Man Walter aeleza Alikiba kuja na ngoma kubwa kuzidi Seduce Me

Producer kutoka studio za Combination Sound, Man Walter amefunguka kuhusu ujio mpya wa mwanamuziki Alikiba.

Akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio Man Walter amesema ngoma ambayo amefanya na Alikiba endapo muimbaji huyo ataitoa itakuwa kubwa kuzidi Seduce Me.
“Baada ya Seduce Me kuna ngoma tumefanya na imeshafanyika video nilivyosikia, kama ndio hiyo itakuwa next track baada ya Seduce Me, pale tuliwaambia ile ni statrr kwa hiyo sasa ndio tunapakuwa msosi wale,” amesema.
Man Walter amekuwa na historia ya aina yake katika muziki wa Alikiba kwani kila msanii huyo anapokaa kipindi kirefu bila kutoa ngoma producer huyo amekuwa akifanikisha comeback yake, alifanya hivyo katika ngoma ya Mwana na Seduce Me.
Man Walter aeleza Alikiba kuja na ngoma kubwa kuzidi Seduce Me Man Walter aeleza Alikiba kuja na ngoma kubwa kuzidi Seduce Me Reviewed by RICH VOICE on Machi 20, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...