Ajali Ya Lori Yaua 7 Kigoma


Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania iliyotokea katika Kijiji cha Mkongoro, Barabara ya Manyovu Wilaya ya Kigoma Vijijini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko.

Amesema ajali hiyo imetokea jana Jumatano Machi 21, saa tatu asubuhi katika Mlima wa Kasagamba ambapo lori lenye namba T741AAB  lilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwamo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Siri Hamis (43) mkazi wa Singida pamoja na utingo wake aliyefahamika kama Ramadhani Saidi (23).

“Katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na watatu wanamume ambapo wengine waliofariki na majina yao hayakufahamika mara moja.

“Ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 ), aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea,” amesema Kamanda Otieno.
Ajali Ya Lori Yaua 7 Kigoma Ajali Ya Lori Yaua 7 Kigoma Reviewed by RICH VOICE on Machi 22, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...