Makonda: Kuna gazeti moja kazi yake ni kunichonganisha
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuna gazeti moja nchini
limekuwa likiandika habari za kumchonganisha yeye na viongozi wengine
au taasisi nyingine za serikali, jambo ambalo amesema halikubaliki wala
hawezi kulifumbia macho.
Makonda
ameyasema hayo jana, Feb. 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa Jengo la
Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Amana, iliyopo Ilala jijini
Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kauli
hiyo ya Makonda imekuja kutokana na maamuzi yake ya kuvunja mabaraza
yote ya ardhi ya mkoa wa Dar, na kutaka kazi hizo zifanywe na makatibu
tarafa hadi pale ambapo utaratibu mwingine utawekwa, jambo ambalo baadhi
ya vyombo vya habari na wanaharakati walidai kuwa anaingilia kazi ya
mahakama.
“Kuna
gazeti moja linahangaika sana kuandika vitu vibaya kuhusu Mkoa wa Dar,
wanajifanya wanajua sana sheria, wanachonganisha, na leo nimeona
wameandika tena, wasitupotezee muda.
“Aliyeanza
kugombanisha duniani ni shetani, lakini ilifika wakati akashindwa, hili
gazeti raha yao wanataka wasikie mahakama imemkataa Mkuu wa Mkoa,
hawaoni mateso ya wanachi wala kuyaripoti.
“Sasa
aelewe tu kwamba hawatafanikiwa, nimeangalia nikabaini kuna ardhi moja
bosi wao aliichukuaga, ipo tu limebaki poli katika eneo moja katika
Wilaya ya Ubungo, tutaangalia taratibu angalau tuwapatie watu lijengwe
soko la kisasa pale,” alisema Makonda bila kutaja ni gazeti gani.
Makonda: Kuna gazeti moja kazi yake ni kunichonganisha
Reviewed by RICH VOICE
on
Februari 15, 2018
Rating:
Hakuna maoni