Wafuasi wa Odinga wachoma matairi Kisumu

Katika maeneo mengi Kisumu, mji ambao ni ngome ya Raila Odinga, wakazi wamefunga barabara na kuchoma matairi.

Mwandiswa BBC Alistair Leithead anasema hajashuhudia kituo chochote ambapo upigaji kura unaendelea.
Ametutumia picha hii:
Kisumu
BBC

HABARI ZA HIVI PUNDEKenyatta apiga kura Kiambu

Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee amepiga kura yake katika eneo la Mutomo, Gatundu katika kaundi ya Kiambu.

Wakazi wafunga barabara Bangladesh, Mombasa

Wakazi katika mtaa wa Bangladesh eneo la Jomvu mjini Mombasa wamefunga barabara za kuelekea kwenye vituo vya kupigia kura.
Wamekabiliana na polisi waliokuwa wakijaribu kuwatawanya.
Bangla
BBC
Bangla
BBC
Bangla
BBC

Heri ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Kenyatta

Rais Kenyatta anatimiza miaka 56 hivi leo. Alizaliwa siku sawa na ya leo mwaka 1961.
Watoto hawa wamekuwa kwenye kituo cha kupigia kura cha Mutomo, ambacho ndicho Bw Kenyatta, wakiwa na fulana zenye ujumbe wa kumtakia heri siku ya kuzaliwa kwake.
Mama yao Joan Wamaitha amemwambia mwandishi wa BBC Anthony Irungu kuwa: "Walitazama video ya heri ya siku ya kuzaliwa ya rais na wakasisitiza wapate fulana hizi na wamsalimie Rais Kenyatta."
Heri ya siku ya kuzaliwa
BBC

Mavazi ya bendera Gatundu

Familia hii imefika katika kituo cha kupigia kura cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu na mavazi ya kipekee - mavazi ya rangi za bendera ya Kenya.
Rais Kenyatta amejiandikisha kupigia kura katika kituo hicho na anatarajiwa kupiga kura baadaye leo.
Bendera
BBC

Naibu Rais William Ruto apiga kura Eldoret

Naibu Rais William Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta, amepiga kura yake katika kituo cha shule ya msingi ya Kosachei eneo la Turbo mjini Eldoret magharibi mwa Kenya.
Ruto akipiga kura
BBC
Ruto foleni
BBC
Ruto akiwa kwenye foleni
Kituo hicho watu wamejitokeza kwa wingi
BBC
Kituo hicho watu wamejitokeza kwa wingi

Wapiga kura wavumilia mvua na baridi kali Kiambu

Wapiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Kimbo katika eneo la Githurai 45, Kiambu wamevumilia mvua na baridi kali kwenye foleni kusubiri fursa ya kupiga kura.
Mvua imenyesha katika maeneo mengi Kenya usiku wa kuamkia leo.
Mvua Githu
BBC
Mvua
BBC
Mvua Githu
BBC

Siku ya kuzaliwa kwa Rais Kenyatta

Leo ni siku ya marudio ya uchaguzi na pia ni siku sawa na aliyozaliwa Rais Uhuru Kenyatta mwaka 1961.
Baadhi ya idara za serikali zimechukua fursa hii kumtumia salamu za heri.

Wafanyakazi wa IEBC wakosa kufika vituoni Kisumu

Katika baadhi ya maeneo Kisumu, ngome ya Raila Odinga, baadhi ya wafanyakazi wa tume ya uchaguzi waliofaa kuendesha uchaguzi wa leo hawajafika vituoni bado.
Msimamizi wa uchaguzi kituo cha shule ya sekondari ya Lions High ameambia BBC kwamba kati ya wafanyakazi 399 eneo hilo, ni watatu pekee waliojitokeza.
Masanduku ya kupigia kura pamoja na vifaa vingine vya uchaguzi vinaendelea kuandalwia.
Kituo
BBC
Vituo kuandaliwa
BBC

IEBC: Upigaji kura vituo vingi ulianza vyema, kwingine muda utaongezwa

Tume ya taifa ya uchaguzi IEBC imesema vituo vingi vilifunguliwa kwa wakati, saa kumi na mbili asubuhi.
Vituo ambavyo vilichelewa kufunguliwa, muda utaongezwa baadaye jioni.
Ripoti

Kituo cha Olympic, Kibera chafunguliwa

Lango la kuingia kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Olympic katika mtaa wa Kibera, Nairobi lilikuwa imefungwa kwa minyororo.
Lakini maafisa wa polisi wamefanikiwa kuvunja minyororo hiyo na sasa kituo hicho kimefunguliwa.
Ripoti

Kisumu Lions hakuna mpiga kura hata mmoja

Katika kituo cha Shule ya upili ya Lions, kufikia saa moja na robo vifaa vya kupigia kura vilikuwa vinawasilishwa kituoni wakati huo.
Hakukuwa na mpiga kura hata mmoja kituoni.
Lions
BBC
Lions
BBC

Hali ilivyo mji mkuu wa Nairobi

Mwandishi wa BBC David Wafula amekuwa katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Moi Avenue, katikati mwa jiji la Nairobi.
Tazama video hii kuhusu hali ilivyo:

Nakuru upigaji kura unaendelea

Mwandishi wetu Robert Kiptoo yupo mjini Nakuru ambapo shughuli ya upigaji kura inaendelea ambapo sawa na kwingine, idadi ya waliojitokeza si sawa na ya waliojitokeza uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.
Nakuru
BBC
Nakuru
BBC

Wafuasi wa Odinga wachoma matairi Kisumu Wafuasi wa Odinga wachoma matairi Kisumu Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 26, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...