Cristiano Ronaldo atuzwa kuwa mchezaji bora wa kiume 2017 duniani

Cristiano Ronaldo

Haki miliki ya pichaEPA
Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu kwa mara ya pili mtawalia.
Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.
Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Aliwashinda Lionel Messi wa Barcelona na mchezaji ghali zaidi duniani anayechezea Paris St-Germain, Mbrazil Neymar.
Messi alimpigia kura mwenzake wa Barcelona Luis Suarez naye Ronaldo alimpigia mwenzake wa Real - Luka Modric.
Meneja wa England Gareth Southgate alimpigia kura Ronaldo.

Ufanisi kwa Cristiano Ronaldo

Ulikuwa ni mwaka mwingine wa ufanisi kwa Ronaldo, aliyekuwa ameshinda tuzo ya kwanza ya Mchezaji Bora wa Fifa kwa mwaka 2016.
Aliendeleza ufanisi wake kutoka mwaka uliopita alipowaongoza Ureno kushinda Euro.
Mwaka huu, alifunga mabao mawili katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Juventus ambapo walishinda 4-1.
Alifungia klabu hiyo mabao 25 katika mechi 29 alizowachezea na klabu yake ilifanikiwa kushinda La Liga kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano.
"Tumefika England kwa mara ya kwanza, na nashinda tuzo hii kwa mara ya pili mtawalia. Huu ni wakati mzuri sana kwangu," Ronaldo alisema wakati wa sherehe za kutangaza washindi London Palladium.
Wachezaji watatu bora
Cristiano Ronaldo - 43.16 %Lionel Messi - 19.25 %Neymar - 6.97%
Lieke MartensHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLieke Martens
Alipokea tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.
Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.
Aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017.
Martens aliwashinda Carli Lloyd, mshindi wa mwaka 2016 anayetoka Marekani United States na Deyna Castellanos wa Venezuela ambaye ana miaka 18 pekee.

Kuna tofauti ya Ballon d'Or na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fifa?

Huu ulikuwa mwaka wa pili kwa Tuzo za Mchezaji Bora wa Fifa kutolewa, na ni tofauti na tuzo ya Ballon d'Or.
Ballon d'Or imekuwa ikitolewa na jarida la soka la Ufaransa tangu 1956, na kwa muda mrefu kwa ushirikiano na Fifa.
Lakini Fifa walihitimisha ubia huo mwaka jana na badala yake wakaanzisha tuzo zao binafsi.
Ronaldo alishinda tuzo ya kwanza kwa mwaka 2016 na kukabidhiwa Januari.
Mchezaji bora na meneja bora hupigiwa kura na manahodha wa timu za taifa na mameneja, wanahabari kadha, na kwa mara ya kwanza mwaka huu mashabiki walipiga kura kupitia mtandao.
Kila kitengo cha kura hujumuisha asilimia 25 ya kura zote.
Wachezaji wengine wa kiume waliokuwa wanashindania tuzo hiyo ni:
4: Luka Modric (Croatia, Real Madrid)
5: Toni Kroos (Germany, Real Madrid)
6: Paulo Dybala (Argentina, Juventus)
7: Sergio Ramos (Spain, Real Madrid)
8: Kylian Mbappe (France, Monaco)
9: Robert Lewandowski (Poland, Bayern Munich)
10: Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Manchester United)

CHANZO :BBC SWAHILI.

Cristiano Ronaldo atuzwa kuwa mchezaji bora wa kiume 2017 duniani Cristiano Ronaldo atuzwa kuwa mchezaji bora wa kiume 2017 duniani Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 24, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...