Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli


Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (Tuico), kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi), yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Arusha.

Mwenyekiti wa Tuico taifa, Paulo Sangeze, alisema, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.

Akizungumza katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu, iliyowashirikisha viongozi wa matawi mbalimbali ya  Tuico mwishoni mwa wiki, iliyofanyika jijini hapa, Mwenyekiti wa Tuico taifa, Sangeze, alisema Shirikisho la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limekiteua chama chao kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi kwa mwaka huu.

Alisema baada ya kupewa fursa hiyo wanafanya vikao vya maandalizi na tayari wamepanga maadhimisho hayo kwa mwaka huu, yatafanyika mkoani Arusha katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

Katibu wa Tuico, Boniface Nkakatisi, alisema maandalizi hayo yanaenda na mialiko ya wageni watakaohudhuria ikiwamo wafanyakazi mbalimbali nchini, wanachama  wa Tuico, mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli Reviewed by RICH VOICE on Machi 21, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...