Diane Rwigara amwomba Rais Kagame afuenz

Rwanda

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDiane Rwigara kiongozi wa upinzani nchini Rwanda
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara amemwomba Rais Paul Kagame kumuachilia yeye, mamake na dadake.
Akiwa mahakamani, Bi Rwigara amesema kwamba serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.
Wanawake hao watatu, ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi tuhuma ambazo wameziita zenye mrengo wa kisiasa.
Bi Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa Rwanda, Uchaguzi ambao Bwana Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa.
Diane Rwigara amwomba Rais Kagame afuenz Diane Rwigara amwomba Rais Kagame afuenz Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 16, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...