WAWEKEZAJI CHANGAMKIENI FURSA MKOANI MANYARA.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akielezea
jambo mbele ya mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Manyara, Missaile Raymond Musa (katikati) mara baada ya kuwasilia katika
Ofisi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Mama
Fissoo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe
wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.
Kutoa kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye
Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage na Katibu Tawala
Msaidizi Serikali za Mitaa wa Mkoa Kennedy Kaganda.
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akizungumza jambo alipokutana na
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo
(kushoto) leo Ofisini kwake mjini Babati, Mkoani Manyara. KBF yupo
mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za
Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu.
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa akisoma kwa makini nakala za Sheria
ya Filamu na Kanuni zake mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) Ofisini
kwake leo mjini Babati. KBF yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ili
kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa na Wilaya kuhusu
Kanuni na Sheria ya Filamu.
Kutoka
Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa WA Mkoa wa Manyara
Kennedy Kaganda na Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye
Katibu wa Bodi ya Filamu Mkoa Bi. Frida Nkarage wakifuatilia mazungumzo
baina ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce
Fissoo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Mkoa, Missaile Raymond Musa (hawapo
pichani) walipokutana ofisi kwa RAS –Manyara, mjini Babati leo.Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Babati
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo akisaini
kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Katibu Tawala
wa Mkoa wa Manyara, mjini Babati Leo. Katibu huyo yupo mkoani Manyara
kwa ziara ya kikazi ili kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za
Mikoa na Wilaya kuhusu Kanuni na Sheria ya Filamu katika mkoa huo. Kulia
ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Missaile Raymond Musa.
Na: Frank Shija – MAELEZO, Babati,
Wawekezaji
wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika Mkoa wa
Manyara badala ya kukimbilia katika maeneo ambayo yamezoeleka na wadau
wengi wa maendeleo.
Rai
hiyo imetolewa leo Mjini Babati na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Manyara alipokuta na ujumbe kutoka Bodi ya Filamu Tanzania ukiongozwa na
Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bibi. Joyce Fissoo mape hii leo.
Kaimu
Katibu Tawala huyo ameema kuwa Mkoa wa Manyara unazo fursa nyingi za
uwekezaji hivyo ni vyema sasa wawekezaji wakatumia fursa hizo na kuja
kuwekeza katika Nyanja tofautitofauti za uwekezaji ikiwemo kilimo,
viwanda na ufugaji.
“
Mkoa wetu wa Manyara unazo fursa nyingi ambazo kama wawekezaji
wakijitokeza watanufaika nazo, hivyo ni wito wangu kwao kuwa waje mkoani
Manyara watumie fursa hizo, tunayo maeneo yakutosha kwa shughuli za
uwekezaji”, alisema Kaimu Katibu Tawala huyo.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania (KBF),
Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa maeneo
ambayo yamekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu nchini hasa
zinazohusisha wageni kutoka nje ya nchi.
Aliongeza
kuwa kitu kikubwa kinachoubeba mkoa huo ni mandhara na jiografia ya
ambayo imekuwa kivutio kikubwa katika uwekezaji hasa katika eneo la
utalii na filamu hapa nchini.
“
Ni jambo muhimu Mkoa wa Manyara mkajivunia kuwa na mandhari inayovutia
wawekezaji, katika tasnia ya filamu wageni wengi kutoka nchi mbalimbali
wamekuwa wanakuja na kuhitaji kutumia mandhari ya Wilaya ya Mbuli katika
uandaaji wa filamu zao hiyo ni moja ya fursa muhimu ambayo pia
itatumika kuutangaza zaidi mkoa wenu”, alisema Bibi. Fissoo.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania yupo mkoani Manyara kwa ziara ya
kikazi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi za Filamu za Mikoa
na Wilaya kuhusu majukumu ya Bodi hizo na zinazoongozwa na Makatibu
Tawala wa Mikoa na Wilaya.
WAWEKEZAJI CHANGAMKIENI FURSA MKOANI MANYARA.
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni