Haji Manara Aingilia Kati Sakata la Diamond na Naibu Waziri


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amefunguka na kumkingia kifua msanii Diamond na wenzake ambao wamekuwa wakitetea haki zo kwa Naibu waziri ambae ameibuka na sera ya kuwafungia wasanii kwa madai kuwa wanaimba nyimbo zisozokuwa na maadili katika jamii.

Hivi karibun Diamond aliongea katika media moja na kusema kuwa hata kama atatakiwa kulala jela kwa sababu ya muziki basi atafanya ilimradi kutetea haki ya muziki kwa sababu watu wanaofungia muziki huo hawajui historia ya muziki wala msanii wanaemfungia.

Haji Manara amesema  kuwa pamoja na kwamba wasanii wanaweza kuwa wamefanya kosa lakini wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la pili na kwa upande wa Diamond ni msanii mkubwa mbaye amekuwa akiiwakilisha nchi katika mambo mbalimbali.
 
"Ngoja na mimi nispitwe na hili..inawezekana kuwa kama binadamu anaweza kuwa amekosea , lakini inabidi tutambua kuhusu muziki wa kisasa na soko lake linataka nini..by the way diamond na wenzie tunawatumia sana katika maswala ya kijamii  na hata kampeni zetu za kisiasa,na huyu ni brand kubwa ,,,walau tufanye staha kidogo na tujitaidi tupende vya kwetu.

NB.mimi napenda muziki mzuri sina cha timu wala cha baba yake na timu….hawakawii wabongo. @diamondplatinumz"

Haji Manara Aingilia Kati Sakata la Diamond na Naibu Waziri Haji Manara Aingilia Kati Sakata la Diamond na Naibu Waziri Reviewed by RICH VOICE on Machi 21, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...