Hakuna mrithi wa Rais Xi Jinping wakati viongozi wapya wanateuliwa China


China"s new Politburo Standing Committee members
Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Xi Jinping na wanachama wa kamati kuu
China imetangaza kamati mpya ya viongozi wakuu na kuachana na mila ya kutomtangaza mrithi wa rais Xi Jinping.
Kutotangazwa mrithi kunaashiria kuongezeka ushawishi wa Xi madarakani katika kipindi cha miaka mitano inayokuja, siku moja baada ya jina lake kujumuishwa katika katiba.
Uteuzi huo ulifanywa kwa kamati ya watu inayojulikana kama Politburo, ambayo ina nguvu zaidi nchini China.
Kamati hiyo mpya ilizinduliwa kwenye ukumbi mashuhuri wa watu wa China.
Kando na Xi mwenye umri wa miaka 64, waziri mkuu Li Keqiang, 62, ndiye mwanachama pekee wa kamati ambaye alidumisha nafasi yake.
Viongozi wa China miongo ya hivi karibuni wamekuwa wakimteua mrithi mmoja ua kadhaa katika kamati kuu, wakati wa kuanza kwa muhula wa mwisho kuonyesha warirhi watakaochukua usukani.
Standing committee
Image captionViongozi wapya nchini China
kumekuwa na uvumi kuwa Bw Xi anaweeza kuwainua wanachama Chen Miner na Hu Chunhua, wote ambao wana umri wa miaka ya 50 kuweza kuwa warithi wake.
Kamati kuu ya kijehi nayo ilitangazwa. Itaongozwa na Xu Qiliang ambye anadumisha cheo hicho na Zhanga Youxia mshirika waa karibu wa Bw. Xi.
Wajumbe pia waliteua kamati kuu ya nguvu ya wanachama 200 ambao hukutana mara mbili kwa mwaka.
Mashirika ya habari ya kimataifa likiwemo la BBC yalinyimwa vibali vya kuingia ukumbi wa matangazo.
Hatua ya kutoteuliwa kwa warithi wa kamati kuu inampa nguvu zaidi Bw Xi katika miaka mitano inayokuja na kuashiria kuendelea kuwepo kwake baada ya mwaka 2022.
Souvenir plates with images of Chinese late Chairman Mao Zedong and Chinese President Xi Jinping are seen at a shop during the ongoing 19th National Congress of the Communist Party of China, in Beijing, China 21 October 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMabadiliko ya katiba yanamweka Xi (kushoto) kiwango kimoja na mwanzilishi Mao Zedong (kulia)
Hakuna mrithi wa Rais Xi Jinping wakati viongozi wapya wanateuliwa China Hakuna mrithi wa Rais Xi Jinping wakati viongozi wapya wanateuliwa China Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 25, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...