikia dakika sitini.
Kampeni
hiyo ilikamilishwa kwa bao la Ayoub El Kaabi, aliyegonga chuma mara
mbili , na kufanikiwa kulifunga bao lake la tisa katika mashindano hayo
ya wachezaji wa nyumbani wa timu za Afrika.
Nafasi ya kwanza ya
Morocco ilikuja kunako dakika tatu za mechi wakati Walid El Karti
aliposukuma tobwe katika eneo la karibuna lango kuu.
Wenyeji hao walidhani wameshafunga bao lao la kwanza katika dakika ya
nne alipoisakata ngozi , kwa bahati mbaya naibu refa akanyanyua
bendera akidai kiki hiyo ilisukumwa vibaya kabla ya kumfikia
mshambuliaji huyo.
El Kaabi akasukuma hedi na kipa wa Nigeria Oladele Ajiboye ilibidi aokoe matobwe mawili kabla ya shinikizo la Morocco kujipa.
Kwa
ukubwa Nigeria ilitegemea pasi ndefu kwa mashambulio yao na Anas
Zniti wa Morocco hakuwana kibarua kikubwa kuokoa kabla ya muda
wamapumziko.
Dakika mbili baada ya kipindi cha mpumziko Peter
Eneji Moses alitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano
kwa mchezo m'baya dhidi ya Mohammed Nahiri.
Morocco ikaongeza bao
la pili kunako dakika sitina wakati kiki ya El Kaabi ilipogonga chuma
na kurudi nyuma kumwezesha El Haddad kusukuma kwa mara ya pili tobwe
ambalo lilimfanya Ajboye asue sue na kumpa nafasi El Karti kusukuma kwa
urahisi hedi ya nguvu ndani ya wavu.
Dakika tatu baadaye Hadraf alilifunga lake la pili baada ya krosi ya El Haddad kumuangukia .
El Kaabi hatimaye alifanikiwa kulisukuma lake kunako dakikda 73
wakati mpira ulipomuangukia mguuni na kumfanya amalize mashindano hayo
kama mfungaji bora akiwa amefanikiwa kuyafunga tisa kwa jumla.
Kwa kweli timu ya watu 10 ya Nigeria ilishindwa kuitishia Morocco kabisaa katika nusu ya pili.
Magoli
ya El Kaabi huedna yamechangia kummulika mbele ya macho ya koca wa timu
ya taifa ya Morocco Herve Renard aliyekuwa anatizama michuano huyo
pembeni akitazamia kukamilisha kikosi chake tayari kwa michuano ya
kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi.
Siku ya jumamosi Sudani ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Libya penati 4-2 baada ya sare ya bao 1-1.
Katika
hatua ya penalti , Sudan ilifanikiwa kufunga penati na kuambulia
medali ya shaba katika fainali za CHAN baada ya kuibuka tena nafasi
ya tatu walipokuwa waandaaji wa mashindano hayo mwaka 2011, huku Libya
wakiibuka mabingwa miaka mitatu baada ya hapo.
Mataifa 16
yalishiriki michuano hiyo ambayo yalipangwa katika makundi manne,
ambayo ni Kundi A-wenyeji morocco, Mauritania, Guinea na Sudani, Kundi
B-Namibia , Uganda, Zambia na Ivori Coast, Kundi C-Libya Nigeria, Rwanda
na Equtorial Guinea.
Kundi D -Lilikuwa na Timu za Congo ,Angola, Cameroon pamoja na Burkina Faso.
CHAN 2018: Morocco imefunga Nigeria 4-0 na kuibuka washindi
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni