WAMBURA KUTINGA TFF JUMAMOSI ASUBUHI TU, KAMATI INAMSUBIRI


Kaimu Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo aliweka wazi juu ya suala hilo juzi kwa kusema: “Kamati itakutana Jumamosi Machi 31 saa tano asubuhi, pamoja na mambo mengine pia itasikiliza rufaa ya Michael Wambura ambaye alikata rufaa
Ndipo alisema Wambura anaruhusiwa kufika kutoa utetezi wake kwa njia ya mdomo, maandishi au kuleta vielelezo vyote vya utetezi wake pia anaweza kuleta mwakilishi akiwa na barua ya uwakilishi au anaweza kuamua kutokuja kabisa.
Naye wakili wa Wambura, Emmanuel Muga alisema mteja wake amepokea wito kutoka kamati ya rufaa ya maadili na atakwenda kutetea haki yake mbele ya kamati hiyo.
Upande wa Wambura mwenyewe amesema yupo tayari kwenda kutetea haki yake mbele ya kamati na ana hoja zake na amethibitisha kwamba atakwenda.
WAMBURA KUTINGA TFF JUMAMOSI ASUBUHI TU, KAMATI INAMSUBIRI WAMBURA KUTINGA TFF JUMAMOSI ASUBUHI TU, KAMATI INAMSUBIRI Reviewed by RICH VOICE on Machi 30, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...