Eden Hazard ainusuru Chelsea katika sare ya 3-3 dhidi ya Roma


Eden Hazard akifunga mojawapo ya mabao yake mawaili dhidi ya AS Roma
Image captionEden Hazard akifunga mojawapo ya mabao yake mawaili dhidi ya AS Roma
Eden Hazard aliwaokoa Chelsea's kuendeleza msururu wao wa kutofungwa katika kombe la vilabu bingwa baada ya Roma waliotawala mechi hiyo kutoka nyuma na kuongoza katika kiputi kilichojaa mbwembwe za kila aina katika uwanja wa Stamford Bridge.
Hazard alifunga bao kila kipindi cha mchezo ,mwanzo akifunga kichwa kilichosawazisha matokeo kufuatia krosi ya Pedro zikiwa zimesalia dakika 15 mechi kukamilika katika kundi C.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alikuwa ameipatia Chelsea uongozi wa mabao mawili katika kipindi cha kwanza baada ya David Luiz kuiweka Chelsea kifua mbele.
Lakini timu hiyo ya ligi ya Serie A iling'ang'ana huku Aleksandar Kolarov akifunga kabla ya Edin Dzeko kufunga mabao mawili katika dakika sita.
Shambulizi lake la kwanza ulikuwa mpira uliompita kwa juu kipa huku la pili likiwa mchezo mzuri wa nipa ni kupe kati ya Kolarov.


Eden Hazard ainusuru Chelsea katika sare ya 3-3 dhidi ya Roma Eden Hazard ainusuru Chelsea katika sare ya 3-3 dhidi ya Roma Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 19, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...