MEYA MANISPAA ILALA AONGOZA MAZISHI YA MAMA YAKE KUMBILAMOTO


Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akitoa salamu za pole za Manispaa ya Ilala kwa wafiwa wakati wa msiba wa Mama yake Naibu Meya Omary Kumbilamoto.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwa katika majonzi wakati wa kumzika mama yake Mzazi Mwanaisha Omary katika makaburi yaliyopo kijijini kweao Kauzeni Wilaya ya Kisarawe mkoani pwani.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro akitoa salamu za pole za ofsi ya Mkuu wa Wilaya kwenye msiba wa mama yake Naibu Meya wa Manispaa hiyo , Omary Kumbilamoto.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum,akitoa mawaidha wakati wa msiba wa Mama yake Naibu Meya
Waombolezaji wakiswalia mwili wa Marehemu Mama yake Naibu Meya wa Mwanaisha Omary Kumbilamoto katika ibada iliyofanyika nyumbani kwa Naibu Meya Vingunguti Dar es Salaam.
waombolezaji wengine ambao ni Dada zake Naibu Meya Wa Manispaa ya Ilala wakiwa katika majonzi mazito.
Mkuu wa Kikosi Cha Anga 622, Canala Haule akitoa salamu za pole kwa familia hiyo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambapo mmoja wa mtoto wa marehemu anafanyakazi jeshini.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akitoa pole kwa wafiwa katika msiba wa Mama yake Niabu Meya wa Manispa aya Ilala, Mwanaisha Omary.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa waliofika kumfariji Naibu wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto
waombolezaji wakiwa wanahuhifadhi mwili wa Marehemu Mwanaisha Omary Kumbilamoto Kaburini.
MEYA MANISPAA ILALA AONGOZA MAZISHI YA MAMA YAKE KUMBILAMOTO MEYA MANISPAA ILALA AONGOZA MAZISHI YA MAMA YAKE KUMBILAMOTO Reviewed by RICH VOICE on Machi 21, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...