Leo ni siku ya furaha duniani, Fahamu njia 4 zitakazokufanya uishi kwa furaha siku zote


Tokeo la picha la watu wenye furahaKila mwaka Tarehe 20 mwezi Machi Dunia inaadhimisha siku ya furaha duniani na kwa mwaka huu Tanzania inatajwa kuwa ni moja ya nchi zisizo na furaha duniani, ambapo kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zinaitaja Tanzania kuwa nchi ya 153 duniani kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti huo.

Hali ya kukosa furaha wataalamu wa masuala ya afya ya akili wanasema kuwa inapelekea kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukizika hivyo kupelekea mtu kufupisha maisha yake.
Kama unaamini kuwa unakosa furaha kutokana na ugumu wa maisha, huna kazi, unasumbuliwa na mahusiano yako au umefeli kwenye masomo, umetengwa kwenye familia, umekosa mke/mume wa kuoa,  unatafuta mtoto lakini hupati n.k, basi huo ni ugonjwa na unahitaji ubadilike kwani hata ukifanikiwa kuvipata vitu hivyo unavyovihitaji kamwe furaha yako haiwezi kukamilika, Hii ni kutokana na tabia za asili za binadamu.
Hata kama ukipata furaha baada ya kufanikiwa vitu hivyo yaani kwa mfano; upate kazi, upate, mtoto n.k, kunaweza kukufanya uwe na furaha, lakini furaha hiyo huenda isidumu.
Kwa wataalamu wa masuala ya Saikolojia wanasema furaha ya kudumu haitegemei mafanikio au vitu ulivyo navyo. Bali furaha ya kweli inategemea mambo mengine zaidi ili kuweza kuwa na furaha ya kudumu.
1-UPENDO/MAHUSIANO MEMA
Ili uwe na furaha ya kudumu katika maisha yako jifunze kuwa na upendo au mahusiano mema na watu wanaokuzunguuka kwenye jamii yako hii itakufanya uongeze furaha kwenye maisha yako hata kwenye vitabu vya dini hilo limesisitizwa kuwa “Mpende jirani yako kama unavyojipenda”.
Kwa mujibu wa kitabu cha Social Psychology kimeeleza kuwa ikiwa watu wana uhusiano mzuri miongoni mwao, jambo hilo linaweza kuwafanya wafurahie maisha hata kuliko furaha inayopatikana kwa kuwa na kazi, mshahara mnono, kuwa maarufu katika jamii. Kwa ufupi, ili binadamu awe na furaha ya kweli, wanahitaji kupendana .
2- KUKATA TAMAA
Ili uweze kuwa na furaha ya kudumu epuka kukata tamaa au kukatishwa tamaa na mtu, kwa sababu kitendo cha kuruhusu kukataa tamaa ni hatua ya mwisho ambayo hauna uwezo wowote wa kujinasua kimwili au kiakili, usiruhusu hali hiyo jitahidi kuishi kwenye mtazamo chanya muda wote kuwa utafanikiwa kila jambo unalopigania hata kama ukifeli usikate tamaa hii itakufanya uwe mpambanaji na kuifariji nafsi.
Jifunze kuwa mpambanaji na jiepushe na watu ambao watakufanya uwe na furaha muda wote na sio wale wanaokukatisha tamaa kwa kila jambo. Ukirejea katika vitabu vya dini vinaeleza kuwa mtu mwenye furaha ni yule anayeendelea kuvumilia jaribu.
3-EPUKA WIVU NA TAMAA
Kwa mujibu wa kitabu cha Encyclopedia of Social Psychology mtu huwa na mwelekeo wa kumuonea wivu mwenzake ambaye wanalingana naye, huenda katika umri, uzoefu, biashara, kipato, elimu au hata mshahara. Kwa mfano, si rahisi kwa mchezaji wa mpira kumuonea wivu msanii wa muziki Lakini huenda akamwonea wivu mchezaji mpira mwenzake mwenye mafanikio kuliko yeye.
Hata utkirejea katika maana ya neno wivu ni “uchungu au kinyongo kinachotokana na kutambua kwamba mwingine ana kitu ambacho huna, na pia tamaa ya kutaka kuwa na kitu hicho.”
Kwa hiyo ili uweze kuishi kwa furaha ni vyema ukaepukana na wivu kwani itakufanya uwe mwenye furaha na kuamini kwa hicho unachokifanya otherwise utajikuta unaumia roho kwa mafanikio ya watu wengine na kukosa furaha.
4-KUWA MTU WA KURIDHIKA
Katika maisha hakuna pointi ambayo mwanadamu utafika na kusema kuwa umeridhika hii ni kwa mujibu wa vitabu vya Uchumi na vile vile vya masuala ya mahusiano, hivyo kama hutajifunza kukubali kuridhika kwa hicho kidogo unachokipata kamwe hutaweza kuwa na furaha kwani hata kikubwa utaendelea kupoteza furaha kwa kuhitaji kikubwa zaidi.
Kuna baadhi ya misemo inadhirisha hili “Anayependa fedha hatatosheka na fedha, wala anayependa mali hatatosheka na mapato.”.
Kwa mantiki hiyo hata ukiwa kwenye ndoa haimaanishi kuwa mwanamke/mwanaume aliyekuoa ni mzuri zaidi duniani jibu hapana wapo wengi wazuri, lakini ili uweze kudumu naye hauna budi kuridhika naye na kumuona wa kipekee. Hiyo itakufanya uwe na furaha kwenye maisha yako ya ndoa na vivyo hivyo hata kwa wale ambao hawapo kwenye ndoa ni lazima ujifunze kuridhika kwa kile unachokipata ili kukaribisha furaha.
Fahamu kidogo kuhusu siku ya Furaha duniani;
Siku ya kimataifa ya Furaha duniani ilitangazwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2012 kwa kutambua umuhimu wa furaha kwa ustawi wa maisha ya mwanaadamu na kufikia malengo ya ustawi wake.
Furaha ni moja ya msingi wa juhudi za binadamu kuishi katika hali nzuri ya uhai wake, kwa maana nyingine furaha hurefusha umri.
Katika kutambua umuhimu wa furaha na ustawi kama malengo na matarajio katika maisha ya binadamu, mwaka 2012 baraza la Umoja wa mataifa lilitangaza Machi 20 kuwa siku ya kimataifa ya furaha.
Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku ya kwanza ya furaha ulimwenguni, Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, aliwataka watu kushinikiza ahadi ya umoja wa maendeleo ya binadamu na kuanza upya juhudi ya kusaidia wengine.
Leo ni siku ya furaha duniani, Fahamu njia 4 zitakazokufanya uishi kwa furaha siku zote Leo ni siku ya furaha duniani, Fahamu njia 4 zitakazokufanya uishi kwa furaha siku zote Reviewed by RICH VOICE on Machi 20, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...