Serikali ya Nigeria yatamani kufanya mazungumzo na Boko Haram

Serikali ya Nigeria imesema ina mpango wa kutumia njia ya mazungumzo badala ya kutumia nguvu za kijeshi ili kuwaokoa wasichana 110 waliotekwa katika mji wa Daptch hivi karibuni pamoja na wale waliotekwa mjini Chibok mwaka 2014.

Ofisi ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari imesema ingependa kuwapata wasichana waliotekwa Chibok na Daptch wakiwa hai.

Utekaji huo ndio mkubwa zaidi kufanywa na kundi la wanamgambo la Boko Haram lenye itikadi kali ya Jihadi, tangu lilipowateka wasichana wa shule 270 katika mji wa chibok mwaka 2014.

Hata hivyo, taarifa iliyowahi kutolewa na vyombo vya habari vya kiusalama ilidai kuwa takribani wasichana 100 waliachiliwa huru na Boko Haram baada ya kulipwa fidia na serikali.
Serikali ya Nigeria yatamani kufanya mazungumzo na Boko Haram Serikali ya Nigeria yatamani kufanya mazungumzo na Boko Haram Reviewed by RICH VOICE on Machi 14, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...