Mhadhiri alinganisha ziwa la mama na tikitimaji India

Waandamanaji wakishikilia tikiti maji mkononi kutokana na matamshi ya Profesa
Wanafunzi katika chuo cha taasisi cha Farook kusini mwa India katika jimbo la Kerala wamekuwa wakiandamana baada ya profesa mmoja kulinganisha titi la mwanafunzi na tikitimaji.
Kanda ya video iliyorekodiwa ya maoni ya watu kuhusu tamko la mhadhiri huyo ilisambazwa mtandaoni na watu wengi walitoa maoni ya kughadhabishwa.
Wengine waliandamana barabarani wakiwa wamebeba vipande vya tunda la tikitimaji mikononi.
Wanawake wengine waliweka mtandaoni picha zao bila mavazi kutoka kiunoni kwenda juu wakiwa wameshikilia tikitimaji ili kuelezea dhiki ambazo wanawake wazipitia wanapoambiwa kila wanachostahili kuvalia.
Video inayomuonyesha Profesa Jouhar Munavvir T, ambaye anafanya kazi katika chuo cha taasisi cha Farook kilichoko kaskazini mwa Kerela katika mji wa Kozhikode, imesambazwa sana kwenye mitandao wa kijamii baada ya kuchapishwa kwenye tovuti ya Dool News.
Kwenye rekodi hiyo, Pro Munavvir T amewalaumu wanafunzi wanawake ambao hujifunga mitandio vichwani, na kuwacha sehemu ya kifua chao wazi , sehemu aliyoitaja kuwavutia wanaume endapo haitafunikwa.
''Ni kama kipande cha tikitimaji, kilichokatwa kuonyesha jinsi tunda hilo lilivyoiva.''
Tikiti
Baada ya video hiyo kusambazwa na maelfu ya watu, watu walianza kuandamana katika barabara za Kozhikode wakiwa wameshikilia vipande vya tikitimaji na mabango wakitoa malalamiko yao kuhusu matamshi ya profesa huyo
Muungano wa wanafunzi kutoka mirengo tofauti ya kisiasa walishiriki kwenye maandamano hayo.
''Ni udhalilishaji dhidi ya wanawake wote. Katika jimbo kama la Kerala matamshi kama hayo hayawezi kukubalika,'' Nikhil Oambaye ni katibu wa Democratic Youth Federation huko India, ameiambia idhaa ya Kihindi ya BBC.
Mwanamke mmoja, Aarathi S.A ameiambia BBC: "'Nimeweka picha yangu bila nguo ya juu kwa sababu watu wanachukulia mwili wa binadamu kama chanzo kikuu cha kujamiiana.
"Iwapo mtu atavalia sari, kila mara mtu ana wasiwasi kwa sababu hakuna sehemu ya mwili inayostahli kuonekana. Watu hutunyanyasa iwapo tunaonyesha sehemu yoyote ya miili yetu.''

Aarathi anaeleza kuwa tangu kuchapishwa kwa picha hizo bila nguo ya juu "nimeitwa 'Malaya' huku wengine wakisema kwamba uamuzi wangu ni bora.''
Rehana Fathima, ambaye pia alichapisha picha yake bila nguo ya juu akiwa ameshikilia tikitimaji, ameongeza: ''Ni mwili wangu, na haki yangu. Profesa anawafanya wanawake kama chombo.''
Mwanamke mmoja aliuliza kwa nini watu hawaangazii akili ya msichana ambaye husoma kwa ukamilifu, "ama wale ambao wana uwezo wa kuimba vyema, kuandika mashairi, kunengua vyema na kushinda medali.''
Maoni ya wengi kwenye mitandao waliyakashifu matamshi ya profesa.
Mtumiaji anayehusishwa na muungano wa umoja wa Waislamu, amesema matamshi ya profesa huyo yalieleweka nje ya mada.
Huku wakosoaji wengine wa maandamano hayo wakiuliza iwapo muungano wa wanafunzi wana lengo la kuzingatia.
BBC imejaribu kuwasiliana na washika dau wa chuo cha taasisi cha Farook kwa kupata maoni yao lakini hawajapata majibu yoyote.

Mhadhiri alinganisha ziwa la mama na tikitimaji India Mhadhiri alinganisha ziwa la mama na tikitimaji India Reviewed by RICH VOICE on Machi 21, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...