Lewis Hamilton kinara majaribio ya Australian GP, awafunika Ferrari na Red Bull

Dereva wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton ameibuka kinara kwenye majaribio ya magari kabla ya kuanza kwa mashindano ya Australian GP yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi leo Machi 23 siku ya Ijumaa.

Hamilton ameibuka kinara mara mbili kwenye mashindano hayo maarufu kwa jina la Formula One (F1) msimu huu wa mwaka 2018 na kuwazidi washindani wake wakubwa Ferrari na Red Bull.

Hakuna wakutuzuia kuweka historia msimu huu – Lewis Hamilton
Licha ya kuongoza kwa magari hayo ya kampuni ya Mercedes yalipata ushindani mkubwa kwenye mbio hizo za majaribio kabla ya mashindano kutoka kwa Red Bull na Ferrari.

Bingwa huyo wa dunia wa mashindano ya Formula One, Lewis Hamilton amemaliza wa kwanza kwenye mbio hizo za majaribio akimzidi Max Verstappen wa Red Bull aliyeshika nafasi ya pili kwa sekunde 0.7.



Lewis Hamilton kinara majaribio ya Australian GP, awafunika Ferrari na Red Bull Lewis Hamilton kinara majaribio ya Australian GP, awafunika Ferrari na Red Bull Reviewed by RICH VOICE on Machi 23, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...