Ronaldo, Mourinho na kocha wa Monaco washinda tuzo Ureno





Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho usiku wa jana katika mji wa Lisbon wamefanikiwa kushinda tuzo zilizotolewa na shirikisho la soka la Ureno
Ronaldo, 33, ameshinda tuzo hiyo mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo kwa kuwabwaga wachezaji wenzake wengine wa Ureno akiwemo Bernardo Silva (Manchester City) na golikipa Rui Patricio (Sporting CP).

Naye Mourinho ameshinda tuzo ya Vasco de Gama kutokana na kufanya kazi yake kwa ubora na majukumu yake kama ubalozi wa Ureno.
Wakati huo huo kocha wa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa, Leonardo Jardim ameshinda tuzo ya kocha bora kwenye upande wa soka wa wanaume.
Ronaldo, Mourinho na kocha wa Monaco washinda tuzo Ureno Ronaldo, Mourinho na kocha wa Monaco washinda tuzo Ureno Reviewed by RICH VOICE on Machi 20, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...