SIMBA SAFARINI, WANAWAFUATA NJOMBE MJI LAKINI WATAWEKA KITUO


Msafara wa kikosi cha Simba unatarajiwa kuondoka Jumamosi hii kuelekea Iringa kwa ajili ya kuweka kambi kabla ya mchezo wao dhidi ya Njombe Mji FC, Jumanne ijayo.
Simba itakuwa uwanjani kukipiga na timu hiyo ikiwa ni mchezo wao wa 21 katika Ligi Kuu ya Vodacom.
Mchezo huo utaifanya Simba kuwa michezo sawa na Yanga ambao tayari wanalingana pointi lakini Simba wapo kileleni kutokana na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kwamba Simba itakuwa Iringa Jumamosi hadi mapema Jumatatu itakaposafiri kwenda Njombe.
Kuna uwezekano wa Simba kumkosa kiungo wake, Jonas Mkude ambaye aliumia kifundo cha mguu wiki hii mazoezini Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam
SIMBA SAFARINI, WANAWAFUATA NJOMBE MJI LAKINI WATAWEKA KITUO SIMBA SAFARINI, WANAWAFUATA NJOMBE MJI LAKINI WATAWEKA KITUO  Reviewed by RICH VOICE on Machi 30, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...